Uchaguzi 2020 Lazaro Nyalandu atangaza nia ya kuwania Urais kupitia CHADEMA

Uchaguzi 2020 Lazaro Nyalandu atangaza nia ya kuwania Urais kupitia CHADEMA

CHADEMA

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
490
Reaction score
2,471


VIDEO Courtesy: CHADEMA
Lazaro Nyalandu 2020

Mabibi na Mabwana,

Ndugu Wanahabari
,

Leo natangaza rasmi azma yangu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA. Mapema asubuhi ya leo, nimemwandikia burua Katibu Mkuu wa Chama chetu, Mh. John John Mnyika nikimjulisha kusudio langu la kutia nia katika kinyang’anyiro cha kuwa Mgombea Urais kupitia CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 2020.

Nasimama mbele yenu na mbele ya umma wa watanzania, huku moyo wangu ukiwa umejaa shauku kubwa nikitamani kuiona Tanzania, nchi tuipendayo kwa moyo wote inapata ustawi na kuendeleza matamanio, matarajio na ndoto za watu wake katika kuwapatia maendeleo endevu likiwa ni Taifa linalosimamia uhuru na haki za watu, utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari,na demokrasia ya kweli inayowapa wananchi mamlaka ya juu kuhusu mustakadhi na mwelekeo ya nchi kupitia chagua zilizo huru na za haki.

Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliamini katika ulazima wa kuwaunganisha wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ili waishi katika udugu, umoja, usawa, na mshikamano katika Taifa lililo huru na lenye amani, na kuifanya Tanzania kuwa kitivo cha amani na shauku ya wengi barani Afrika na ulimwenguni pote. Wakati Tanganyika inapata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza mwaka 1961, Baba wa Taifa alisema ‘Tuwashe Mwenge, na tukauwe Kilimanjaro, ili uangaze ndani na nje ya mipaka ya nchi yetu. Palipo na chuki kukawe na furaha, palipo na giza kukawe na nuru”. Hii ndio asili ya Tanzania na hii ndio inayopaswa kuwa daima ya Tanzania.

Mabibi na Mabwana,

Watanzania wana matamanio na ndoto za maendeleo, vijana wao wana vipaji lukuki na wamejawa na uthubutu katika kutafuta maisha na kujiendeleza, huku wakiamini katika ahadi ya ukuu wa Taifa lao, na uwepo wa amani tuliyo nayo tangu uhuru. Watanzania wanaamini katika kujenga jamii ya watu huru na wenye ushujaa, huku wakizifuata fursa za kujiendeleza kiuchumi na kukabiliana na changamoto za maisha yao. Taifa letu likiwa bado changa, kwa minajili ya miaka tokea uhuru wake, na kwa sababu ya kuwa Taifa lenye vijana wengi, tuna ulazima wa kusimama pamoja kurejesha tena ndoto zilizo terereka na matumaini yaliyopotea kuhusu ustawi wa maisha yetu ya sasa na kesho yetu, na kuhakikisha tunahuisha tena matarajio na matamanio tuliyoyaamini tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Naamini katika kuiongoza Tanzania na watu wake ili kwa pamoja tuweze kuzifikia ndoto zetu, na tuweze kuhuisha tena imani na marajio ya kila mwananchi wetu katika kipindi ambacho uchumi wa mtu mmoja moja umedondoka, ugumu wa maisha umekithiri katika jamii, na simanzi la kutokujiamini limetanda katika nyuso za wengi , huku kukiwa na mashaka na sintofamu kuhusu kesho yetu. Kama ilivyoandikwa katika vitabu, “yeye aliye mnyonge na aseme mimi ni nina nguvu!”, naam, Aliye maskini na aseme, Mimi ni tajiri!”. KWA KUWA, Kwa umoja wetu, na kwa kuthubutu kwetu, kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020, tunaweza kubadili mwelekeo wetu na kuirejesha tena Tanzania yenye fanaka, heri, na amani ya moyo kwa kila mtanzania. Kwa pamoja, tuna uwezo wa kuuambia mlima huu ung’oke na ukatupwe bahari. Tunaweza, kwa pamoja, ifikapo Oktoba 2020, kutumia maji na kuni kuyaivisha mawe, ili historia iandikwe juu ya uthubutu wa kizazi chetu, KWA KUWA wahenga walisema kizazi chenye adili kitabarikiwa. Katika kipindi na majira haya, hata aliyemnyonge na asimame, SOTE tuvae uthubutu wa kurejesha upya U-Tanzania wetu katika ubora wake, KWA KUWA Tanzania yenye NEEMA ya daima ndiyo yalikuwa maono ya Mwasisi wa Taifa, Mwalimu Nyerere aliposema “Ili tuendelee, tunahitaji WATU, Siasa safi, na UONGOZI bora”.

