Leeds United: Nyota iliyozimika katika ulimwengu wa soka

Leeds United: Nyota iliyozimika katika ulimwengu wa soka

Kweli, post umenigusa,Leeds kweli imepotea niliipenda baada ya gunners.
kuna dogo alikuwa anaitwa harte bek 3 atakuwa huyo aliye kushoto kwa Rio fednand,hatari,kwa"direct kick" na guu la kushoto,hatari sana.Nadhani Bartez anamjua harte.
Ukisikia askari anakufa na bunduki yake basi ndio hao leeds walishuka na utamu wao huyu mfaransa dacourt ilikuwa khabari nyingine huyo mtu.
 
Waliosimama kuanzia kushoto ni Mark Viduka, Danny Mills "kipara", Rio Ferdinand aliyevaa kitambaa cha unahodha na bila kumsahau beki Iane Harte bora wa kupiga mipira iliyokufa katika EPL baada ya zama za Denis Irwin.

Waliochuchumaa kuna kijana mtukutu Alan Smith, kuna mbabe Lee Bowyer, Oliver Dacourt na wa mwisho ni Harry Kewell.

Hapo kikosini wanakosekana Majemedari kama Lucas Radebe, Robbie Keane na wengineo.

Uwanja wao wa " ELLAND ROAD " ulikuwa mgumu sana kwa sisi Man Utd.

cc Guasa Amboni
Mzee mwenzangu shukurani nyingi kwa mwaliko huyu rapa ana asili ya uchokozi na uchochezi mada zake nyingi hutufanya tujione kama matukio yametokea jana kumbe ni zaidi ya miongo miwili.
 
Unamaanisha nini unaposema wamepotea katika ramani ya soka la Uingereza ilhali wapo Championship tokea walipotoka EPL hadi sasa...

Na ligi ya Championship ni ngumu kuliko baadhi ya ligi nyingi tu kubwa barani Ulaya, kwa mtazamo wangu ni ngumu kuliko hata Ligue 1...
Fuatilia vyema historia yao mara baada ya kushuka
 
Unamaanisha nini unaposema wamepotea katika ramani ya soka la Uingereza ilhali wapo Championship tokea walipotoka EPL hadi sasa...

Na ligi ya Championship ni ngumu kuliko baadhi ya ligi nyingi tu kubwa barani Ulaya, kwa mtazamo wangu ni ngumu kuliko hata Ligue 1...
Ni kweli kabsa hiyo ligi ni ngumu mno
 
Huu uzi umenifanya niwakumbuke watu hawa wawili japo hawakupita leeds United wa kwanza ni Reuel adrian fox chuma hiki kilikuwa tottenham na Newcastle winga matata sana ya kulia mzaliwa wa Ipswich town huyu jamaa mwingine ni Chris Armstrong aah jamaa nilikuwa namkubali miaka hiyo ya 90 katikati shughuli yake pale mbele ulikuwa unaburudika. Palikuwa na gazeti linaitwa the shoot lilikuwa likitoka kila mwezi basi hapo ndio tulikuwa tunapata khabari za ligi ya uingereza.
 
Unamaanisha nini unaposema wamepotea katika ramani ya soka la Uingereza ilhali wapo Championship tokea walipotoka EPL hadi sasa...

Na ligi ya Championship ni ngumu kuliko baadhi ya ligi nyingi tu kubwa barani Ulaya, kwa mtazamo wangu ni ngumu kuliko hata Ligue 1...
Daaah kweli man ...yani anayeongoza league anaweza kukalishwa na kilaza wa chini
 
Mimi namkumbuka Mack Viduka ndio alikuwa nyota wao enzi hizo, na Allan Smith kama sikosei naye alikuwa hapo
 
maendeleo yao yapoje mpaka sasa mkuu?
Naona wamerudi tena chini zaidi mwenendo wao ni kama Arsenal tu wanashinda game moja wanapoteza mechi 3......

Kwa kweli mpaka sasa sijajua ni kitu gani kilicho wasibu hawa mambwana naona kwenye ligi wapo nafasi ya 12 thou najua wakipambana wanaweza ingia kwenye zile zitu 4 zitakazo cheza play off....
 
Back
Top Bottom