Le Mutuz case: Ubovu wa Sekta ya Afya Nchini

Le Mutuz case: Ubovu wa Sekta ya Afya Nchini

Ndio lemutuz alikuwa na shida ya moyo ila kuna kuna mambo yalichangia kifo chake.

1: lemutuz anaishi peke yake wenda alipodondoka walinzi walimuona muda umeenda, wenda angekuwa na mke angemkimbiza hata mhimbili na sio mnazi mmoja.
2: ex bf wangu alinifundisha huduma ya kwanza pale mtu anapo dondoka gafla na akasititiza kila mtu anatakiwa kujua hii huduma.
Mtu akidindoka gafla unatakiwa kuweka mikono miwili pale kifuani kwenye moyo na kumshutua kwa nguvu kuamsha mapigo ya moyo. Sasa wale walinzi hata kabla ya kumpekeka hospital ilibidi wajaribu hiyo huduma wenda angezinduka.
Miaka iliyopita nilikuwa natokea mjini nikashuka kituo kimoja nikakuta mmama kadondoka watu wamejaa pale eti wameagiza gari wampeleke hospital.

Moyo ukaniambia sogea pale uone nn kinaendelea nikakuta mmama kalala flat kabisa nikakuta mtu anampepea nikamwambia weka mikono miwili hapo kwenye kifua mpamp kwa nguvu alifanya hilo zoezi kama mara 7 hivi yule mama akatoa sauti mmmmm na kupumua kama mtu aliechoka na akatikisa mguu. Mpaka gari linakuja alikuwa anapumua wakampeleka hospital.

Jamani tunatakiwa kujua hizi huduma za kwanza ndogo ndo ingawa mwisho wa siku Mungu ndio muamuzi.

Lemutuz kuishi peke yake plus stress za mtoto wake kumtukana ndo maana kila siku alikuwa akienda batani may be alikuwa anapunguza stress. Coz angekuwa na mtu wa kumjali alipo kuwa huko batani angeulizwa mbona umechelewa kurudi? Uko wapi? Na alipofika hata angedondoka mkewe ndo angekuwa wa kwanza kujua mme wake hospital ipi inamfaa kutokana na tatizo lake.

Hakuna kitu kibaya kukosa mtu wa karibu wa kukujari.
Apumzike kwa amani maana aliishi maisha ya kusimangwa kisa mtoto wa mchepuko, kila siku yeye ni kuji defend as if alituma maombi azaliwe. Rip lemutuz.
Inaitwa CPR hivi ni wangapi wanajuwa kufanya hii procedure
Je watanzania wanajuwa hii kitu au ndiyo wako bize na kuimba na kucheza bongo fleva,kubishana simba yanga,uchawa,udaku tu

Ova
 
Tatizo Mzee Bomaye alishakata tamaa... alikuwa anapost mgonjwa.. akitoka tu hospital mbio kwenye bata. Mgonjwa wa moyo anakaaje wavuvi kempu usiku kucha? Ukimshauri kwenye comment anakutukana na kukublock. Na jinsi alivyokuwa anajitapa kuwa na akili kubwa angeamua kuachana na kina Mange waongee hadi wachoke. Sasa hivi kawapa tabu sana watu wake wa karibu kumtetea... kila mmoja anasema maisha yake yalikuwa tofauti na mtandaoni. Sasa mtu hadi uje ujue maisha yake yalikuwa tofauti na mtandaoni ni lini? Damage aliyojisababishia ilikuwa kubwa sana.
 
Inaitwa CPR hivi ni wangapi wanajuwa kufanya hii procedure
Je watanzania wanajuwa hii kitu au ndiyo wako bize na kuimba na kucheza bongo fleva,kubishana simba yanga,uchawa,udaku tu

Ova

Niliwahi kuhudhulia First Aid course na CPR training ilikuwa mojawapo, tulipotoka nikamwuliza mwenzangu Ile mashine ya kustua Moto inaitwaje akasema mwalimu anaijua
 
Mimi naamini katika uwepo wa nguvu kuu kupita zote(The super natural power) ,hii nguvu akiamua utoke ni kweli unatoka , na ikiamua kukusimamamia unaweza nusurika hata kwenye mdomo wa mamba,so nature ilikuwa imeshaamua lemutuz apishe ,aache wengine waendelee,.

Unaweza jiuliza tukio la Mh. Lissu kunusurika kifo kwa kupigwa risasi 17 ,wakati tembo na ukubwa wake anakalishwa na risasi moja tu!,hii inaitwa uwezo wa the so called super natural power
 
Wewe ukishakuwa na tatizo la Moyo issue ya kufa ni sekunde au wewe ukishasikia nani amepona magonjwa ya Moyo?