Mabibi na Mabwana,

Katika majira na nyakati kama hizi , changamoto na adui mkubwa anayetukabili sasa kama ni Taifa ni hofu iliyotanda miongoni mwa wanajamii, na kwa pamoja tunaweza kusimama kama nchi na kuishinda hii hofu. Vijana waliomaliza masomo na kukosa ajira, chaguzi zilizofanyika bila kufuata misingi ya haki na demokrasia katika kuwapata baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa, huku watu wengi wakiwa na mashaka kama chaguzi zijazo zitakuwa huru na za haki, hofu ya kutokuwa na kipato cha kulisha familia na kusomesha watoto. Hofu kwamba haki inaweza isitendeke endapo mwananchi ana shauri mahakamani. Hofu juu ya uwepo wa uhuru wa vyombo vya habari na uandishi, na hofu ya kujieleza na kujiunga na vikundi vya kisiasa ama kijamii kwa utashi wa mtu binafsi. SOTE tunashuhudia uwepo wa hofu kubwa miongoni mwa jamii, na ni sharti tusimame kama mashujaa wa kizazi chetu na kuishinda hofu.

Mabibi na mabwana,

Katika wakati wa utawala wake, Rais Benjamni W. Mkapa aliamini katika ushindani wa kisiasa na kuongoza serikali ambayo kauli mbiu yake ilikuwa Uwazi na Ukweli. Aliwahimiza watanzania kuhusu nidhamu ya kujenga uchumi na taasisi endelevu katika Taifa na kupambana na deni la Taifa na mfumuko wa bei. Katika awamu ya nne ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tulishuhudia kuongezeka kwa wigo na fursa za demokrasia, ikiwa ni pamoja na wanawake wengi zaidi kupata nafasi za uongozi katika siasa na sehemu nyeti za maamuzi Tanzania. Katika awamu ya nne, tulishuhudia kupanuka kwa wigo wa demokrasia huku vyama vya upinzania vikiongeza viti vyao katika Bunge la Tanzania. Katika kauli mbiu yake ya Ari Mpya na Kasi Mpya, Rais Kikwete aliweza kuiongezea Tanzania heshima kubwa katika Nyanja za mahusiano ya Kimataifa. Awamu ya Sita chini ya uongozi wangu itaenzi misingi bora iliyojengwa na waasisi na viongozi waliotangulia, huku ikiimarisha mifumo na taasisi za kuongoza nchi kupitia utawala thabiti wa sheria ambako mihimili ya serikali, Bunge na Mahamaka zitakuwa huru na kuwepo kwa Uthibiti na Uhakiki katika kuongoza nchi, kutungua sheria, na kusimamia utoaji haki kwa wote.

Mabibi na Mabwana,

Endapo Chama changu kitaniteua kuwa Mgombea na watanzania wakanipa ridhaa ya kuongoza Taifa, serikali nitakayoiongoza itatarajia kujikita katika kutekeleza mambo yafuata katika siku 100 za kwanza za uongozi wangu:-

