Lazima tukazikwe "nyumbani"?

Lazima tukazikwe "nyumbani"?

inaprndeza ukizikwa kwenu maana kabuli litakuwepo siku zote kumbukumbu tofauti namjini ambapo hawachelewi kuhamisha makabuli kama ambayvo iliwahi kutokea


Huwa najiuliza kila wakati, hivi kutokana na kupanuka kwa miji, bado maeneo ya makaburi yatazidi kuheshimiwa huko vijijini kunakokuita sasa?? manaka hata ukienda katika Makaburi Makubwa Kama Kinondoni, kuna watu wamezikwa miaka ya 1800 hvi wakati huo nadhani palikuwa porini pakiitwa kijiji, saa kaburi ukipata ni juu ya kaburi jingine pengine zaidi ya matano pamoja.

Na hata kwa mfano Ilala Boma ambapo wakati fulani paliwahi kulea mvutano wa kuhamisha makaburi, sina shaka wakati huo eneo la makaburi lilipoanzishwa palikua kama kijijini na waliozikwa walisema wapo nyumbani...sijui kukua kwa miji yetu kama hakuna athari ya kuwepo pia kwa dhana ya kuhifadhi maeneo ya Makaburi ???.....
 
hao wanaoacha maagizo nikazikwe sehemu fulani wako selfish!....ukiacha agizo kama hili then lazima uwe umepanga jinsi litakavyotekelezeka...ili usiwape wenzio usumbufu!!...
..pray ufe kifo cha amani na upate decent funeral baasi!,ishu za kukompliketi mambo wakati saa hizo wewe ni marehemu sio VIZURI,..

---kuna 'waliopotea' kny sunami na ajali nyengine baharini,kuna ambao maiti zao hazijatambuliwa..hivyo zinaishia kuzikwa na serikali au zinapelekwa kwa wanafunzi wale wa udaktari na forensic science...hujiulizi watu hawa walimkosea nini mungu...maisha yao kuishia vile???kabla hujatoa maamuzi ya kijinga ....tafakari!
 
Ni upotevu tu wa resources na time. Kwa mfano unakuta Mtanzania kafa nje ya nchi zinachangwa hadi $20,000 ili kuusafirisha mwili na bado kuna gharama za wale watakaoshindikiza na labda huyu alikuwa na mke/mume na watoto. Na mapesa haya yote yanatumika wakati mchango huu ungeweza kuisaidia sana familia ya marehemu na hivyo kupunguza gharama za mazishi kama angezikwa alikofia.
 
hayo ni mambo ya mwilini sana, na kutawaliwa na mila, lakini mie nijuavyo maiti haina kwao

aliye hai ndo anakwao, hivyo ni vijimambo vya kibinadamu tu, wala havina uhusiano na

imani takatifu, kama ujuavyo binadamu kuongozwa na roho wa Mungu tuna 20%

na pengine -0% kabisa hivy kuacha maagizo ya namna hiyo si ajabu.
 
Back
Top Bottom