Kama Miaka ya karibuni ndio serikali walau imejenga emergency departments kwenye hospital za Wilaya na Mkoa Zenye vifaa sembuse huko chini kwenye Vituo vya Afya?

Mkiambiwa lipeni tozo Serikali iwekeze kwenye Afya mkasema walamba asali wanakula Sasa ngoja Kila mtu apambane na Afya yake.
Muda wako wa kuwabwekea wezi unakaribia
 
Kutokana na taarifa za tukio la kifo cha nguli wa mitandao ya kijamii nchini Ndugu William Malecela ajulikaye kama Le Mutuz.

Nini hatma ya sekta ya Afya nchini katika kuwa na uwezo wa kuwa na wataalamu wa magonjwa ya moyo na vifaa vya kukabiliana na magonjwa ya dhararu kama magonjwa ya moyo.katika kila kituo cha afya nchini hususani katika majiji makubwa nchini ikiwemo mji mkuu wa nchi(ndio ukeli wenyewe) kama Dar Es Salaam.

Inasemekana na kuthibitishwa na Le Mutus mwenyewe kuwa alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya ugonjwa wa moyo na pia kuweza kupata kusafiri nje ya nchi kupata matibabu ya moyo nchini India na South Africa.

Habari za kifo cha William Malecela A.K,A Le Mutuz, zinasemekana alikutwa na aidha walinzi au majira kuwa ameanguka ghafla huku akiwa hoi bin taabani na kwa mshtuko wa walioweza kuwa eneo la tukio, na katika kutathmini haraka kutokana na eneo alipokutwa na akiishi, kituo kilicho karibu zaidi kwa kuweza kumpeleka kupata huduma ya matibabu haraka na ya dhararua ilikuwa ni Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Katika kumbukumbu zangu za utotoni na kwa kuwa nilikulia katika jiji la Dar es Salaam, nimeshawahi kupelekwa kwenye Hospitali ya Mnazi Mmoja kupata huduma ya matibabu katika miaka ya 80 na kwa kweli , japo hiki kituo kipo katikati ya jiji la Dar es Salaam lakini hali ya mazingira na huduma ilikuwa inatolewa pale hasa ukizingatia ni kituo cha afya kinachomilikiwa na serikali, ilikuwa siyo ya kuridhisha kwa hata mimi na umri wangu kung.amua hivyo baada ya kukaa masaa kadhaa bila kuonwa na mtaalamu yeyeto wa afya, na baada kupata fursa, nilionwa na Nesi tu, ambayo alienda kumtafuta daktari, lakini alirudi na cheti kutoka kwa daktai ambaye hakuniona kinasema nipigwe sindano za PPF kutokana jeraha niliopata baada ya kuanguka na baiskeli.

Turudi sasa kwa Ndugu yetu LeMutuz, baada ya kukutwa katika hali aliyokuwa nayo, na uamuzi wa kutokana na eneo anapoishi, ikaonekane akimbizwe katika hii hospitali ya Mnazi Mmoja ilikuwa kama ni kwenda kuandikiwa cheti cha kifo, maana inasemakana baada ya kufikishwa ktuoni hapo, kulikuwa hakuna hata daktari yeyeto aling'amua kuwa mgonjwa kutokana na historia ya afya yake inawezekana amepatwa na Cardica arrest, ugonjwa ambao huduma yake kwanza ilitakiwa kuwa ni matumizi ya Defibrillator (kifaa kinachotumika kuamsha au kusahihisha mapigo ya moyo kwa kuchakachua hali ya afya ya moyo (automatically) kujiseti chenyewe ili kumchoma mngonjwa na nguvu ya umeme ili kurekebisha mwenendo wa mapigo ya moyo), hiki ni kifaa cha msingi kinachotakiwa kuwepo sio katika kila kituo cha afya, kwa wenzetu nchi zilizoendelea kipo kila sehemu hata sokoni, mahoteli makubwa na vituo vya mabasi au treni.

Je katika Hosptali ya Mnazi Mmoja walikuwa na hata na hiki kifaa?

Sasa tunaomba wana Jamii Forum ambao ni wataalumu wa afya yaani madaktari wa ukweli(no ameatures) wanaofanya kazi katika aidha huu mfumo wa sekta ya afya wa vituo vya serikali au binafsi watuaelimishe na kutufafanulia.

Je, kuna uwezekano kuwa kama kungekuwa na wataalamu na vifaa sahihi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja katika siku ya tukio, kungewezesha kuyaokoa maisha ya Le Mutuz?
Unaongelea ubovu wa huduma ya afya mwaka 2023 ukifanya marejeo ya mwaka 1980.
Kuna ulinganifu kweli hapo?
 
