Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Wanamlipa sh. Ngapi sisi ndio tunamjua huyu ndio mana tunasema hivi Katelekeza Familia yake New york kwa rafiki yake halafu useme analipwa sijui nin nin upambanaji kukimbia familia
Unasema amekimbia familia kwani ww ndio ulikua unashika miguu wakati wanakwichkwich?? Mambo ya familia yana mambo mengi usikute mwanamke alikua anamfrustrate akae tu kwa vile yeye ana moyo wa chuma?? Wangapi wamekimbia familia na ni hapo hapo dar?? Le mutuz yuko vizuri sasa nimeanza kumuelewa.
 
Huyu jamaa akili yake ina matatizo, nashangaa watu wanavyompromote ## jamaa ana stress za maisha ## ana hitaji msaada wa kimawazo
 
Mkuu humu kwenye story zake ndo nimemuelewa jamaa anapigana vita isiyokwisha ndio kuna pahali kasema vita ya mauti.
Hajamtaja mtu ila ukiconect dots unajua kitendo cha yeye kurudisha majeshi bongo hakikufurahiwa ndo pale alimention imekua threat kwamba ataclaim Mali za baba akifa .
Simple mathe .
Dr Mwelee Malecela daughter. (Goodmother to Mange).
Le Mutuz Malecela son (shame to a family )
Ipyana(rip)and others dnt know nothing .
The battle is big , mi nimepitia haya mambo so i know,i give respect to blaza le mbamia himself.
 
Kwa hilo la uwezekano wa kukimbia child support, ndo maana nikasema sina uhakika walitengana lini lakini kama walitengana wakati wa hustle zake, unachosema ni 90% possible manake ambacho kingebaki hapo ni yeye kugeuka msukule wa mwanamke in the name of child support.

Kuhusu malipo kwa trucks drivers ni kweli manake nilishawahi kufanya freelancing job as a Freight Agent (Logistics) with a US shipping logistics agent. Anyway, ilikuwa ni kazi ya kijungu meko na bora mkono kinywani lakini pamoja na yote hayo, kwa CDL Class A Drivers (kama ambavyo Le Mutuz amesema nae alikuwa hivyo); wao wanalipwa vizuri sana!!

Lakini yote hayo, mbele ya child support, bado unaweza kugeuka kuwa msukule tu!

Hilo la siasa zake, ah! Binafsi hata page yake huwa sikumbuki nimewahi kutembelea lini na anachonikera zaidi ni aina ya siasa zake.
 
Ushasafiri kuishi nje we mpuuzi .
Le Mutuz ana family na watoto huko US.
Mkiachana kisheria mke anamilikishwa kila kitu alee watoto.
We unatolewa live kwako na bado unapigwa palanja asilimia kadhaa za mshahara anapewa yule ex.
ndo mana mkubwa Le alisoma alama za nyakati akarudisha majeshi
 
We're 99.9% even...
 
PART 10:- "MY AMERICAN EXPERIENCE" .

.kesha Saa Kumi Asubuhi nilikua nimeshafika Yard at the Bronx Terminal nikaanza mazoezi ya kuendesha ili nikafanye mtihani rasmi wa kuendesha nishinde nitimize ndoto yangu ya kuwa na kazi ya Uhakika na Mshahara mzuri yalikua yamebaki masaa 3 yaani from Saa Kumi Asubuhi mpaka Saa Moja Kamili.


Niliyopangiwa kuingia mtihani so hapa Yard nilikua najaribu kukumbuka kila kitu kinachotakiwa ili nikifanye kwenye mtihani niweze kushinda so Saa Kumi na Mbili na Nusu Errol Mzee Mjamaica aliyenifundisha sana hii kazi alikuja na ndiye aliyekua ananipeleka kwenye mtihanl maana ni lazima uende na Dreva mwenye Leseni.


Mzee Errol akaniambia "African najua utashinda na afanya mambo makubwa sana yako maana una akili sana" akaniuliza "Hivi Waafrika wote wana Akili kama wewe?" sikumjibu kitu zaidi yan "Twende kwenye mtihani imebaki Dakika 30.

tukaondoka mimi naendesha yeye amekaa pembeni tulipofika mahali pa mtihani Inspector Maalum toka New York City Department of Motor Vehicle akaingia ndani ya Truck akimuashiria Errol kushuka na yeye akakaa pembeni akaangalia makaratasi yote yanayohusika na akaniuliza "wewe ndiye ulikua unaendesha mlipokua mnakuja?" nikamjibu "Ndio" kwa mshangao mkubwa sana Inspector akaniambia "Jinsi ulivyokuja hapa mpaka uka Park hili truck sihitaji hata kukufanyia test maana nina kazi nyingi sana so nakupa leseni yako.

