Lazaro Nyalandu: Nitapeleka muswada binafsi kurudisha mchakato wa katiba ya Warioba ili tupate katiba mpya

Kuna jamaa alisoma na Nyalandu Ilboru kipindi kile ya magenius.Anasema hajawahi kuona genius kama huyu jamaa...hata kama akikosa masomo darasani mwezi mzima kama hayupo,lakini akirudi bado namba moja!
 
Huyo ni Nyarandu ama Nyalandu
 
Muda si mrefu kama hajaghulikiwa na watu wasiojulikana basi atabambikiwa bonge la kesi. Maana hapo anataka kutia mchanga kitumbua cha Baba Bashite na kaumu yake.
 
Nyalandu tunamuunga mkono,ile rasimu ya Lumumba haikubaliki
 
Ngoja sasa tuuone uzalendo wa CCM; mh Lazaro asante ila angalia position yako ndani ya chama isije ikawa reviewed.
 
Haiwezekani mabilioni ya fedha za watanzania zilizotumika wakati wa mchakato wa kutafuta katiba ya warioba halafu chochote kisifanyike. Hongera Lazaro Nyalandu
 
Kwahiyo hilo ndio linakutoa roho, suala la mwehu mkamia ukaliona na maana. Poleni sana, na bado kunazidi kucha!!
 
Hatuhitaji kura ya maoni kwa Katiba pendekezwa ambayo kimsingi haina maana yeyote. Ni kupoteza fedha bure. Mchakato wa kuipitia Katiba Upya uanze tukiongozwa na maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Muswada wa Katiba maarufu kwa jina la Warioba.
Katiba pendekezwa ya Kikwete hivi ina uhalali wa kupigiwa kura ya maoni kweli?
Maana mawazo yote ya maana yaliyokusanywa na mzee Warioba toka kwa wananchi yalichezewa Ama wanavyoita vijana, yalikojolewa na bunge la katiba.
Mimi ninaona njia iliyosahihi na kupunguza gharama, ni kuitisha upya bunge la katiba kwa kutumia rasimu ya Warioba, lakini kwa masharti kwamba ni marufuku kwa wale wote walioshiriki kutuharibia katika bunge lile lililopita, wasisogeze pua zao hata mmoja.
Hapo kidogo tunaweza kupata kitu cha maana.
 
Hana lolote hyu jamaa, yote hayo ni kukosa nafasi yoyote kwenye serikali ya JPM, laiti angeipata tusingesikia lolote. Njaaa mbaya sana.
 
Amegundua ndipo kick ya kisiaaa ilipo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…