Le Mutuz case: Ubovu wa Sekta ya Afya Nchini

Inaitwa CPR hivi ni wangapi wanajuwa kufanya hii procedure
Je watanzania wanajuwa hii kitu au ndiyo wako bize na kuimba na kucheza bongo fleva,kubishana simba yanga,uchawa,udaku tu

Ova
 
Tatizo Mzee Bomaye alishakata tamaa... alikuwa anapost mgonjwa.. akitoka tu hospital mbio kwenye bata. Mgonjwa wa moyo anakaaje wavuvi kempu usiku kucha? Ukimshauri kwenye comment anakutukana na kukublock. Na jinsi alivyokuwa anajitapa kuwa na akili kubwa angeamua kuachana na kina Mange waongee hadi wachoke. Sasa hivi kawapa tabu sana watu wake wa karibu kumtetea... kila mmoja anasema maisha yake yalikuwa tofauti na mtandaoni. Sasa mtu hadi uje ujue maisha yake yalikuwa tofauti na mtandaoni ni lini? Damage aliyojisababishia ilikuwa kubwa sana.
 
Inaitwa CPR hivi ni wangapi wanajuwa kufanya hii procedure
Je watanzania wanajuwa hii kitu au ndiyo wako bize na kuimba na kucheza bongo fleva,kubishana simba yanga,uchawa,udaku tu

Ova

Niliwahi kuhudhulia First Aid course na CPR training ilikuwa mojawapo, tulipotoka nikamwuliza mwenzangu Ile mashine ya kustua Moto inaitwaje akasema mwalimu anaijua
 
Mimi naamini katika uwepo wa nguvu kuu kupita zote(The super natural power) ,hii nguvu akiamua utoke ni kweli unatoka , na ikiamua kukusimamamia unaweza nusurika hata kwenye mdomo wa mamba,so nature ilikuwa imeshaamua lemutuz apishe ,aache wengine waendelee,.

Unaweza jiuliza tukio la Mh. Lissu kunusurika kifo kwa kupigwa risasi 17 ,wakati tembo na ukubwa wake anakalishwa na risasi moja tu!,hii inaitwa uwezo wa the so called super natural power
 
Muda wako wa kuwabwekea wezi unakaribia
 
Unaongelea ubovu wa huduma ya afya mwaka 2023 ukifanya marejeo ya mwaka 1980.
Kuna ulinganifu kweli hapo?
 
Inaitwa CPR hivi ni wangapi wanajuwa kufanya hii procedure
Je watanzania wanajuwa hii kitu au ndiyo wako bize na kuimba na kucheza bongo fleva,kubishana simba yanga,uchawa,udaku tu

Ova
CPR ni huduma ya kwanza muhimu sana kwa mti aliyeshikwa na ugonjwa wa moyo, cha ajabu watu wengi hawaijui. Hii usipomfanyia mgonjwa kabla ya kumpeleka hospital, basi elewa ukimkimbiza hivyohibyo unaweza kufikisha maiti au mahututi wa kuelekea kukata roho.

Hii inahusisha kukandamiza kifua mara kadhaa huku ukimpulizia mgonjewa hewa nzuri.
 
Asante kwa kirefu cha CPR nimekumbuka, my ex was a doctor na ni dr wa moyo so vitu vingi alikuwa akiniambia.

Siku moja baba mmoja kijijini kwetu alikuwa alisha staafu akajipambanua kijijini kwetu akaweka almost kila huduma ilikuwa inapatikana kwake.
Mke wa huyo baba alikuwa ni doctor mstaafu na bado yuko fit tu.

Siku moja huyo baba alidondoka bafuni akawa kwenye koma kwa siku mbili na akafa.
Kijiji kizima kila mtu alimlilia yule baba.

Sasa ilikuwa hivi alienda kuoga akadondoka bafuni akamaliza huko kama 2hr ndo wakaja gundua baada ya kuona hatoki.

