Lazaro Nyalandu: Nitapeleka muswada binafsi kurudisha mchakato wa katiba ya Warioba ili tupate katiba mpya

Lazaro Nyalandu: Nitapeleka muswada binafsi kurudisha mchakato wa katiba ya Warioba ili tupate katiba mpya

Kuna jamaa alisoma na Nyalandu Ilboru kipindi kile ya magenius.Anasema hajawahi kuona genius kama huyu jamaa...hata kama akikosa masomo darasani mwezi mzima kama hayupo,lakini akirudi bado namba moja!
 
Bunge la katiba lilishaipitisha huwezi rudisha mchakato nyuma tena kinachosubiriwa ni kura ya maoni Ya wananchi wa bara na visiwani kupiga kura Kama hiyo katiba ambayo iliridhiwa Na bunge la katiba lenye wawakilishi wa wananchi wanaitaka au la. Tume ya warioba ilikuwa kazi kukusanya maoni tu na kuyapeleka kwa wawakilishi wa wananchi yaani wabunge waiangalie wajadili na waje na rasimu ya bunge wakiipitisha raisi aipeleke kupigiwa kura na wananchi wote waseme yafaa au la. Wengi hawaelewi kazi ya tume ya warioba ilikuwa Nini. Ilikuwa kukusanya maoni tu ambayo si lazima bunge likubaliane nayo. Na hilo si mara ya kwanza bunge kupiga chini maoni ya tume au kuyarekebisha. Mfano iliundwa tume ya kukusanya maoni ya wananchi Kama wanataka kuingia mfumo wa vyama vingi au la wabaki na chama kimoja Asilimia 80 walikataa kuwa hawataki vyama vingi bunge lilipopelekewa likakubali maoni ya wachache waliotaka mfumo wa vyama vingi likatunga sheria ya kuruhusu vyama vingi. Tume ya maoni sio Final!!!! Ya tume ya warioba yalishapita!!! Hiyo hoja hata ikipelekwa itaenda tupwa shimo la choo cha bunge
Huyo ni Nyarandu ama Nyalandu
 
Muda si mrefu kama hajaghulikiwa na watu wasiojulikana basi atabambikiwa bonge la kesi. Maana hapo anataka kutia mchanga kitumbua cha Baba Bashite na kaumu yake.
 
Nyalando nadhani anaelekea kurukwa na akili.
Mchakato ulifikia hatua ya kupiga kura ya maoni,na waliopitisha kwa wingi ni wao wabunge,simuelewi anavyotaka kurudi reverse,kisheria tunangoja tu kura ya maoni.
Ni kura ya hapana tu itarudisha upya mchakato,Nyalando usitake kutuharibia nchi kisa tu umenyimwa uwaziri,mbona hukusema haya wakati unauza vitalu
Nyalandu tunamuunga mkono,ile rasimu ya Lumumba haikubaliki
 
Ngoja sasa tuuone uzalendo wa CCM; mh Lazaro asante ila angalia position yako ndani ya chama isije ikawa reviewed.
 
Haiwezekani mabilioni ya fedha za watanzania zilizotumika wakati wa mchakato wa kutafuta katiba ya warioba halafu chochote kisifanyike. Hongera Lazaro Nyalandu
 
Nyalando nadhani anaelekea kurukwa na akili.
Mchakato ulifikia hatua ya kupiga kura ya maoni,na waliopitisha kwa wingi ni wao wabunge,simuelewi anavyotaka kurudi reverse,kisheria tunangoja tu kura ya maoni.
Ni kura ya hapana tu itarudisha upya mchakato,Nyalando usitake kutuharibia nchi kisa tu umenyimwa uwaziri,mbona hukusema haya wakati unauza vitalu
Kwahiyo hilo ndio linakutoa roho, suala la mwehu mkamia ukaliona na maana. Poleni sana, na bado kunazidi kucha!!
 
Hatuhitaji kura ya maoni kwa Katiba pendekezwa ambayo kimsingi haina maana yeyote. Ni kupoteza fedha bure. Mchakato wa kuipitia Katiba Upya uanze tukiongozwa na maoni ya wananchi yaliyomo kwenye Muswada wa Katiba maarufu kwa jina la Warioba.
Katiba pendekezwa ya Kikwete hivi ina uhalali wa kupigiwa kura ya maoni kweli?
Maana mawazo yote ya maana yaliyokusanywa na mzee Warioba toka kwa wananchi yalichezewa Ama wanavyoita vijana, yalikojolewa na bunge la katiba.
Mimi ninaona njia iliyosahihi na kupunguza gharama, ni kuitisha upya bunge la katiba kwa kutumia rasimu ya Warioba, lakini kwa masharti kwamba ni marufuku kwa wale wote walioshiriki kutuharibia katika bunge lile lililopita, wasisogeze pua zao hata mmoja.
Hapo kidogo tunaweza kupata kitu cha maana.
 
Hana lolote hyu jamaa, yote hayo ni kukosa nafasi yoyote kwenye serikali ya JPM, laiti angeipata tusingesikia lolote. Njaaa mbaya sana.
 
Nyalando nadhani anaelekea kurukwa na akili.
Mchakato ulifikia hatua ya kupiga kura ya maoni,na waliopitisha kwa wingi ni wao wabunge,simuelewi anavyotaka kurudi reverse,kisheria tunangoja tu kura ya maoni.
Ni kura ya hapana tu itarudisha upya mchakato,Nyalando usitake kutuharibia nchi kisa tu umenyimwa uwaziri,mbona hukusema haya wakati unauza vitalu
Amegundua ndipo kick ya kisiaaa ilipo
 
Back
Top Bottom