  • Kuunda Tume ya maridhiano ya kitaifa
  • Kufuta sheria zote kandamizi zinazosababisha watu kuwekwa kizuizini bila haki ya kupatiwa dhamana, na kuwatoa gerezani watu wote walioonewa
  • Kuweka sera mpya ya uchumi wa uchukuzi. (Transport economics) kwa kutumia reli ya Kati na kulenga soko
  • kubwa la nchi zisizo na bandari.
  • Kwa kuwa wajibu wa kiongozi mkuu wa nchi kuhakisha watu wake wanao ulinzi na usalama, na kwamba wanaweze kumudu kujikimu kimaisha, nitahakikisha kwamba tunafanya kila linalowezekana kuongeza ajira kwa vijana na watanzania kwa ujumla, huku sekta binafsi ikiwa kipaumbele kama sekta kiongozi kwenye upatikanaji wa ajira nchini.
  • Tutaanza mara moja kuipitia upya rasimu ya Katiba Mpya ya Tanzania, kwa kuanzia na rasimu ya Jaji warioba
  • Tutairekebisha sheria ya Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA ili iwe taasisi inayojitegemea na isiyolalamikiwa kuhusu uendeshaji wake au kuingiliwa kisiasa. Hatua hii itahusisha pia kupunguza utitiri wa kodi, na kuwa na mfumo wa kodi ulio wazi na wa kueleweka kwa lengo la kupanua wigo wa walipa kodi na kuongeza mapato ya serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
  • Tutaweka sera mpya itakayosimama sekta ya kilimo na uvuvi, ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa pembejeo, uhakika wa masoko, kilimo cha umwagiliaji, na kuboresha shughuli za uvuvi katika maziwa na bahari kuu kwa lengo la kuwanufaisha wavuvi wadogo wadogo na kuthibiti wizi wa raslimali zetu katika bahari kuu.
  • Tutaipitia upya na kuirekebisha sheria ya Bodi ya mikopo ya elimu ya juu kwa lengo la kuwaondolea wanafunzi faini za malimbikizo, na kuondoa ulazima wa kuanza kurejesha mkopo kabla ya mwanafunzi husika kupata ajira. Aidha, tutarekebisha na kupunguza kiwango cha asilimia ya marejesho anayopaswa kuyafanya mwanafunzi ili kumpa unafuu wa kumudu maisha kwa kuongeza muda wa malipo.
  • Tutaweka sera mpya kuongoza sekta ya afya na kuinua kiwango cha utoaji huduma ya kitabibu nchini. Tupitia upya mpango wa Taifa wa upatikanaji wa maji safi na salama vijijini, na mijini.
  • Tutatunga sera mpya na wezeshi ili kufufua sekta ya mafuta na gesi na kuruhusu uwekezaji wa mitaji mikubwa-FDIs, na kuruhusu serikali kuhodhi asilimia ya hisa kwa niaba ya wananchi wa Tanzania. Hatua hii itawezesha kuanzishwa Liquidified Natural Gas Plant-LNG katika ukanda wa Mtwara na kuifanya Tanzania kuwa nchi kiongozi katika uzalishaji wa gesi asilia na mafuta katika ukanda wa Afrika mashariki na SADC. Hatua hii pia itahusisha kuihusha sekta ya madini iwafaidishe wachimbaji wadogo wadogo na kuruhusu uingizwaji wa mitaji mikubwa katika sekta hii, ikiwepo dhahabu, tanzanite, graphite, na urani.
  • Tutaimarisha mahusiano ya kikanda kwa kuidhinisha itifaki ya Afrika Mashariki kuhusu ‘Free Movement of persons, goods and services”, na ushirikiano wa ulinzi na usalama-Mutual Defense Pact, na kuongeza ushirikiano wa mafunzo katika kuimarisha Majeshi yetu ukanda wa Afrika Mashariki.
  • Tutarejea upya makubaliano ya biashara kati ya ukanda wa Afrika Mashariki na Jumuiya ya Ulaya-EPA, na kuidhinisha ushirikiano wenye maslahi kwa wafanyabiashara wa Tanzania hasa kwa fursa ya kuuza bidhaa zetu bila kodi katika nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
  • Tutaingia mara moja kwenye “Bilateral Negotiation” kwa mkataba mpya wa kibiashara kati ya Tanzania na United Kingdom, kwa kuwa UK sio tena mwanachama wa EU.
  • Tutaongeza idadi ya nchi ambazo watanzania wanaweza kusafiri bila ulazima wa kuwa na visa (visa free) kupitia makubalino baina ya nchi na nchi na kwa kuzingatia utaratibu wa kidiplomasia wa “resprocity”. Hatua hii itaongeza idadi ya watalii wanaokuja nchini, na itawawezesha watanzania kusafiri kwa shughuli za kibiashara au vinginevyo katika mataifa mengi na kuiletea heshima pasipoti ya Tanzania.
  • Tutaweka sera ya kudumu ya kuimarisha utayari wa Majeshi ya ulinzi na usalama katika kuilinda nje yetu dhidi ya maadui na kulifanya Jeshi la Wanachi wa Tanzania liendelee kuwa la kisasa Zaidi.
  • Tutatunga sheria kuruhusu ‘Dual Nationality”, ambako Mtanzania yeyote anayekubali uraia wa nchi nyingine hawezi kunyang’anywa haki ya Utanzania wake. Hatua hii itawasaidia watanzania waliopo nchi za nje kuweza kuendelea kuwekeza kiuchumi katika nchi yetu na kuongeza pato la Taifa huku tukiendelea kuhakikisha kila mtanzania anabaki kuwa raia wa Tanzania.
  • Tutaruhusu shughuli zote za kisiasa kutoka kwa vyama vya upinzani na wanaharati katika kukusanyika na kuwa na uhuru wa kuikosoa serikali. Hatua hii itaongeza wigo wa demokrasia na kuvipa vyama vya upinzani nafasi ya kujiandaa kisera na kimuundo kwa ajili ya uchaguzi unaofuata.
  • Tutarekebisha sheria ya Habari ili kuruhusu uhuru kamili wa vyombo vya habari, na uhuru kamili wa wanahabari (reporters), ikiwa ni pamoja na haki ya kulinda vyanzo vya habari kama nguzo muhimu kwa upatikanaji wa habari.
  • Tutarejesha Bunge live.
  • Tutaendeleza uhuru uliopo wa kuabudu, na kuweka zuio la kudumu ili kusiwe na tozo za kodi kwa mashirika ya dini, na taaisi za kiraia ili ziendelee kushiriki kama wadau wa maendeleo nchini.
  • Tutaruhuru vyombo vya usafirishaji vyote (Mabasi, malori, meli, ndege, nk) kuwa huru kufanya safari zao usiku na mchana. Hatua hii itaongeza kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa.
  • Tutaboresha sekta ya elimu nchini, na kupitia upya haki na stahiki za walimu, kuanzia kupandishwa madaraja na mishara, haki ya kupata uhamisho kujiunga na familia kwa wale waliioa au kuolewa, na malimbikizo ya mishahara kwa ngazi zote za elimu ya umma nchini.
  • Tutaimarisha uhifadhi, na kuongeza utalii nchini kwa kurekebisha mifumo ya kodi, tozo, mitaji, rasilimali watu, masoko, na uendeshaji wa sekta hii.
  • Tutaimarisha ushiriki wa Tanzania katika jitihada za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya Tabia nchi na athari zinazotarajiwa kulikumba eneo la Ikweta, ambako nchi yetu ipo.
  • Tutaimarisha ushiriki wa Tanzania katika Taasisi ya Kimataifa na kuimarisha mahusiano na ushirikiano wa kikanda, na kimataifa, na kuongeza nguvu ya diplomasia ya Tanzania katika Nyanja za kiuchumi, kisiasi, kiulinzi, na kijamii.
  • Tutarekebisha sheria ya ardhi kuruhusu wananchi kumiliki ardhi bila ukomo (Freehold lease) na kuwapimia wananchi maeneo ya ardhi kote nchini ili kurasimisha utajiri wa watanzania wote kupitia ardhi tunayoimiliki. Hatua hii italeta ukomo kwa serikali kuu kupitia Rais wa nchi kuwa mmiliki wa ardhi ya watanzania, jambo linalowafanya wananchi wote kuwa wapangaji katika nchi yao wenyewe. Aidha, hati zote za umiliki ardhi zitakuwa na thamani katika mabenki na amani za kifedha na kumwezesha mwananchi wa kawaidi kukopesheka na kuwa na mali isiyohamishika.
Ndugu wanahabari, mabibi na mabwana,

