Lazaro Nyalandu: Tanzania inahitaji Katiba mpya ili mihimili ya utawala iwe na mipaka iliyo wazi

Lazaro Nyalandu: Tanzania inahitaji Katiba mpya ili mihimili ya utawala iwe na mipaka iliyo wazi

Hakuna anayepinga uwepo wa katiba mpya, ila je vipaumbele vyetu kama taifa kwa sasa ni vipi?? Je ni demokrasia au ni ufaidikaji na rasirimali zetu? In short katiba mpya kwa sasa siyo agenda ya taifa, maana hata ukiwa na katiba mpya kwa jinsi baadhi ya viongozi wa upinzani (akiwemo na yeye huyu mnafiki nyalandu) uelewa wao wa mambo ni mdogo sana tena sana, na wanaendeshwa na matumbo yao, yaani kama kuna kitu kinashibisha tumbo lake basi atalalia huko huko, ila kama kuna kitu kinasababisha njaa tumbo lake basi atakipinga kweli kweli. Viongozi wetu wa upinzani hawajitambui kabisa, yaani uelewa wao unaendeshwa na ubinafsi na siyo maslahi mapana ya taifa. Wanataka vile wanavyovitaka wao na siyo inavyovitaka Tanzania, na ndiyo maana kwa kizazi chetu kamwe tusitegemee upinzani kushindwa uchaguzi wa rais au kuongoza serikali, maana akili zao zinawaza matumbo na ubinafsi. Yaani mpaka wachungaji akina Mh. Msigwa hela imewatawala na siyo Tanzania. Wapinzani wetu (including Nyarandu) wapo tayari kushirikiana na mataifa maadui zetu ili kufanikisha ajenda zao. Mungu alisha walaani wapinzani wa Tanzania, na laana hiyo ikae juu yao kwa usaliti na uzandiki. Mungu Mbariki sana tena sana Dkt Magufuli na CCM yetu.
Toka tupate uhuru sijawahi sikia chama cha upinzani kinatawala,unayoyaona leo yote yamefanywa na CCM na magu akiwa waziri kwa nini hakupinga?
Jibu ni katiba
 
Hivi mafisadi na wala rushwa kwani nini bado wanapeta tu
 
Yupo askofu katoliki bukoba nae kasema hayo Leo,
Wenye akili wameshanusa harufu ya dikteta
 
Nyarandu may be right,only that his timing is not right. Kwani hakijui chama chake!kelele zikizidi watasikiliza na watafanya kweli,lakini watafanya vile wanataka wao. Wale jamaa hawashinikiziki jamani. Mark my words.
 
Jamani mbona xkuelewiiii hivi ww ni me au ke maana nimegundua kitu kwako hebu jibu kwanzaa au unampenda nyalandu ?
Mkuu naomba nikujibu mimi mwana saikolojia niliyosomea Uk., huyu ni me ila siyo riziki mkuu.....
 
Bila kujali uchama aluchokisema ni kweli. Ifikie kipindi iwe utaifa kwanza chama baadae.

Hilo siyo geni hata kidogo. Ilikuwa agenda kuu kwenye rasimu ya katiba ya warioba na iliingizwa hivyo kwenye rasimu yao. Lkn wote tunajua walicha kifanya CCM na viongozi wake
 
Huyu jamaa cjui alofiaga wapi na cjui nn kilichomfufua nadhani kuna kitu kipya cha chinichini kinaendelea kwa baadhi ya Viongoz wa JK
Time will tell
Mara paap
 
MUDAWOTE; Umeanza unamshambulia Nyarandu baadae upinzani bila hata kuweka koma, vp nyarandu ameishakuwa mpizaniwa ccm ?
 
Huyu nae ana washwa washwa tuu....kwani kwenye mchakato wa katibu alikuwa na cheo gani?
Rais alishasema swala la katiba si kipaumbele kabisa kwa sasa...
Kwanza katiba mpya haina msaada wowote ule....
Ndiyo uelewa wenu uvccm....ila akibadilisha msimamo kuwa ni muhimu katiba mpya ipatikane kipindi hiki ,kwajinsi ambavyo hamjitambui nanyinyi mtashabikia tena na kuunga mkono....yaani.nyie uvccm ni bomu jingine la taifa hili....
 
Hakuna anayepinga uwepo wa katiba mpya, ila je vipaumbele vyetu kama taifa kwa sasa ni vipi?? Je ni demokrasia au ni ufaidikaji na rasirimali zetu? In short katiba mpya kwa sasa siyo agenda ya taifa, maana hata ukiwa na katiba mpya kwa jinsi baadhi ya viongozi wa upinzani (akiwemo na yeye huyu mnafiki nyalandu) uelewa wao wa mambo ni mdogo sana tena sana, na wanaendeshwa na matumbo yao, yaani kama kuna kitu kinashibisha tumbo lake basi atalalia huko huko, ila kama kuna kitu kinasababisha njaa tumbo lake basi atakipinga kweli kweli. Viongozi wetu wa upinzani hawajitambui kabisa, yaani uelewa wao unaendeshwa na ubinafsi na siyo maslahi mapana ya taifa. Wanataka vile wanavyovitaka wao na siyo inavyovitaka Tanzania, na ndiyo maana kwa kizazi chetu kamwe tusitegemee upinzani kushindwa uchaguzi wa rais au kuongoza serikali, maana akili zao zinawaza matumbo na ubinafsi. Yaani mpaka wachungaji akina Mh. Msigwa hela imewatawala na siyo Tanzania. Wapinzani wetu (including Nyarandu) wapo tayari kushirikiana na mataifa maadui zetu ili kufanikisha ajenda zao. Mungu alisha walaani wapinzani wa Tanzania, na laana hiyo ikae juu yao kwa usaliti na uzandiki. Mungu Mbariki sana tena sana Dkt Magufuli na CCM yetu.

