LBL: Pyramid Scheme Inayowatapeli Watu kwa Kisingizio cha Uwekezaji

LBL: Pyramid Scheme Inayowatapeli Watu kwa Kisingizio cha Uwekezaji

Status
Not open for further replies.
Una uhakika upi hizo sadaka zina tumia vyema na ipasavyo, huko misikitini na makanisani?.

au ndio mna wekeza kuwa nunulia wachungaji na mashekhe magari, halafu nyie njaa kali!.

Bora usaidie yatima, vilema walio mtaani, kuliko kuchangia sehemu usiyo jua hela Ina tumika vipi.
 
Toeni zaka kamili
Toeni sadaka makanisan na misiikitini

Wekezeni ujenzi WA makanisa

Wekezeni kwenye shuhuli za makanisa na misikiti

Mungu awainue
Lbl wapo waumini wa makanisa na wa mwamposa nao wanawekeza huko wakipata gawio wanapeleka kwa mwamposa
 
Wadau wa JF, Salaam!

Hii dunia ni ya ajabu sana. Kuna jamaa anakuambia kuna mti fulani, ukiusogelea na kuuangalia tu kwa dakika chache, unanyesha noti. Wengine wanakuambia kama unataka utajiri, usihangaike sana—jiunge na jukwaa fulani, alika watu, angalia video kadhaa, fanya “tasks” rahisi, na boom! Pesa zinakutiririka kama maji ya mto.

Ni ajabu, sivyo? Lakini cha kushangaza zaidi, watu wanaingia kwa fujo. Wanaacha kazi zao za uhakika, wanakimbilia ndoto ya pesa za haraka bila hata kuuliza maswali ya msingi: Hizi pesa zinatoka wapi? Hii biashara inaendaje? Kwanini kila mtu anahamasishwa alete watu wapya badala ya bidhaa halisi kuuzwa?

Kwa macho ya kawaida, hizi zinaonekana kama fursa za kipekee—njia rahisi ya kupata kipato. Lakini kwa macho ya ndani, kuna giza, mitego, na machozi ya wengi waliovutwa na tamaa ya pesa rahisi.

Wimbi la LBL na Miradi Mingine ya Ulaghai

Kwa siku za hivi karibuni, tumeona ongezeko kubwa la makampuni yanayojinadi kuwa ni fursa za kipekee za kipato mtandaoni. Utasikia majina kama LBL, TaskPay, Click2Earn, na mengine mengi. Wanajitokeza ghafla, wanapiga kelele kwa nguvu mitandaoni, wanatumia lugha tamu na ushuhuda bandia, kisha wanapotea kama moshi.

Hawa jamaa wana mbinu zile zile:

Unajiunga na kampuni yao kwa kulipia kiasi fulani au kwa bure lakini ukifanya kazi kama kutazama video au kulika watu.

Unapewa matumaini makubwa—hata ushuhuda wa watu waliopata mamilioni!

Unalipwa kwa kufanya “tasks” fulani ndogo—lakini ili upate hela kubwa, unatakiwa kuleta watu wapya!

Kadri unavyoleta watu, ndivyo unavyopandishwa daraja na kuahidiwa malipo makubwa zaidi.

Mwisho wa siku, mfumo unafika mahali hauna pesa za kulipa watu, kampuni inatoweka, na walioweka pesa zao wanabaki na machozi.


Ndugu zangu, hii ni mbinu kongwe sana inayojulikana kama Ponzi Scheme au Pyramid Scheme. Wanatumia mfumo wa kutegemea ada au michango ya wanachama wapya ili kuwalipa waliowatangulia. Hakuna biashara halali hapa, ni utapeli mtupu!

Lakini Mbona Wengine Wanafanikiwa?

Unajiuliza, “Lakini nimeshuhudia watu fulani wakipata pesa?” Ndiyo, ni kweli! Lakini hao ni sehemu ya mfumo—either wapo kwenye level ya juu au wanatumiwa kama chambo cha kuvuta wengine. Mfumo unakufa pale wanachama wapya wanapopungua, na hapo wale wa chini wanabaki wameumia.

Kitu cha kushangaza, hata watu wanapoumia, wapo wanaorudi na kujaribu miradi mingine ya aina hii wakitumaini safari hii mambo yatakuwa tofauti. Lakini sheria ya ulimwengu iko wazi: Hakuna hela rahisi!

Funzo na Ushauri Kwa Wana JF.

1. Usikubali tamaa ikupofushe macho – Pesa haziji rahisi, ukiona fursa ya kupata hela bila kazi halali, jiulize maswali mengi.


2. Jifunze kuhusu biashara halali – Kama unataka kuwekeza au kupata kipato mtandaoni, chunguza mifumo halali kama freelancing, e-commerce, na ujasiriamali wa kweli.


3. Uliza maswali ya msingi– Kampuni inatoa huduma gani? Mapato yao yanatoka wapi? Je, kama watu wapya wakikoma kujiunga, bado itaendelea kulipa?


4. Usiwe sehemu ya mzunguko wa ulaghai – Unaposhiriki na kuwavuta wengine kwenye haya matapeli, unakuwa sehemu ya tatizo.



Ni hitimishe kwa kusema,

Tumechoka na hii “miradi za kutajirika haraka.” Ni wakati wa kufungua macho na kuwa makini. Kabla hujaingia kwenye chochote kinachohusisha pesa zako, chunguza kwa kina, usiamini kelele za mitandaoni, na usiingie kwa sababu tu unamuona jirani yako amepata faida.

Ukweli ni huu: Njia pekee ya uhakika ya kupata pesa ni kwa kufanya kazi halali na kujenga maarifa halisi.(Build skills)

Wadau wa JF, naomba tujadili! Ushawai kushuhudia au kuingia kwenye mojawapo ya hizi schem? Ulijifunza nini?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom