Lazaro Nyalandu: Tanzania inahitaji Katiba mpya ili mihimili ya utawala iwe na mipaka iliyo wazi

Lazaro Nyalandu: Tanzania inahitaji Katiba mpya ili mihimili ya utawala iwe na mipaka iliyo wazi

Kumbe msopojipendekeza CCM akili zenu zinakua nzuri safi Nyalandu
 
Nyalandu tatizo hauziki. Tangu Magu awakatae wageni wake waliokuwa wakila nae madili kule mali asili na utalii amekuwa akitafuta kiki mpya mpya ila nazo zinazima fasta!!!

Yes we need katiba mpya, ila vp naye alishiriki kuipitisha ile ya magumashi ya JK?
 
Huyu leo katika kikao chao hicho lazima awepo kwenye Agenda.
Anaongea anachokiamini.Maana kuna wengine wanaamini
FB_IMG_1506512718422.jpg
 
CCM lazima watamuhoji tu, maana wanasema haya mambo wayafikishe kwenye vikao vya chama na si mitandaoni, kufanya hivyo ni kukihujumu chama ambalo ni kosa la kimaadili huku ukiwa kiongozi (mbunge) wa CCM
 
Lazaro ni mbunge.. Apeleke mswada bungeni wa kutaka katiba mpya ile ya Warioba.. Sasa huku mitandaoni haitafika kokote, i hope anajua utaratibu, aufuate
 
Kama wabunge wote wa ccm wataanza kujitambua kama Nyalandu basi huo utakuwa ukombozi mkubwa wa wana ccm Na Nchi Kwa ujumla kutoka kwenye ukoloni mamboleo wa "ZIDUMU FIKRA ZA MHE: MWENYEKITI hata kama kakosea njia"
 
soon bashe atajilipua pia makamba, kigwangala na mwigulu mpka wapigwe makofi ndo watajilipua
 
Wakati mchakato ulipo pelekwa bungeni huyu mkuu alikuwa Waziri, wakaikoroga wanavyo taka wao. Sasa katiba imembana anataka kutuaminisha kivingine... Hii ni kujifunza kutokana na makosa
Unafiki kwa wabunge wetu wa chama chao cha kijani unazidi mipaka yaani unakereka mpaka basi huyu ni mnafiki to the highest level.
 
Bila kujali uchama aluchokisema ni kweli. Ifikie kipindi iwe utaifa kwanza chama baadae.
impact ya unafiki ishaanza kuwatafuna unakumbuka walivyoshangilia kipindi kile. sasa waje tuongee lugha moja
 
Watanzania wa ajabu sana yaani mpaka uone ugali wako uko hatarini ndo ghafla unapata hekima ya namna hii!
 
Mukimfukuza bwana wenu na mkimuacha mnamuogopa.
 
Back
Top Bottom