Lazaro Nyalandu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati

Lazaro Nyalandu amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kati

WanaJF

Habari za hivi Punde kutoka kule Kanda ya Kati zinasema Lazaro Nyalandu amechaguliwa kwa kishindo kikubwa kuongoza CDM katika kanda hiyo.

Nyalandu amepata kura 60 dhidi ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Kanda hiyo Alphonce Mbassa aliyepata kura 26.

Lazaro Nyalandu mwanasiasa mwenye hekima ya hali ya juu ambaye amewahi kuwa Waziri na mbunge kutokea CCM ushindi wake umedhihirisha ndani ya chama wanachama wote wana haki sawa hata kama umejiunga na chama hicho siku za usoni.

Kwa ushindi huu sasa Lazaro Nyalandu anaingia kwenye vikao vikuu vya maamuzi kama Mjumbe wa Kamati Kuu

Update no 2

Yafuatayo ni matokeo kwa Kanda zilizofanya ucyaguzi leo

CHAGUZI ZA KANDA - CHADEMA.

Leo kanda tano za Chadema zimefanya uchaguzi wa viongozi wake. Kanda ya Serengeti, Nyasa, Kati, Victoria na Magharibi. Katika nafasi ya Mwenyekiti matokeo ni kama ifuatavyo;

KANDA YA SERENGETI;
1. Ester Matiko - 44 sawa na 53.6%
2. John Heche - 38 sawa na 46.3%

Heche ndiye Mwenyekiti anayemaliza muda wake na ameshindwa kutetea kiti chake.

KANDA YA KATI;
1. Lazaro Nyalandu - 60 sawa na 69.7%
2. Alphonce Mbasa - 26 sawa na 30.3%

Mbassa ndiye Mwenyekiti anayemaliza muda wake na ameshindwa kutetea kiti chake.

KANDA YA NYASA;
1. Peter Msigwa - 66 sawa na 62.2%
2. Boniface Mwabuskusi - 26 sawa na 24.5%
3. Sadick Malila - 14 sawa na 13.3%

Msigwa ndiye Mwenyekiti anayemaliza muda wake na amefanikiwa kutetea kiti chake.!

KANDA YA MAGHARIBI
1. Gaston Garubindi - 39 sawa na 52%
2. Ngaza Mboje - 36 sawa na 48%

Mboje ndiye Mwenyekiti anayemaliza muda wake na ameshindwa kutetea kiti chake.

KANDA YA VICTORIA
1. Ezekiah Wenje 55 sawa na 68.7%
2. Chief Karumna 25 sawa na 31.3%

Wenje ndiye Mwenyekiti anayemaliza muda wake na amefanikiwa kutetea kiti chake.!
Nyalandu ataisaidia sana Chadema itakapokuwa haina ruzuku!
 
Njaghamba ne ahitye umusaliti muna akwe Tundu Lissu
 
Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini nchini Tanzania, Lazaro Nyalandu amechaguliwa kuwa mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati baada ya kupata kura 60 kati ya 86 zilizopigwa.

Waziri huyo wa zamani wa Maliasili na Utalii ameshinda kwa asilimia 66.8 katika uchaguzi huo uliofanyika mjini Dodoma na kusimamiwa na mwenyekiti wa Baraza la Vijana la Chadema (Bavicha), Patrick Sosopi akisaidiana na katibu mkuu wa baraza hilo, Julius Mwita.

Akitangaza matokeo hayo leo Jumapili Desemba Mosi, 2019, Sosopi amesema waliopiga kura walikuwa 86, hakuna kura iliyoharibika.

Amesema aliyekuwa mwenyekiti wa Kanda hiyo, Alphonce Mbasa amepata kura 26, sawa na asilimia 33.2.

Katika nafasi ya mweka hazina, Mbunge wa Viti Maalum, Devotha Minja ameibuka mshindi baada ya kupata kura 44 sawa na asilimia 51.2 huku mshindani wake, Tully Kiwanga akipata kura 42 sawa na asilimia 48.8.

Uchaguzi wa makamu mwenyekiti umerudiwa baada ya kukosekana mgombea aliyepata zaidi ya asilimia 50.

View attachment 1278430
Nyalandu mjanja sana,angesema anagombea kiti cha Taifa ,asingepata kura za ushindi...
 
Anastahili. Kwa muda mfupi aliojiunga, ameonekana akifanya kazi kubwa ya kukiimarisha chama na kujiimarisha yeye mwenyewe. Zilionekana wazi juhudi zake binafsi alizokuwa akizifanya.

Na huyu alijiunga CHADEMA akitokea CCM kwa namna ya pekee kidogo. Nadhani ni mtu wa pili kutoka CCM aliyeamua kuacha ubunge na marupurupu yote. Walio wengi wanajiunga na upinzani baada ya kutemwa na CCM.

Hongera sana Nyalandu. Nina imani, chini ya uongozi wa Nyalandu, kanda ya kati inaenda kubadilika, na kuongeza kanda zenye watu wenye uelewa juu ya umuhimu wa kuwa na watawala wanaoheshima katiba, sheria, haki, uhuru wa maoni na haki za kidemokrasia.

Viongozi wa CHADEMA, ni muhimu sana kutumia mbinu za chini kwa chini, kama ambavyo amekuwa akifanya Nyalandu, kuliko kutegemea mikutano ya wazi.

Nguvu kubwa itumike kuwapa watu elimu katika makundi madogo madogo. Watu wakiwa na uelewa, wakapata elimu sahihi, hakuna mtu asiye mnafiki atakayeunga upuuzi kama huu uliotokea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa.
Safi sana
 
Back
Top Bottom