I almost fainted kwenye kiti cha dreva nilipakua nimekaa infact machozi yalinitoka sijuii kwa nini Boom Inspector akanipa mkono na kunitakia heri "Good Luck".


Mzee Errol akarudi na kuniuliza kwa mshangao kwanini sijaenda naye kwenye mtihani? nikamuambia kilichotokea ...

Dina mmiliki wa Kampuni yetu American Harzadous Waste Inc. akapiga simu hapo hapo kuulizia matokeo nikamuambia kuwa nimefanikiwa akaniambia ukirudi ofisini nina zawadi yako..


.Mzee Errol kwa mshangao makubwa sana akaniambia African mpaka Mzungu mwenye Kampuni anafuatilia leseni yako? You mean a lot to those White folks" akaongeza "ukiona Mzungu anakufurahia mweusi hivi ujue kesha ona potential yako ya kumuingizia pesa tukarudi Yard nikaagana na Mzee Errol nikaenda ofisini kwa My Big Boss Dina ...ITAENDELEA! 11
 
PART 11:- "MY AMERICAN EXPERIENCE"

my Bosi Dina nilimkuta na Mume wake Russ anisubiri 0fisini nikapiga nao Breakfast Dina akanipa,Bahasha yenye USD $5000 akaniambia ni zawadi yangu kutoka kwake kwa kushinda Leseni na akanipa Majukumu mapya kuanzia Jumatatu inayofuatia kwani alinipa Likizo ya bure ya Wiki Moja akaniambia kazi yangu mpya na Maalum sana itakua kuzifanyia kazi Hospitali kubwa tu za Downtown Manhattan ambazo aliniambia zimekua zikiwasumbua sana Madreva wote wengine akasema Utakapo rudi Jumatatu nataka uje na pln

namna utakavyofanyia kazi kila siku" na cha msingi zaidi akaniambia Sasa unahitaji kuachana na zile kazi zako za usiku hii kazi moja itakulipa pesa za kutosha nikamjibu kua ni sawa sina tatiza ila Ninataka kusoma College Usiku" akaniambia hamna tatizo.


Hospitali kubwa Manahttan nilizotakiwa kuzipigia kazi ni Memorial Sloan Hospital, Columbia Hospital, Harlem Hospital, Lenox Hill Hospital, Lower Manhattan Hospital, Mt. Sinai na Berth lsrael hizi ni Hospitali kubwa sana na zenye Harzadous Waste Materials nyingi sana zikaishia kuwa my territory ya kazi kwa Miaka Mingi Sana ....baada ya Dina kunipa zawadi nikaamua kwenda Miami Florida kupumzika nikanunua tiketi ya ndege dola 300 Disneyland Five Star Hotel siku Tano so haya mambo sikuanza leo nilitumia jumla Dola 1000 safari nzima then nikarudi kuanza kazi yangu rasmi

nikamuomba Dina ili niifanye kwa ufanisi niwe ninaanza kazi Saa yoyote ninayotaka Usiku akakubali nikafanya mipango na Mabossi wa Hospitali zote wakanipa ruhusa ya kwenda muda wowote ninaotaka as long as watu wao watakua wamenitayarishia mzigo wa kuchukua now kazi yangu ilikua ni kuja na Trailer tupu lenye Makontena masafi ya kuwekea Harzadous Waste ninabadilisha na kuchukua lililojaa Waste in one month nilikua nimetatua tatizo sugu liliowasumbua Hospitali na kampuni yangu kwa muda mrefu Sana .

there l was hahahaha mshahara wangu now ulikua ni Dola 15 kwa Saa na Overtime ambayo ni Dola 30 kwa Saa na nilikua napiga masaa kuanzia 50 mpaka 100 kwa wiki nikaanza kua na Uhakika wa Dola 1800 mpaka 2000 kwa wiki so now ikawa lengo langu la EDUCATION kupata Elimu nikaanza kutafuta Shule nikapata Upstate NY ...ITAENDELEA! 12
 
Aliingia na Kutoka before.
Sio mada,we unayejua nielimishe
Au unaongelea multi viza? Entry ni kama unavyokwenda Nairobi au South Africa tu hupaswi kuomba viza ubalozini bali unagongewa entry kwenye boda utakayoingilia.

Multi viza ni viza unayokuruhusu kuingia na kutoka kwa muda wote wa validity ya viza yako.

Kwa mfano sasa hivi Marekani hawatoi single entry wanatowa multi viza one year.
 
Tatizo mijitu mingi humu haijatoka nje kwahio haijui maisha ya ma membelez. Ukishadivorce huko utapaona pachungu ni bora ujirudie bongo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…