Field Marshal, ni juzi juzi tu hapa uliongelea kuhusu ulichokiita nanukuu "tabia chafu za kutembea na wake za watu", sitaki kuiweka hiyo posti hapa, lakini ni wakati ule wa kudiscuss issue kati ya Mwalimu na Malecela baada ya kutokea msiba wa mwanamama mmoja(jina nalihifadhi), ukiitaka hiyo posti nitakuwekea hapa maana ipo mkuu. sasa sijui unalichukuliaje mme wa mtu kutembea na wanawake wengine nje ya ndoa yake!.na pia mara kadhaa umekuwa ukirejea biblia kujenga hoja zako(rejea ishu ya uchawi ) ulipodai kuwa biblia unayoiamini imesema uchawi upo kwa hiyo nawe unaamini upo.sasa mimi nakushangaa unaposimama kutetea upuuzi huu wa kimaadili wa viongozi wetu kwa madai eti "maadamu hajala pesa zetu basi hilo halituhusu", kweli mkuu unaweza kusimama kwenye kioo na kutamka hayo maneno kisha ukaridhika na moyo ukatulia kisha ukalala usingizi safi?, hivi kweli Biblia unayoiamini inatufundisha kwamba Binadamu anaweza kuishi kwa mkate pekee?, yaani maadamu watanzania tunapata ka mkate ketu basi maadili mema ambayo sisi kama jamii tunayakubali, kama vile kutokwenda nje ya ndoa siyo ishu ya kukemea kwa nguvu zote hususan kwa viongozi wetu?,(nimetumia biblia kwa sababu hapo awali umeitumia kuegemeza hoja zako"). kwamba uzinzi siyo ishu?.kwamba tukiwa na kiongozi basha,hiyo siyo ishu yetu, kwamba tukiwa na kiongozi msagaji Watanzania tusikemee maadam haibi pesa yetu, kwamba tukiwa na kiongozi mwenye tabia za kubaka kuku na mbuzi Watanzania tusikemee maadamu hali pesa yetu. Jamani
Binadamu hataishi kwa mkate tu!. ndugu FieldMarshall tunajua kuwa fika Masha ni rafiki yako, na urafiki usikutie upofu ukauficha ukweli ilhali unafahamu jamaa yako amechemsha, Mwambie ajirekebishe lau kama hawezi ajiuzulu, hatuwezi kuendelea kuwapa dhamana viongozi wasiofahamu umuhimu wa kuwa na uchungu wa kulinda na kuziheshimu ndoa na familia zao,hao watu wataweza vipi kulilinda na kuliheshimu Taifa?