Akili haiko sahihi. Yaani kudai katiba ni usaliti? Kwa nani kwa mfano? Au unaandika kujifurahisha tu? Una maandishi ya kichochezi sana wewe. Jaribu kuwa mzalendo basi. Rais wetu atakaa muda wa miongo 2 then anaondoka. Kwa sababu katiba iliyopo inawaumiza wananchi ndo maana inaombwa. Kuwa mzalendo dada
 
Hakuna anayepinga uwepo wa katiba mpya, ila je vipaumbele vyetu kama taifa kwa sasa ni vipi?? Je ni demokrasia au ni ufaidikaji na rasirimali zetu? In short katiba mpya kwa sasa siyo agenda ya taifa, maana hata ukiwa na katiba mpya kwa jinsi baadhi ya viongozi wa upinzani (akiwemo na yeye huyu mnafiki nyalandu) uelewa wao wa mambo ni mdogo sana tena sana, na wanaendeshwa na matumbo yao, yaani kama kuna kitu kinashibisha tumbo lake basi atalalia huko huko, ila kama kuna kitu kinasababisha njaa tumbo lake basi atakipinga kweli kweli. Viongozi wetu wa upinzani hawajitambui kabisa, yaani uelewa wao unaendeshwa na ubinafsi na siyo maslahi mapana ya taifa. Wanataka vile wanavyovitaka wao na siyo inavyovitaka Tanzania, na ndiyo maana kwa kizazi chetu kamwe tusitegemee upinzani kushindwa uchaguzi wa rais au kuongoza serikali, maana akili zao zinawaza matumbo na ubinafsi. Yaani mpaka wachungaji akina Mh. Msigwa hela imewatawala na siyo Tanzania. Wapinzani wetu (including Nyarandu) wapo tayari kushirikiana na mataifa maadui zetu ili kufanikisha ajenda zao. Mungu alisha walaani wapinzani wa Tanzania, na laana hiyo ikae juu yao kwa usaliti na uzandiki. Mungu Mbariki sana tena sana Dkt Magufuli na CCM yetu.
Umeniharibia siku yangu kwa ulicho kiandika. Ingawa kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni yake. Ila sio kila anaetoa maoni anastahili kusikilizwa.
 
Mbunge Nyalandu asema Tz inahitaji katiba mpya ili mihimili iwe na mipaka iliyowazi na kuwepo kwa uangalizi wa Bunge, Mahakama na Serikali.

Watu wa singida wamekuwa chachu ya mabadiliko Tanzania, hongera Lissu & nyalandu ya kuthubutu ktk utawala huu. Nikiwa rais wa Tanzania makao makuu yatahamia singida toka Dom
 
Kuna mstari mmoja ambao tukiweza kuuvuka wa Tz tutapiga hatua kubwa kimaendeleo. Kama anavyosema JPM uvyama vyama! Amini nawaambia adui mkubwa wa amani,utulivu na hata maendeleo nchini kwetu si udini wala ukabila. Adui ni vyama vyetu vya siasa vilivyotufunga akili zetu kwenye box.
Kwamba mtu kama si wa chama chako, lolote alisemalo au atakalotenda hata kama ni kwa maslahi mapana ya nchi ni rubbish! Damu za watu zimemwagwa na zitaendelea kumwagika sio kwa udini wala ukabila ila sababu ya uvyama

Natamani mheshimiwa Rais anapolikemea suala hilo aende mbali zaidi, avunje huu unyanyepa wa kivyama kwa vitendo na kwa dhati kabisa maana yeye anayo nafasi ya kipekee kuanzisha hilo

kitu ukiasisi mwenyewe harafu ukemee nani atakuamini?

Unapo wakataza wengine wasifanye siasa na wewe unafanya hadi kwenye sherhe za kijeshi kinyume na mila na desturi za watanzania ukikemea uvyama nani atakuamini?
Kuwafanya wapinzani wako wenyeji vituo vya polisi na mahabusu za magereza kisha unadai tuache uchama nani atakuami?

Huruma ya wananchi dhidi ya anaenyanyaswa ndio matokeo ya kile unachokiita uchama kwa kifupi sio uchama ni upinzani dhidi ya unafiki, uonevu na ukiukaji wa haki za kiraia
 
Wakati mchakato ulipo pelekwa bungeni huyu mkuu alikuwa Waziri, wakaikoroga wanavyo taka wao. Sasa katiba imembana anataka kutuaminisha kivingine... Hii ni kujifunza kutokana na makosa
Which is okay!
 
Kuitwa mwanaume sio lazima uwe na uume...ni jinsi.utakavyojiamini na kusimamia kile unachoamini bila kua na nidhamu ya woga wala unafiki
 
Ushauri mzuri ingawa hataeleweka kwa wachache ingawaje wanaufahamu ukweli!
Fursa ya katiba mpya ilijitokeza. Lakini wao kwasababu walikuwa na malengo yao, kwa manufaa yao wakaikataa! Sasa baada ya kuona wamesahauliwa kwenye utukufu wa awamu ya 5 ndio wanakumbuka shuka wakati kumeshakucha! Na ndio kinachoifanya Afrika izidi kurudi nyuma! Kila mwanasiasa ana msimamo fulani kwasababu ya maslahi yake.
 
Alipokuwa kwenye "system" hakuuona umuhimu huu ila sasa kwa kuwa yuko nje ndo anauona!
Ni sawa kabisa ndivyo inavyokuwa. Kwani ukiingiza benchi la ufundi uwanjani wanaweza kufanya mavitu wanayowaelekeza walioko uwanjani. Ukiwa nje unaona!!!!
 
  • Thanks
Reactions: bbc
Back
Top Bottom