Inaitwa CPR hivi ni wangapi wanajuwa kufanya hii procedure
Je watanzania wanajuwa hii kitu au ndiyo wako bize na kuimba na kucheza bongo fleva,kubishana simba yanga,uchawa,udaku tu

Ova
CPR ni huduma ya kwanza muhimu sana kwa mti aliyeshikwa na ugonjwa wa moyo, cha ajabu watu wengi hawaijui. Hii usipomfanyia mgonjwa kabla ya kumpeleka hospital, basi elewa ukimkimbiza hivyohibyo unaweza kufikisha maiti au mahututi wa kuelekea kukata roho.

Hii inahusisha kukandamiza kifua mara kadhaa huku ukimpulizia mgonjewa hewa nzuri.
 
Safi sana
Fikiria hata nadhani pale hospitalini hakuna hata aliyejaribu au kuwa na akili ya kufikiria kufanya hivi
Kila mtu muda wake utafika, ni kweli lakini siyo kizembe kama hapa kwetu

Unajua nchi za Ulaya na US, jinsi mfumo unavyofanya kazi, mpaka imefikia, wananchi wanauhuru kuweka kwenye rekodi yake ya afya siku nikipata matatizo yanahitaji kunikoa kwa kutumia hii njia uliofanya inaiitwa CPR(Cardio Pulmonary Resucitation) au kutumia Defibrillator, anaweka saini msinifanyie hivi au msinikoe , niacheni nife. na hospitali inaheshimu huo uamuzi
Asante kwa kirefu cha CPR nimekumbuka, my ex was a doctor na ni dr wa moyo so vitu vingi alikuwa akiniambia.

Siku moja baba mmoja kijijini kwetu alikuwa alisha staafu akajipambanua kijijini kwetu akaweka almost kila huduma ilikuwa inapatikana kwake.
Mke wa huyo baba alikuwa ni doctor mstaafu na bado yuko fit tu.

Siku moja huyo baba alidondoka bafuni akawa kwenye koma kwa siku mbili na akafa.
Kijiji kizima kila mtu alimlilia yule baba.

Sasa ilikuwa hivi alienda kuoga akadondoka bafuni akamaliza huko kama 2hr ndo wakaja gundua baada ya kuona hatoki.

Baada ya kukuta kadondoka wakampeleka hospital ilokuwa karibu, asubuhi yake kapelekwa hospital ya wilaya akawekewa oxygen wakati wanataka kumpa rufaa akafa.

Nikakumbuka hii CPR yaani yule baba alikufa kizembe sana.

Nikamsimulia ex wangu ilivyokuwa akaniambia inasikitisha sana kuwa huku bongo mtu ni dr mstaafu hajui hata hiyo CPR yeye ndo angekuwa mtu wa kwanza kumpa hiyo huduma walivyo kumzululisha mgonjwa kwa huo muda wote kwenye hospital za kawaida angepata cpr wenda angestuka ndo akapelekwa hospital.

baba wa watu na hizo pesa zote akafa mengine nimeficha kwa sababu ya usalama.
Mtu ana mapesa yale yote walishindwa hata kukodi ndege maana mgonjwa alikuwa tiyari mjini na akamaliza siku mbili bila huduma inayo staili. Angewahishwa hospital kubwa nao wakajaribu.

Rafiki wa marehemu alipopata taarifa rafiki yake yuko maututi, siku mbili yupo hospital isiyokuwa na huduma. Akafanya utaratibu wa kukodi ndege maskini wakati wanataka kuondoka akafariki kizembe kabisa.

Kifo hakizuiliki ila jambo linapotokea watu wasizembee including ma doctor, usiku ma dr wetu huwezi wakuta hospital wanaacha ma ness wao wanalala. Dah Mungu tuhurumie.
 
Kuwa na mawazo kama haya, yanachangia kwa asilimia kutokuwa na uwajibikaji kwa wattaluma wetu wa afya, na hivyo kusababisha vifo vingi vya wananchi kizembe ambapo vingeweza kuepukwa.
Uwajibikaji bila imani ni sawa na bure keep the faith
 
Wewe ukishakuwa na tatizo la Moyo issue ya kufa ni sekunde au wewe ukishasikia nani amepona magonjwa ya Moyo?

Kama Miaka ya karibuni ndio serikali walau imejenga emergency departments kwenye hospital za Wilaya na Mkoa Zenye vifaa sembuse huko chini kwenye Vituo vya Afya?

