Lay JayDee na Nyota Ndogo wametuonesha UNAFIKI wa marafiki unavyoweza kuua biashara yako kisa urafiki

Lay JayDee na Nyota Ndogo wametuonesha UNAFIKI wa marafiki unavyoweza kuua biashara yako kisa urafiki

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
ac03c68b-709c-4d17-9ef7-fd2d7bdca488.jpg

Wiki hii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee aliamua kutoa yake ya moyoni kuhusu marafiki zake kutomuunga mkono katika biashara zake.

JayDee alisema kuwa kuna baadhi ya watu ambao hawaungi mkoni biashara yake ya chakula, lakini wakishapiga ‘vyombo’ usiku wanaanza kumpigia simu mbele za watu ili waonekana wanamjua sana.

Anasema watu hao wakishapiga vyombo vyao wakasikiliza nyimbo zake basi wanaanza sifa za kujuana wakati hawaendi kumuungisha kwenye biashara zake na wala kwenye shoo zake hawaendi.

Siku moja baada ya kauli hiyo, mkongwe mwingine wa muziki wa Kenya, Nyota Ndogo aliyewahi kutamba na nyimbo za ‘Watu na Viatu’ na ‘Nibebe’ aliomshirikisha Nonini naye ametoa povu kuhusu mashabiki wanaokwenda hotelini kwake kula na kunywa bila kulipia huduma hiyo.

"Nasema sababu naona inazidi, tuko na Mashabiki na Marafiki.... watakwambia tunatafuta hoteli yako hatujui ilipo kisha wanakuja watano au sita wanaagiza kuku, pilau, nyama na kila kitu wakishamaliza kula wanakisifu chakula wanaingia kwenye gari wanaondoka zao.

"Mnakula chakula cha karibu 4000 Ksh. (Tsh. 79,000) mimi nina Watu nataka niwalipe nina kodi pia ya nyumba ya kulipa kama nyinyi ni Marafiki hamtokuja kula bure bali mtasema mnakuja kum-suport Nyota na huo sio Urafiki ni unafiki," - amesema Nyota.
 
Ni stress tu za kufulia kimziki na kukosa kiki, huwezi kulazimisha watu wale kwenye mgahawa wako hata kama ni mashabiki, kusikiliza nyimbo zako ni support tosha wamependa mziki na siyo misosi yenu, mnawaforce wale kwenu mwisho wa siku wanakula bure.
 
Ni stress tu za kufulia kimziki na kukosa kiki,huwezi kulazimisha watu wale kwenye mgahawa wako hata kama ni madhabiki,kusikiliza nyimbo zako ni support tosha wamependa mziki na siyo misosi yenu,mnawaforce wale kwenu mwisho wa siku wanakula bure.
Suport gani kusikiza kwenye bar, waweke screenshort, wakisikiza ONLINE kwenye SPOTIFY BOOMPLAY and Co tutaona kweli wanasurpot

Wabongo unafiki mwingi wewe anaejidai rafiki yake akikupa kazi umfanyie anakupunja ELA tena sometime hakupi kabisa
sasa kazi hiyohiyo itokee wewe haupo anatotoleshwa ELA kibao na fresh
 
Tatizo mfano kwa Lady Jaydee, ukute chakula hakipikwi vizuri au si kizuri kwa ujumla, ila mziki wake ni mzuri, mimi kama rafiki yake kwanini nisipende na hata kumpigia simu nikiwa na wadau wengine, kumsifu kuhusu mziki wake?

Mimi siwezi kuja kula chakula kwako eti nakusapoti wakati yawezekana ni kibaya,nakua 'selektivu' bhana. Aboreshe huduma ya chakula na 'showz' zake pia kama hapafom vizuri.

Kuhusu huyo Nyota ndogo, kwakweli hao marafiki uchwara wanazingua, wanampa hasara, wanazingua sana, bora walipie siku hiyo, na kama hawajapenda chakula husika, wampe maoni yao, ili aboreshe au wasiende tena, ila walipe kama wamekula. Wajue analipa wafanyakazi nayeye mwenyewe anatakiwa apate kipato cha wategemezi wake hapo.

Anyway, wanamziki wa sasa, wajifunze kupitia hao ma-legend hao, inaonekana Mr. Nice hajatosha kutoa funzo.
 
Ni stress tu za kufulia kimziki na kukosa kiki,huwezi kulazimisha watu wale kwenye mgahawa wako hata kama ni madhabiki,kusikiliza nyimbo zako ni support tosha wamependa mziki na siyo misosi yenu,mnawaforce wale kwenu mwisho wa siku wanakula bure.
Basi usimpigie simu na kujidai mwamjua na hamsupport biashara zake huu ni upuuzi mtu anaenda kufaidisha mtu mwingine halafu wakishafaidisha mtu mwingine saa wameshiba wana dai oh nakujua
 
Kweli kabisa mkuu. Huwezi kumlazimisha mtu ale kwako eti kisa ni rafiki yako.

Hata mziki pia huwezi kulazimisha nikusupport kama unachoimba sijapenda, nikikusupport itakuwa kwa muda mfupi maana nasupport kitu anbacho sijapenda.
 
Basi usimpigie simu na kujidai mwamjua na hamsupport biashara zake huu ni upuuzi mtu anaenda kufaidisha mtu mwingine halafu wakishafaidisha mtu mwingine saa wameshiba wana dai oh nakujua
Hao ni mashabiki waliompendea mziki siyo chakula. Wanampenda kama mwanamziki siyo kama mama ntilie
 
Ilikua aje hi mkuu. Mbona sijawahi kusikia kuhusu hiii
Unajua chanzo cha ugomvi wa Ali kiba na TID mnyama ila cocastic atakupa mwangaza ila ilikuwa skendo kubwa sana na ulinzi wa Tabata pale mamaake ndio anaamua nani aingie akisema out hakuna mjadala.
 
Back
Top Bottom