Taifa letu linahitaji mabadiliko, na saa ya ukombozi imefika. Ungana nami (kupitia tovuti yangu lazaronyalandu.com) katika safari ya kuleta tumaini jipya kwa Watanzania. SOTE tunaowajibu kwa nchi yetu.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Wote hao wanakwenda kumzuia lissu,halafu siku ya mwisho mwamba anajitokeza na magongo yake anachukua na kurudisha na kuteuliwa siku hiyo jiyo

Lissu ameona mbali ndio.maana kaomba michango ajitafunie za wajinga mapema
 
safi hii, inadhihirisha kweli hiki ni chama cha kidemokrasia na sio sisiemu ambao wanajiandaa kuwatangazia mburura uchukuaji wa fomu huku ikitolewa ya mtu mmoja
 
Kumekucha kumekucha.......... kumekucha..............kumekucha.......
 
nimepita huko youtube kuangalia hotuba ya Mh. Msigwa, kuna matusi mengi sana dhidi yake wakimwambia amwachie Tundu......nimeshangaa kidogo!
 
Huu ndiyo mfano wa chama komavu ktk haki demokrasia na maendeleo yaani kupitia CHADEMA.

CCM Mpya ni full hofu hawawezi kuruhusu demokrasia hata ktk kutangaza nia, kuchukua fomu kuelekea chaguzi za ndani ya chama kufanya uteuzi wa mgombea bora..
 
Nyalandu huyo aliyempelekaga Anti Ezekiel US kutangaza utalii wiki kadhaa, kumbe walienda kufanya ufuska wao
 
Back
Top Bottom