Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Ahsante sana mkuu, basi alikua na mchango muhimu sana maana inainaekana aliipokea nchi ikiws hali mbaya sana
 
Ahsante sana mkuu, basi alikua na mchango muhimu sana maana inainaekana aliipokea nchi ikiws hali mbaya sana

Hali ilikuwa mbaya kupita maelezo
nchi nzima watu wanavaa katambuga
sabuni za magadi na majani ya mpapai..
mahindi ya msaada kutoka marekani ya njano
yaliitwa mahindi ya Yanga....
ukikutwa na sigara box zima unakamatwa kwa uhujumu uchumi
 
Alikuwa anamsikiliza Nyerere weeeeee, hambishii, akitoka hapo anafanya anavyoona yeye inafaa!

Enzi zake vijana wakaanza kwenda Dubai kuleta mali

Aliamua makusudi kutokusanya kodi kutoka kwa Makabwela ili kuwajengea watu uwezo wa kifedha, ili baadae wapatikane watu wa kuwatoza kodi..

Alilichinjilia mbali Azimio la Kimasikini lile Azimio la Arusha, Wewe umewahi kuona wapi Azimio linazuia watu kumiliki hata nyumba ya kupangisha eti kisa wewe ni Mwenyekiti wa kijiji.

Wakati anaondoka madarakani almost kila mtu akawa ana TV, watu tumeangalia World Cup mwaka 1994 ITV, tumeangalia Kombe la Mataifa huru ya Afrika yaliyofanyika Tunisia mwaka 1994 Live kila mtu na kideo chake nyumbani!

Pesa ilikuwa inapatikana, Vijana wakaanza kuangusha majumba ya hatari Mbezi, Tabata, Sinza

Aliandikwa vibaya sana na Magazeti kama RAI ya Jenerali Ulimwengu lakini hukusikia anayafungia!

Long live mzee Ruksa, Uko mioyoni mwetu forever!
 
Mkuu kinacho nishangaza ni kuwa mfumo wa vyama vingi sifa nyingi anapewa Nyerere wakati aliyekuwepo madarakani ni Mwinyi sijajua kwa nini anasifiwa Nyerere
 
Uzushi tu
hata Kikwete walizusha kaoa pia
inatokea tu pale mnapokuwa na uhuru wa kujieleza bila hofu
Inasemekana siti aliolewa baada ya kwanza kutopenda kuonekana hadharani ndio maana
tena kuna stori nyingi zaidi wakati anaoa na hali ilivyokua ambazo wacha niziite za vijiweni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…