Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Kuelewa mchango wa Mwinyi unapaswa kwanza kuelewa hali ya nchi ilivyokuwa wakati anakuwa Rais...

Nchi ilikuwa na Redio moja tu Redio Tanzania..na magazeti ya chama na serikali...

hakuna kabisa sehemu ya kukosoa wala kueleza matatizo...

na baada ya vita ya Iddi Amin kiuchumi nchi ndo ikayumba kabisa

Sera za Nyerere za ujamaa na kila kitu kufanywa na serikali kuanzia kuuza mikate
hadi nguo n kadhalika ilisha feli....

watu wanapanga foleni kununua sukari na sigara

mtu akienda Kenya mnamuagiza colgate na sabuni za lux...

hali ilikuwa mbaya except kwa wachache waliokuwa na nafasi...

Mwinyi akaapishwa mwaka 1985....by the time anaondoka 1995..

Ilikuwa nchi tofauti kabisa.......magazeti tele..TV na redio...tele
vyama vya upinzani.....hadi uchaguzi wa 1995 kulikuwa na mdahalo kwenye tv

hapo ndo Lipumba akaibukia CUF....

Vitongoji kama Sinza vikawa maarufu wakati wa Nyerere ni kulikuwa na mashamba tu ya mpunga..
magari ikawa ruksa unanunua bila kuomba kibali..

Sasa wapo wanaosema hakufanya lolote...
labda mabadiliko yangekuja tu bila yeye...

but wengi wanaosema hivyo hawakuwepo enzi hizo
Ahsante sana mkuu, basi alikua na mchango muhimu sana maana inainaekana aliipokea nchi ikiws hali mbaya sana
 
Ahsante sana mkuu, basi alikua na mchango muhimu sana maana inainaekana aliipokea nchi ikiws hali mbaya sana

Hali ilikuwa mbaya kupita maelezo
nchi nzima watu wanavaa katambuga
sabuni za magadi na majani ya mpapai..
mahindi ya msaada kutoka marekani ya njano
yaliitwa mahindi ya Yanga....
ukikutwa na sigara box zima unakamatwa kwa uhujumu uchumi
 
Alikuwa anamsikiliza Nyerere weeeeee, hambishii, akitoka hapo anafanya anavyoona yeye inafaa!

Enzi zake vijana wakaanza kwenda Dubai kuleta mali

Aliamua makusudi kutokusanya kodi kutoka kwa Makabwela ili kuwajengea watu uwezo wa kifedha, ili baadae wapatikane watu wa kuwatoza kodi..

Alilichinjilia mbali Azimio la Kimasikini lile Azimio la Arusha, Wewe umewahi kuona wapi Azimio linazuia watu kumiliki hata nyumba ya kupangisha eti kisa wewe ni Mwenyekiti wa kijiji.

Wakati anaondoka madarakani almost kila mtu akawa ana TV, watu tumeangalia World Cup mwaka 1994 ITV, tumeangalia Kombe la Mataifa huru ya Afrika yaliyofanyika Tunisia mwaka 1994 Live kila mtu na kideo chake nyumbani!

Pesa ilikuwa inapatikana, Vijana wakaanza kuangusha majumba ya hatari Mbezi, Tabata, Sinza

Aliandikwa vibaya sana na Magazeti kama RAI ya Jenerali Ulimwengu lakini hukusikia anayafungia!

Long live mzee Ruksa, Uko mioyoni mwetu forever!
 
1.Aliitoa nchi toka mfumo wa kimashariki -ujamaa (socialim) kwenda mfumo wa kimagharibi-ubepari (capitalism) tuliokuwa nao hivi sasa chini ya sera maarufu ya RUKSA
2.Ndie muanzilishi wa mfumo wa vyama vingi uliopo hivi sasa baada ya mara ya kwanza kuondolewa miaka ya 1976-70
3.Hakua mbaguzi wa dini aliamini kila Mtanzania ana haki regardless ya jinsi na jinsia aliyenayo
Mkuu kinacho nishangaza ni kuwa mfumo wa vyama vingi sifa nyingi anapewa Nyerere wakati aliyekuwepo madarakani ni Mwinyi sijajua kwa nini anasifiwa Nyerere
 
Uzushi tu
hata Kikwete walizusha kaoa pia
inatokea tu pale mnapokuwa na uhuru wa kujieleza bila hofu
Inasemekana siti aliolewa baada ya kwanza kutopenda kuonekana hadharani ndio maana
tena kuna stori nyingi zaidi wakati anaoa na hali ilivyokua ambazo wacha niziite za vijiweni
 
Back
Top Bottom