Mkiambiwa lipeni tozo Serikali iwekeze kwenye Afya mkasema walamba asali wanakula Sasa ngoja Kila mtu apambane na Afya yake.
Kwani tozo hatulipi? Na hosp ya Mnazimmoja ni ya Leo? Ilipaswa kama ni maboresho ya vituo vya afya ingetakiwa ipate maboresho no 1, Maana ipo katikati ya jiji.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono Hoja, lkn je Le Mutuz alikuwa na mke? Kama alikuwa hana mke namna ya kifo chake kilivyotokea ni sahihi kabsa.

Hoja dhaifu sana. Mtoa mada anazungumzia ubovu wa huduma za afya wewe unaleta mambo ya mke.
Inahusiana vipi sasa?!
 
Kwani tozo hatulipi? Na hosp ya Mnazimmoja ni ya Leo? Ilipaswa kama ni maboresho ya vituo vya afya ingetakiwa ipate maboresho no 1, Maana ipo katikati ya jiji.

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
Kila sehemu Kuna mahitaji ya hivyo Wala hapo mnazi mmja hapana huo upekee,la sivyo nenda hospital kubwa zote ziko hapo hapo Dar..

Mwisho mlikataa kulipa tozo Hadi Serikalini ikaamua kuzifuta na kupunguza sana kiasi hakuna kitu Cha maana wanapata.
 
CPR ni huduma ya kwanza muhimu sana kwa mti aliyeshikwa na ugonjwa wa moyo, cha ajabu watu wengi hawaijui. Hii usipomfanyia mgonjwa kabla ya kumpeleka hospital, basi elewa ukimkimbiza hivyohibyo unaweza kufikisha maiti au mahututi wa kuelekea kukata roho.

Hii inahusisha kukandamiza kifua mara kadhaa huku ukimpulizia mgonjewa hewa nzuri.
Yah,kwa tuliyopitia ubaharia na kuwa sehemu fulani fulani hii kitu tumefundishwa sana
Na tunaimudu haswaaa
Je kwa kizazi cha sasa watoto, watu wanafundishwa masuala haya ?

Ova
 
Ndio lemutuz alikuwa na shida ya moyo ila kuna kuna mambo yalichangia kifo chake.

1: lemutuz anaishi peke yake wenda alipodondoka walinzi walimuona muda umeenda, wenda angekuwa na mke angemkimbiza hata mhimbili na sio mnazi mmoja.
2: ex bf wangu alinifundisha huduma ya kwanza pale mtu anapo dondoka gafla na akasititiza kila mtu anatakiwa kujua hii huduma.
Mtu akidindoka gafla unatakiwa kuweka mikono miwili pale kifuani kwenye moyo na kumshutua kwa nguvu kuamsha mapigo ya moyo. Sasa wale walinzi hata kabla ya kumpekeka hospital ilibidi wajaribu hiyo huduma wenda angezinduka.
Miaka iliyopita nilikuwa natokea mjini nikashuka kituo kimoja nikakuta mmama kadondoka watu wamejaa pale eti wameagiza gari wampeleke hospital.

Moyo ukaniambia sogea pale uone nn kinaendelea nikakuta mmama kalala flat kabisa nikakuta mtu anampepea nikamwambia weka mikono miwili hapo kwenye kifua mpamp kwa nguvu alifanya hilo zoezi kama mara 7 hivi yule mama akatoa sauti mmmmm na kupumua kama mtu aliechoka na akatikisa mguu. Mpaka gari linakuja alikuwa anapumua wakampeleka hospital.

Jamani tunatakiwa kujua hizi huduma za kwanza ndogo ndo ingawa mwisho wa siku Mungu ndio muamuzi.

Lemutuz kuishi peke yake plus stress za mtoto wake kumtukana ndo maana kila siku alikuwa akienda batani may be alikuwa anapunguza stress. Coz angekuwa na mtu wa kumjali alipo kuwa huko batani angeulizwa mbona umechelewa kurudi? Uko wapi? Na alipofika hata angedondoka mkewe ndo angekuwa wa kwanza kujua mme wake hospital ipi inamfaa kutokana na tatizo lake.

Hakuna kitu kibaya kukosa mtu wa karibu wa kukujari.
Apumzike kwa amani maana aliishi maisha ya kusimangwa kisa mtoto wa mchepuko, kila siku yeye ni kuji defend as if alituma maombi azaliwe. Rip lemutuz.
Angalau wenzetu wana ile mtu kazidiwa unapiga ile namba ya emergency wanakuuliza amepatwa na nini unaeleza wanakupa tips za kufanya ukiendelea kusubiri huduma ya kupelekwa hospitali.
Sisi huku hatuna na wala hatujui.
Serikali na wadau wa elimu wangeingiza hii watu wajifunze mashuleni kama somo la huduma ya kwanza angalau tuwe na tips chache za kusaidia mpaka nchi itakapokuwa na uwezo kama wenzetu.
 
Back
Top Bottom