Lee Min Ho na plastic surgery zaidi ya 12 usoni

Lee Min Ho na plastic surgery zaidi ya 12 usoni

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2019
Posts
3,862
Reaction score
6,438
Sikuwahi kuwa Shabiki kindaki ndaki korean DRAMAS , Aidha ipambwe na ihit sana mtandaoni hapo ningejisogeza nipate kuangalia

Kutokuwa shabiki wa movie hizo haimaanishi hawajui hawa jamaa kwenye movie zao wako makini mno
Movie zao ni kali shout out kwa "Waongozaji wao"

Kwakweli movie zao ni kali ila maswala ya watu mnakutana Episode ya kwanza mnakuja Kudate Episode ya Mwisho mimi yalinishindaga kwa kweli ,,, kitu cha mzungu mzee Episode ya kwanza tu Washangonoka(,jokes,)

Dada zetu ndiyo wapenzi haswa wapenzi wa korean Dramas ,

Ndiyo kusema kwamba baadhi magirl wangu, nliowahi kupita nao huko nyuma , walikuwa wananisukuma kucheki hizi movie hasa tukiwa wote,hapo kidogo ningefatilia

Na nlikuwa najua kama nashare na mchizi Lee min hoo maana daah Wadada huwaambii kitu kwa huyu mwamba....Isiwe kesi as long as nlishare na Star wa movie duniani basi mambo yente japo yeye alikuwa hajui.🤣🤣🤣

Pongezi kwa Pisi yangu ya sasa ,maana wanasema utampata wa kufanana nae , Huyu anapenda Kubeti, Shabiki wa arsenal na anakula Moshi kama kawa.,binti huyu wa mombasa Anatafuna hadi miraa
Asante mama mkwe kwa kuniletea huyu kiumbe Duniani ubarikiwe sana popote ulipo

Turudi kwenye madaa

Nadhani wengi wetu tunamfahamu mwamba Lee min hoo ,

Muigizaji wa Korea Kusini na mwanamitindo Lee Min Ho, aliyejulikana zaidi kwenye kazi zake "BOYS OVER FLOWER" na "CITY HUNTER", na nyingine nyingi zilizofanya poa kunako soko la Dunia

Hizi tetesi tulianza kuziskia muda mrefu inasemekana kuwa mwamba kapigwa kisu cha upasuaji wa plastiki ili kuboresha Sura yake

Screenshot_20210228-074200.png

Hili linaipa nguvu sana kutokana na na KOREA kuwa nchi kinara kwa ufanyaji wa plastic surgery ikifwatiwa na THAILAND

Lee Min Ho, inakisiwa kufanya upasuaji wa kubadilishi muonekano wake, akitengeneza pua yake, kapiga sindano ya kutengeneza midomo (lips) ,kupunguzwa kidevu na kunyoshwa sura

Screenshot_20210228-074520.png

Hata hivyo madai mengine yanaidai sasa hivi sura Imekuwa nyeupe zaidi ya mwanzo. ni zaidi ya Surgery 12 ndizo alizofanyiwa "inasemeka"
 
Nimetizama Korean drama nyingi kiasi chake Naona Kuna mastar wengi huwa Wanafanya vizuri kumzidi Kama ile series ya city Hunter Mimi sijawahi kuielewa kabisa hauwezi kui- compare na bridal mask au Ile IRISH(sijui ndio inaitwa hivyo)

IRISH episode 1 mpaka 4 Ni balaa Ni series haswaa ya kijasusi
IRIS ndio series bora ya kikorea iliyobamba ulimwenguni na kuwa rated sana kuliko series yeyote huko korea
 
IRIS ndio series bora ya kikorea iliyobamba ulimwenguni na kuwa rated sana kuliko series yeyote huko korea
Aaahh ile series unaweza ukalia Yaani changamoto alizokuwa anapitia yule Sterling na demu wake Ni balaa na nusu

Yaani unaona kabisa yes hii kweli ni series ya kijasusi ila huyo Lee min ho sijui naonaga hamna kitu kabisa hauwezi kumfananisha hata na yule jamaa aliye act series ya city Hunter Yaani unatazama series mpaka una wish isiishe
 
Kumbe siko peke yangu [emoji16][emoji16]

Jamaa sijawahi kumuelewa
Nikiri kwamba nilianza kuangalia korean drama kwenye ile series ya jumong.

Nilikua najua kwa jamii ya watu wa asia wakicheza movie katika mazingira ya kifalme au ya kibush kama flying swords, taichi master, true legend basi movie inakua ina mkono mwanzo mwisho

Jumong ndio ilikia series ya kwanza kuni prove wrong, wanaruka ruka tu na mashuka yao mpaka episode inaisha ni mizunguko tu sijui mwana wa mfalme katoka gogolio kaenda kupeleka umbea

Ilinishinda kwa kweli
 
Aaahh ile series unaweza ukalia Yaani changamoto alizokuwa anapitia yule Sterling na demu wake Ni balaa na nusu

Yaani unaona kabisa yes hii kweli ni series ya kijasusi ila huyo Lee min ho sijui naonaga hamna kitu kabisa hauwezi kumfananisha hata na yule jamaa aliye act series ya city Hunter Yaani unatazama series mpaka una wish isiishe
Ile series imetulia sio utani mpaka kuna muda nikawa nahisi idea ya ile movie haikutoka korea. Kutokana na u wack wa movies za korea nilijijengea dhana hiyo na mpaka leo nina wasiwasi huenda nilikua sahihi

Ile series iko na part two na zote ni kali zimetengenezwa kwa weledi mkubwa sana ni unpredictable. Hii series ndio iliyoutambulisha ulimwengu kuwa korea nako kuna waigizaji.
 
Nimetizama Korean drama nyingi kiasi chake Naona Kuna mastar wengi huwa Wanafanya vizuri kumzidi Kama ile series ya city Hunter Mimi sijawahi kuielewa kabisa hauwezi kui- compare na bridal mask au Ile IRISH(sijui ndio inaitwa hivyo)

IRISH episode 1 mpaka 4 Ni balaa Ni series haswaa ya kijasusi
Iris kile ni Chumaa mkuu , kaliii sana
 
Back
Top Bottom