LEAK: Document ya hukumu ya Godbless Lema HAPA

LEAK: Document ya hukumu ya Godbless Lema HAPA

Swala siyo lugha ni muda wa kupitia yote kwanza,hata hivyo makae mjue kua Serikali ya ccm inatumia sana mahakama kufanya yale yanayotaka yawe,wakati wowote wapinzani watapoteza tena jimbo lingine,haswahaswa la Singida Mashariki,kwa Lissu,kuna kampeni kubwa ya watu wa usalama na viongozi wa mkoa pamoja na mahakama kufanikisha hilo.
 
jamani kidhungu noma nimesoma sentesi za kiswahili tu zinatosha
 
Siaelewa unapose the document has been leaked. Hata kupata huku za mahakama imekuwa siri sasa?
 
Hivi huyu jaji angekuwepo arumeru mashariki akamsikia Lusinde sijui angesemaje?karibu mambo yote kuhusu Buliani ni kweli kwani hakuwahi kukanusha binafsi wala huyo Laigwanani wake
Mkuu, heshima mbele. Unaweza kupingana nami na kupingwa na wengi, lakini hoja ya msingi sio kuwa ni kweli au uongo yaliyosemwa dhidi ya Batilda. Tusi ni tusi tu. Hapa panazungumziwa matusi anayoshutmiwa Mh. Lema dhidi ya Batilda. Suala liwe kwa Mh. Lema kukata rufaa na kuthibitisha kuwa hakutamka maeneo hayo, na hata kama aliyatamka, kuwe na sababu za kujenga hoja kuwa yale hayakuwa matusi.

Nilishawahi kutoa maoni juu ya "dhambi" tunayoifanya ya kulinganisha ukubwa wa matusi. Hoja kuwa matusi ya Lusinde yalikuwa makubwa zaidi, yasichukuliwe kama kigezo cha wengine kuhalalisha kutukana "kidogo" halafu waende kulinganisha na matusi ya mwengine.
 
mliosoma vizuri someni
mtudadavulie na sisi akina maimunaz.
 
Wadau msiiogope lugha ya kawaida hiyo ngaja tuipitie tuone madudu ya Mhaya Rwakibarila
 
lugha ya kimahakama ni ngumu kama sio mwanasheria lazima ushike kamusi.
 
TISS ni zaidi ya JF. Maana JF waliipata kabla hata haijasomwa. Mmesahau kuwa JK alikuwa na hukumu hata kabla haijasomwa? Mmesahau CCM walikuwa na hukumu hata kabla haijasomwa?
 
Jargon nyingi sana humo hatuwezi kusoma, by the way kwanini mahakama ya Tanzania inatumia kimombo?

Naomba tuweke kwenye katiba mpya KIswahili kitumike, maana kesi inaendeshwa kiswahili hukumu inaandikwa kimombo wakati kuna maneno mengine hayatafsiriki kirahisi.
 
Kwa uelewa wangu mdogo wa sheria: Kinachokosekana hapa ni kile sheria huwa inasema: "Prove beyond reasonable doubt". Sidhani kama mahakam iliridhika na ushahidi wa midomo tu ya watu pasipo kuwa na vivid evidence kuwa Lema aliyatamka hayo maneno. Mimi naona Judge hajatenda haki kwa kukubali ushahidi wa mdomo wa upande wa mashitaka na kuukataa ushahidi wa upande wa utetezi. Kesi kama hii Lema akiambiwa alete mashahidi wengine ambao si wananchama wa chadema atashindwa kuwapata? maana kigezo cha kuukataa ushahidi wa Lema ni kwa kuwa baadhi yao eti ni wananchadema. Je kama akiweza kuleta mashahidi ambao si wananchadema na wakashudia kuwa hakutamka hizo statements, je hukumu hii itakuwa validi? Mimi ninacho amini hukumu lazima iwe imetumia ushahidi ambao haunamashaka na hata kama utakuwa subjected to any challenge bado utabaki intact na hukumu haiwezi kubadilika. Hapa hakuna "BEYOND REASONABLE DOUBT"

Nikionacho mimi hukumu hii haikupata evidence amabazo ni "beyond reasonable doubt" kumfanya judge atokea hukumu kama hiyo. Tulitegemea mashahidi wa upande wa utetezi wangepeleka ushahidi kama wa recored voice ya Lema au maandishi ya vyombo vya habari au evidence ya mashitaka kama ya udhalilishaji aliyofanyiwa batilda. Ushahidi wa mdomo tu ni ngumu kujilizisha kuwa mashahidi hawa hawakuwa na masilahi ya kuhongwa kufanya hivyo. Judge ametumia kigezo dhaifu kudai kuwa wale mashaidi walikuwa genuine kisa tu eti walikuwa wa kada tofautitofauti na hawakuwa wananchama wa ccm.

Mwingine anaweza kuongezea au kuchallenge mtazamo wangu.
 
Hivi hizi hukumu za namna hii zinaruhusiwa kweli, ni kweli watanzania hatujui sheria lakini mbona hii hukumu inaonyesha kabisa kwamba niya ni kudholotesha maisha ya wapigania uhuru wa tanzania ambayo iko chini ya mkoloni sisiem!

Hakika ningekuwa kiongozi wa chadema ningemchukulia hatua lusinde kwa matusi makubwa waliyokuwanayatoa arumeru yeye, mkapa pamoja na wasira, waziri asiyekuwa na nidhamu kabisa.

Lakini ikumbukwe kwamba: ukitaka kula na kipofu usimguse mikono yake
! watanzania tumeshafunguka sasa.
 
Hichi kimomo cha sheria wengine ni sawa na mnatufunga Kamba shingoni na kutupeleka mahali tusipopajua"MASIKINI KABWELA MIMI"
 
Siaelewa unapose the document has been leaked. Hata kupata huku za mahakama imekuwa siri sasa?
Mkuu cha muhimu ni kuwa hiyo doc. imepatikana. Suala la ku-leak au kuto-leak sidhani kama ni muhimu.
Kama ingekuwa ni rahisi kupatikana kama unavyotaka kujigamba, kwa nini wewe umeshindwa kuileta hapa?
 
Wadau nimepitia hukumu ya huyu jaji na ninaona inamapupungufu makubwa. Hakukuwa na ushahidi wa kiwango cha kutosha kuweza kuthibitisha kama kweli yale maneno yalitamkwa na LEMA. Ushahidi umetolewa wa mtu mmoja mmoja kwa kila tukio. Kisheria ushahidi huu ni sharti uungwe mkono vilivyo na ushahidi wa mtu au watu wengine yaani uwe collaborated. Hili katika kesi hii halikufanyika there is no collobarative evidence on all the alleged events!. Suprisingly, katika siku za leo hii nilitegemea maneno yao yaungwe mkono na picha ya video etc au recorded speech lakini hili hakuna na jaji kaliachia na kudhani wamethibitisha madai yao on balance of probability

Pili Walalamikaji hawakwenda kuthibitisha ni vipi maneno yale yamewaathiri wao kama wapiga kura katika huo uchaguzi ukizingatia wengine wanakiri katika ushahidi wao hawana chama wala maslahi yeyote ni vipi sasa wameathirika? Na kama wakisema Buriani ndiyo ameathirika then wao hawan haki ya kulalamikia hilo yao cause of action. Kwani kwa tasfiri ya jaji mtu yeyote mwenye kitambulisho cha kupiga kura anahaki ya kuleta malalamiko yeyeto dhidi ya mgombea. Nadhani hii sio tafsiri sahihi lazima kuwe na mipaka ya kile mlalamikaji anachokileta na kipimo kiwe yeye kama yeye ameathirika vipi...

Kwa sasa ni haya wadau tuendelee na analysis ya judgememt!
 
Jargon nyingi sana humo hatuwezi kusoma, by the way kwanini mahakama ya Tanzania inatumia kimombo?

Naomba tuweke kwenye katiba mpya KIswahili kitumike, maana kesi inaendeshwa kiswahili hukumu inaandikwa kimombo wakati kuna maneno mengine hayatafsiriki kirahisi.

Hii hukumu haikuandikwa na Rwakibarila, Imeandikwa na Dr Masumbuko Lamwai, Rwakibarila kapewa desa tu hapo na kusoma na kuandika jina lake. Hii ni 'miscarriage' kubwa sana ya justice kuwahi kutolewa na mahakama kuu.
 
Back
Top Bottom