Baada ya kukuta kadondoka wakampeleka hospital ilokuwa karibu, asubuhi yake kapelekwa hospital ya wilaya akawekewa oxygen wakati wanataka kumpa rufaa akafa.

Nikakumbuka hii CPR yaani yule baba alikufa kizembe sana.

Nikamsimulia ex wangu ilivyokuwa akaniambia inasikitisha sana kuwa huku bongo mtu ni dr mstaafu hajui hata hiyo CPR yeye ndo angekuwa mtu wa kwanza kumpa hiyo huduma walivyo kumzululisha mgonjwa kwa huo muda wote kwenye hospital za kawaida angepata cpr wenda angestuka ndo akapelekwa hospital.

baba wa watu na hizo pesa zote akafa mengine nimeficha kwa sababu ya usalama.
Mtu ana mapesa yale yote walishindwa hata kukodi ndege maana mgonjwa alikuwa tiyari mjini na akamaliza siku mbili bila huduma inayo staili. Angewahishwa hospital kubwa nao wakajaribu.

Rafiki wa marehemu alipopata taarifa rafiki yake yuko maututi, siku mbili yupo hospital isiyokuwa na huduma. Akafanya utaratibu wa kukodi ndege maskini wakati wanataka kuondoka akafariki kizembe kabisa.

Kifo hakizuiliki ila jambo linapotokea watu wasizembee including ma doctor, usiku ma dr wetu huwezi wakuta hospital wanaacha ma ness wao wanalala. Dah Mungu tuhurumie.
 
Kuwa na mawazo kama haya, yanachangia kwa asilimia kutokuwa na uwajibikaji kwa wattaluma wetu wa afya, na hivyo kusababisha vifo vingi vya wananchi kizembe ambapo vingeweza kuepukwa.
Uwajibikaji bila imani ni sawa na bure keep the faith
 
Kwani tozo hatulipi? Na hosp ya Mnazimmoja ni ya Leo? Ilipaswa kama ni maboresho ya vituo vya afya ingetakiwa ipate maboresho no 1, Maana ipo katikati ya jiji.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono Hoja, lkn je Le Mutuz alikuwa na mke? Kama alikuwa hana mke namna ya kifo chake kilivyotokea ni sahihi kabsa.

Hoja dhaifu sana. Mtoa mada anazungumzia ubovu wa huduma za afya wewe unaleta mambo ya mke.
Inahusiana vipi sasa?!
 
Eti inasemekana, zinasemekana.Upupu mtupu
 
Kwani tozo hatulipi? Na hosp ya Mnazimmoja ni ya Leo? Ilipaswa kama ni maboresho ya vituo vya afya ingetakiwa ipate maboresho no 1, Maana ipo katikati ya jiji.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Kila sehemu Kuna mahitaji ya hivyo Wala hapo mnazi mmja hapana huo upekee,la sivyo nenda hospital kubwa zote ziko hapo hapo Dar..

Mwisho mlikataa kulipa tozo Hadi Serikalini ikaamua kuzifuta na kupunguza sana kiasi hakuna kitu Cha maana wanapata.
 
Yah,kwa tuliyopitia ubaharia na kuwa sehemu fulani fulani hii kitu tumefundishwa sana
Na tunaimudu haswaaa
Je kwa kizazi cha sasa watoto, watu wanafundishwa masuala haya ?

Ova
 
Angalau wenzetu wana ile mtu kazidiwa unapiga ile namba ya emergency wanakuuliza amepatwa na nini unaeleza wanakupa tips za kufanya ukiendelea kusubiri huduma ya kupelekwa hospitali.
Sisi huku hatuna na wala hatujui.
Serikali na wadau wa elimu wangeingiza hii watu wajifunze mashuleni kama somo la huduma ya kwanza angalau tuwe na tips chache za kusaidia mpaka nchi itakapokuwa na uwezo kama wenzetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…