Le Mutuz (W. Malecela) Vs Alberto Msando: Hii ni vita ya kupigania haki za wasanii au kopo la Coca?

Le Mutuz (W. Malecela) Vs Alberto Msando: Hii ni vita ya kupigania haki za wasanii au kopo la Coca?

Status
Not open for further replies.

Leak

JF-Expert Member
Joined
Feb 22, 2012
Posts
52,916
Reaction score
43,505
Wajamvi wasalaam.

Kuna vita ya maneno imezuka na inayo endelea kati ya Lemutuz na Mwana sheria Albert Msando.
Hii vita ya maneno imezuka baada ya kampuni ya Coca-cola kutangaza kampeni ya kuweka majina ya watu maarufu kwenye makopo ya Kinywaji cha Coca-cola na bila shaka hii vita imezuka baada ya wawili hao kushindwa kuelewana kwenye hili swala maana kila mmoja ana malengo yake.

Lemutuz ameonesha kuwa Msando ana wivu kwa kuwa jina lake halipo kwenye list ya watakao wekwa kwenye makopo huku Msando akisisitiza kuwa Wasanii wasikubali kuwekwa Majina yao kama hawalipwi na akisema kukubali hilo ni kukubali unyonyaji.

Kimsingi Alberto Msando amepinga wasanii anao wasimamia kukubali kuwekwa majina yao kwenye vinywaji hivyo bila malipo yeyote yale. Na katika hili nami naungana na Msando kuwashauri Wasanii wote au watu maarufu kutokubali mpango huu wa kutumika majina yao kuwatajirisha Coca-cola.

Kimsingi Coca-cola watatumia Majina ya Wasanii na watu maarufu kuingiza pesa huku wenye majina wakibaki watupu mifukoni! Hakika hili litatokea Tanzania pekee kama watu watakubali kutumiwa bure.

Kuna watu wako tayari kutumiwa bure lakini hawa Wasanii wetu kwakweli itakuwa ni aibu sana na sitaki kuamini kama Coca-cola wana mpango wa kuwanyonya Wasanii kwa njia hii huku wao wakitajirika.

Wasanii wanatakiwa kuonesha msimamo wao kwenye hili na kulipinga na wahakikishe wanalipwa ndio wakubaliane na mpango huu.

Katika hili kuna mmoja anapigania haki za Wasanii na mwingine anapigania kopo la Coca-cola
Karibuni wanajamvi.

attachment.php
attachment.php

 
Haaaahaa duh hapo sasa Coca cola wanajua udhaifu wa celebs uchwara wa Bongo inawezekana vipi watumie majina yao bila malipo,naamini celebs wanaojitambua hawawezi kukubali majina yao yawatajirishe wengine ila kuna ambao kuona majina yao tu kwao mafanikio tosha.
 
Kwani Coca wamesema nan kalipwa nan hajalipwa? Inawezekana le mutuz anafanya hivo ili malipo yazidi kwa kuwekwa jina lake na kuitangaza coke zaid. Na amesema well kwamba ukiamua kuelimisha sio mpaka utukane.
 
Tatizo la msando anataka kuwachukulia wasanii au viceleb vya bongo vyote vijinga na kwa kiasi kikubwa kawawin wengi amesahau kama Le mutuz kuna mambo huwezi kulipeleka. ..ujue ukiwa mtoto wa town hata ukiwa boya kiasi gani huwezi kupelekeshwa na mtu wa mkoani. ..Le mutuz town moja,msando mkoa moja
 
Kwani Coca wamesema nan kalipwa nan hajalipwa? Inawezekana le mutuz anafanya hivo ili malipo yazidi kwa kuwekwa jina lake na kuitangaza coke zaid. Na amesema well kwamba ukiamua kuelimisha sio mpaka utukane.

Nimeshindwa kuweka attachment ya maandishi ya Msando anasema hili swala ni bure na amewakataza wasanii anao wasimamia kama Ay na Mwana Fa kukubali majina yao kuwekwa bila malipo! Me mwenyewe mwanzo nilidhani wanalipwa lakini hawalipwi! Nitashangaa wasanii kukubali hili swala!
 
Haaaahaa duh hapo sasa Coca cola wanajua udhaifu wa celebs uchwara wa Bongo inawezekana vipi watumie majina yao bila malipo,naamini celebs wanaojitambua hawawezi kukubali majina yao yawatajirishe wengine ila kuna ambao kuona majina yao tu kwao mafanikio tosha.

Kwakweli me mwenye hadi sasa siamini kama Coca-cola hawawalipi lakini lakini Msando anaonesha hawalipwi zaidi ya umaarufu tuu! Hakika katika hili ndio tutapima uwezo wa wasanii wetu!
 
Yapo majina ya watu zaidi ya mia mbili unategemea watalipwa kweli?
 
Mbona yule bikra wa kisukuma nae naona anasema kuna mtu anaona wivu cos jina lake halipo.. nikajua anamuongelea le mutu
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom