hongera story yako ni nzuri, ila mwanamke wako aisee ni kichwa maji sana. hata hivyo, tumesikia upande wa kwanza, kwetu sisi wanasheria umetuaminisha kuwa mwanamke ni wa aina hiyo, tukisikia upande wa pili nao ulete story yake hapa, usijeshangaa mambo yanabadilika ghafla. kwetu sisi wanasheria, huwezi kuamua kesi kwa kusikiliza upande mmoja, kila mtu ana story yake, lakini kwa harakaharaka, kwa kadiri nilivyoanza kukufuatilia nimeamini wewe huwa unaongea kilichopo moyoni na kuna uwezekano mkubwa ukawa mkweli.....umeshaestablish primafacie case inayohitaji x wako au watu wengine wanaokujua upande mwingine wajitetee ili jamii itoe hukumu kwa either kujifunza au kuwakosoa. but generally, kuna jambo kubwa sala la kujifunza kwenye maisha yako, na kwa mwili wako huo angekuwa mtu mwingine angeshakufa kwa pressure zamani sana, au angeshapata stroke...utakuwa uliumia moyo sana.