Legacy huwa haitetewi

Legacy huwa haitetewi

Behaviourist

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2016
Posts
39,926
Reaction score
95,626
Legacy nzuri ya mtu huwa haitetewi. Legacy nzuri huwa inajitetea yenyewe kupitia mambo mazuri pamoja na matendo mazuri aliyofanya mhusika.

Ukiona kuna mtu watu wanatetea kwa nguvu zote kuwa ameacha legacy nzuri sana jua huyo mtu alikuwa ni laghai. Kuna watu wanatetea kwa nguvu zote kuwa kaacha legacy nzuri sana, hii inadhihirisha wazi kuwa alikuwa ni laghai. Kama Kayafa kaacha legacy nzuri sana basi aachwe ili hiyo legacy ijitetee yenyewe kupitia hayo mambo mazuri aliyofanya.

Alikuwa ni hopeless populist and hopeless sinner ambae alijificha kwenye chaka la siasa za propaganda ili kulaghai watu wajinga kuwa yeye ndiye yule ajae na wala wasimtazamie mwingine.

 
Legacy ya Magufuli bado itaendelea kuishi.

Hakuna atakaefuta legacy yake leo wala kesho.

Kikundi cha wahuni wachache kinapambana kila siku mitandaoni kupambana na legacy ya Magufuli.

Magufuli ataendelea kuishi kwenye mioyo wa watanzania wengi kwa mema na kwa mabaya lakini ataendelea kuishi kwenye mioyo yao.

Tusilazimishane, kila mtu amkumbuke Magufuli anavyotaka. Kama wewe utakumbuka kwa mabaya basi iwe juu yako na usilazimishe watu ama usitumie nguvu kubwa kulazimisha watu wamkumbuke unavyotaka.
 
Mbaka umemkumbuka basi legacy yake inajitetea!
Na inajitetea kweli kweli...
Screenshot_20210328-162203.jpg
Screenshot_20210324-224310.jpg
 
Ila kuponda ni ruksa? Namumbuka Lissu kwenye Bunge la Katiba alimshambulia Mwl Nyerere mpaka Mtei akamuonya kuwa aangalie vitu vya kuongea.

Kwaiyo ukimponda yule ambae watu wanaamini alifanya mema hawatokuacha..!!

Kwenye Soka huko vijana wa sasa wanasema Messi na Ronaldo ndo wachezaji bora wa muda wote, lakini wakongwe wa kwenye soko watakubishia na watakuuliza ulimuona Pele wewe? Ulimuona Marodona? Ofcourse itabadi uwatetee tu no way.
 
Mpenzi wako wa zamani uliyekosana naye zamani, ukafuta na no zake, ukifikia kipindi cha kuanza kukumbuka ubaya aliofanya Wakati huo, ujue utakumbuka na vitu vizuri alivyowahi kukutendea

Na ndicho kinacho/kitakachoendelea Kwa JPM, tusidanganyane, hakuna atayeacha kumkumbuka huyu Mwamba, vitabu vitaandika na historia yake haiwezi futika kamwe,

SGR, Itakaa zaidi ya miaka 300 Mbele na kila atayekujua Nani mwanzilishi, litatajwa Jina la JPM na sio la Lissu Wala Mbowe
 
Kitendo cha mtu kutumia akili yake na resources kusema kwa ajili ya Legacy ya JMP ndio kujitetea kwa hiyo legacy kwenyewe huko.

Hata Mungu alisema, wanadamu kama mkikaa kimya mawe yatapaza sauti. Hata tusiposema kuhusu JPM basi jua, madaraja, mabarabara, vituo vya afya na zahanati, masoko, stendi, sigiara na sitesheni zake iapoti etc. Vyote hiivi vitakuwa kielezo cha utendaji, uongozi na usimamizi uliotukuka wa JPM.

Na hapo ndipo watu hesabu ziliwapiga chenga kwa kushindwa kuzingatia yatokanayo.
 
Legacy ya Magufuli bado itaendelea kuishi.

Hakuna atakaefuta legacy yake leo wala kesho.

Kikundi cha wahuni wachache kinapambana kila siku mitandaoni kupambana na legacy ya Magufuli.

Magufuli ataendelea kuishi kwenye mioyo wa watanzania wengi kwa mema na kwa mabaya lakini ataendelea kuishi kwenye mioyo yao.

Tusilazimishane, kila mtu amkumbuke Magufuli anavyotaka. Kama wewe utakumbuka kwa mabaya basi iwe juu yako na usilazimishe watu ama usitumie nguvu kubwa kulazimisha watu wamkumbuke unavyotaka.
Ni kweli ,mfano hai ni jinsi Tundu Lissu anavyotembea kwa kuvuta mguu wake uliojaa vyuma.
 
Back
Top Bottom