Lay JayDee na Nyota Ndogo wametuonesha UNAFIKI wa marafiki unavyoweza kuua biashara yako kisa urafiki

Lay JayDee na Nyota Ndogo wametuonesha UNAFIKI wa marafiki unavyoweza kuua biashara yako kisa urafiki

Marafiki wengi kwa bongo ni miyeyusho tu wengi wanafiki sana wachache wako real.
Fid q alishawahi kuimba sihitaji marafiki.
 
Sawa lakini ukweli ndio huo. Watu wanasupport vitu wanavyopenda kama wanakusupport just kukusupport haiwezi kudumu itakuwa kwa muda mfupi tu maana wanakuungisha tu. Lakini kama unafanya kitu wanapenda, watakuja wao wenyewe. Usifanye kitu ili mradi ukitegemea watu wakubackup kisa wewe ni rafiki yao, backup itakuwa kwa muda mfupi tu
Amesema wale wanaompigia simu usiku wa manane wakiwa wamelewa ili kuonesha watu waliokua nao kua wanafahamiana nae sana ili hali hawa support kazi wala biashara zake,

Point yake ipo kwenye kusumbuana usiku wakati ni unafki.
 
Amesema wale wanaompigia simu usiku wa manane wakiwa wamelewa ili kuonesha watu waliokua nao kua wanafahamiana nae sana ili hali hawa support kazi wala biashara zake,

Point yake ipo kwenye kusumbuana usiku wakati ni unafki.
Binafsi nimemuelewa
 
Wiki hii mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Lady Jay Dee aliamua kutoa yake ya moyoni kuhusu marafiki zake kutomuunga mkono katika biashara zake.

JayDee alisema kuwa kuna baadhi ya watu ambao hawaungi mkoni biashara yake ya chakula, lakini wakishapiga ‘vyombo’ usiku wanaanza kumpigia simu mbele za watu ili waonekana wanamjua sana.

Anasema watu hao wakishapiga vyombo vyao wakasikiliza nyimbo zake basi wanaanza sifa za kujuana wakati hawaendi kumuungisha kwenye biashara zake na wala kwenye shoo zake hawaendi.

Siku moja baada ya kauli hiyo, mkongwe mwingine wa muziki wa Kenya, Nyota Ndogo aliyewahi kutamba na nyimbo za ‘Watu na Viatu’ na ‘Nibebe’ aliomshirikisha Nonini naye ametoa povu kuhusu mashabiki wanaokwenda hotelini kwake kula na kunywa bila kulipia huduma hiyo.

"Nasema sababu naona inazidi, tuko na Mashabiki na Marafiki.... watakwambia tunatafuta hoteli yako hatujui ilipo kisha wanakuja watano au sita wanaagiza kuku, pilau, nyama na kila kitu wakishamaliza kula wanakisifu chakula wanaingia kwenye gari wanaondoka zao.

"Mnakula chakula cha karibu 4000 Ksh. (Tsh. 79,000) mimi nina Watu nataka niwalipe nina kodi pia ya nyumba ya kulipa kama nyinyi ni Marafiki hamtokuja kula bure bali mtasema mnakuja kum-suport Nyota na huo sio Urafiki ni unafiki," - amesema Nyota.
Neno..biashara ya chakula wewe umwlitoa wapi? Yeye kaongelea muziki
 
Katika dunia ya sasa ukitaka kila mtu awe rafiki yako basi unakaribisha wanafiki na maadui watupu katika maisha yako
 
Back
Top Bottom