Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Le Mutuz: Historia ya kweli juu ya maisha yangu (My American experience)

Why compare his hustles with others? Uliposema tuu "Lemutuz cha mtoto" tayari hayo ni mashindano


Lakini kuna watu wamehustle kivyao mpaka wameitoa na wanapiga kimya tu. Kama hayo unaita ni mashindano ya shida, then okay.
 
Ndani ya Basi la Greyhound kutoka Ottawa/Canada tunaelekea New York City/USA nilikuwa ninawaza nitakapofika New York City itakuwaje? Simjui mtu so sitakuwa na mahali pa kulala JE ITAKUWAJE?................

Kuna Mbongo mshikaji wangu nilikuwa na namba yake ya simu aliahidi kuja kunipokea lakini dakika ya mwisho HAKUJA nikashuka na begi langu dogo la nguo kama kawa nikakuta Ma Homeless kibao wanajitayarisha kulala so nikatafuta mahali saafi nikatoa Blanketi langu

naomba ufafanuzi.......humjui mtu ila kuna mtu umempigia aje akupokee
Hili jamaa ni liongo kwelikweli, kuna matutusa yake humu hayajawahi hata kufika Nairobi ndio wanavutiwa na porojo zake.
 
Unajua wewe jamaa ni mbishi sana?? Sasa mie nakuambia hapa huko bongo niliacha kazi niliokua nikifanya customs kila siku nikitoka job nina kama tshs 2m. Nikaja huku US nikaanza kazi za kubeba mabox kwanza huku nasoma hadi sasa nimekaa vizuri nina kazi nzuri na familia na maisha yansonga msuano. Itakuwa kuacha ubaharia kazi ya kukaa miezi 6 majini tu. Hio kitu acha kabisa inaitwa sacrifice. Na hapo le mutuz ni kua dad ake alikua PM lakini aliamua kuingia front mwenyewe kwenye kikosi cha mizinga kujilipua. Acha ubishi wa kwenye ghahawa za saigon .
Kwahiyo kwa wiki ulikuwa unatengeneza Tsh Millioni 10 na ukaacha kazi!![emoji3] [emoji3]

Anyway wapo mazezeta wenzako humu watakaokuamini kwa hizi porojo zako.
 
Kuna wazee wanazeeka vibaya nisaidie mungu nije kuwa mzee mwenye busara
 
Hahaha najua unatania, mark hataki attention ili watu wa muone, yupo bzz kufanya coding ili imuingizie pesa ndo maana hajuagi fassion mpya za nguo anaangalia acc inasoma billion ngapi. Mambo ya kuvaa wamewaachia watu weusi km akina PDidy, Nelly nk kwakuwa hawana kitu kichwani. Yaani km anavyoelezea Le mutuz ndo napata picha ya Nigers
We kweli mburula unasema mtu kama pdidy hana kitu.
 
PART 17- "MY AMERICAN EXPERIENCE"


nikaanza Dating tena baada ya kuacha kwa muda mrefu sababu ya kuteswa na kivuli cha Ericka nikaanza na Msichana Nigga kwenye picha kwa jina Antoniette with experience ya Ericka nilikua ninayo idea tayari ingawa huyu now was Black ni tofauti kabisa alikua anafanya kazi ila anaishi na Mama yake mzazi aliyekua na Uwezo mkubwa sana wanaishi Uzunguni North

d0ea0900a4b9c8514ed738ce0768f731.jpg


mimi ninaishi South in USA always kuna o Class ya North kwa wenye Uwezo na South kwa Masikini pia alikua na Dada zake 2 Mmoja Light Skin na mwingine Mweusi.


Katika kutumia rule ya Divide and Rule yaani kuwagawanya Weusi ili wawatawale sawa sawa Wazungu walifanya makosa ya kibinadam ya kutembea na Watumwa wakaishia kuzaa watoto ma Half Aibu yao Wazungu wakaanza kuwa treat wale watoto wao Cast k tofauti na Watumwa wengine wakawafanya Superior kuliko wenzao weusi kabisa ni Ugonjwa walipandikiza kwa weusi mpaka leo wa kuamini Half Cast ni bora recently.


nimeanza kuona Ugonjwa huu ukiingia mpaka Bongo na kama ilivyo USA kwenye Movies na Music Videos msichana mzuri lazima awe Mweupe so Blacks karibu wote huwa ni lazima wawe na mtoto mmoja Half Cast ambaye Mama aliamua kwa makusudi kuzaa na Mzungu au Bwana mweupe ili apate mtoto mmoja mweupe.


so huyu ndiye anakuwa kipenzi cha Mama always kuliko wote wengine cause ni mweupe na yeye anakua na majivuno ya ajabu sana so my Babe naye alikua na Dada mmoja kwa jina Shawn mweupe ila urefu wangu na kupiga kazi sana ukamfanya huyu Dada mtu anipende sana na kwa sababu yeye alinipenda na Mama mzazi naye akawa hana Choice ila kunipenda so na Antoinette naye akani penda sana ila hakua na Elimu kubwa ingawa alikua na kazi nzuri ya Serikali.


now Shawn akaanza kunishauri nihamie nyumbani kwaa kwa vile hawana Mwanaume kwenye nyumba nikaanza kutafakari idea huku nikijiuliza maswali mazito sana ya maana halisi ni kua MARIO yaani nataka kutunzwa na Mwanamke na familia yake nilikua najichekea mwenyewe peke yangu nikakumbuka mafundisho ya Jandoni kua Mwanaume huwezi kutunzwa na Mwanamke how can I do that now?

but nikihamia kwao nitaokoa Dola 1,000 za kodi ya nyumba kila mwezi JE NIHAMIE AU NISIHAMIE? ....ITAENDELEA 18
Huo ni uongo halfcast ni nigga tu hakuna et higher class
 
Back
Top Bottom