LBL: Pyramid Scheme Inayowatapeli Watu kwa Kisingizio cha Uwekezaji

Status
Not open for further replies.

Mshangazi dot com

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2011
Posts
1,345
Reaction score
3,503
Kwanini watanzania wengi wanatapeliwa na Ponzi schemes kama LBL Tanzania?
Nini chanzo cha watu kutokupenda kufanya tafiti na kutafuta taarifa kabla ya kuinvest pesa.

Hakuna kampuni inayoitwa LBL Advertising Media LTD ambayo imesajiliwa Tanzania, ila kuna Kampuni yenye jina sawia imesajiliwa uingereza na raia wa marekani anaitwa Challis (see image). Hapa Tanzania kuna makampuni zaidi ya kumi yenye majina ya kufanana na hilo ambayo yamesajiliwa hivi karibuni. Kama kuna watu wa Brela humu wafanye uchunguzi yakinifu kuhusu uhusiano wa hizi kampuni.

TAHADHARI: Najua umeshawishiwa na kuona watu wanapata pesa, ila huu ni utapeli, kama umeweka pesa yako huko itoe chap, la sivyo soon utalambwa.

Nawasilisha!


=====

Maelezo ya ziada kuhus utapeli unaofanywa na kampuni hiyo

 
Hii ni pyramid scheme nzuri sana ukianza nayo itakapokufa utavukana sana Mimi binafsi Nimeanza nayo Kwa kuweka 1089k sasa Nina mwezi wa nne navuna 36000 kila siku ni almost 4.3 ikifa Leo sina hasara
 
Intern utakula zako elfu Tano....then ukitoka hapo utaambiwa uchague kiasi Cha kuwekeza kuanzia 50k Hadi 540k
Mimi sikushawishiwa na mtu niliona tangazo you tube nikasema ngoja nikaangalie Kuna Nini huko,,,nilivyomaliza intern nilivyoona nimepata 5k nikawa Sina habari nayo....wakawa wananilazimisha niitoe ....ilikaa km week 3 ndio nikaitoa nikajiunga bando....ila kilichonishangaza kwenye kutoa ela system haikuruhusu Moja Kwa Moja kutoa ela ni mpaka sijui nani aidhinishe.....nikawauliza km hii kampuni ni kubwa km mnavyosema ipo nje ya nchi na ndani ya nchi kwanini msiruhusu system yenyewe ikampa access mtu kutoa ela yake sijui bila kupitia sijui Kwa nani.....walivuojibu kwa ubabaifu nikazoom nikaona Hawa wasanii na Mimi mwenyewe msanii nikaachana nao....hio ilikuwa mwaka Jana kama mwezi wa nane ivi
 
Shortcut is always the longest way you were not going
 
HAHAHAHAHA hivi mtu ananunua udongo kwenye kijiko laki tano bado unaumiza kichwa kwa ajili yake kweli?? hebu tumia huo ubongo hata kukatia gogo wakati unapanga mipango ya jioni utafanya nini kwa maendeleo yako binafsi.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…