Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Inasemekana siti aliolewa baada ya kwanza kutopenda kuonekana hadharani ndio maana
tena kuna stori nyingi zaidi wakati anaoa na hali ilivyokua ambazo wacha niziite za vijiweni


Sio kweli
Sitti na Khadijah wote aliwaoa zamani sana
wakati anajiuzulu uwaziri wa mambo ya ndani...alikuwa na wake wawili
akawa ameyumba kiuchumi kiaina
Rafiki yake Kitwana Kondo akamsaidia sana....ndo chanzo cha Kitwana Kondo
kuja kuwa untouchable kiaina wakati wa Mwinyi
 
Hakuwahi kutamani watanzania waishi kama mashetani bali malaika. Hakuongozwa na jazba, visasi, mihemuko wala kupenda sifa za kijinga. Hakuigeuza dini yake kuwa sasa ni zamu yetu. Kwangu mimi ndio rais muungwana kabisa kuongoza nchi hii. Pia ndio rais aliyetutoa matongotongo ya dunia hii, kabla yake kuwa na video ndani ilikuwa ni kama uko na malaika ndani. Kwa wengi wa huku bara ndio tulianza kuziona tv wakati wa utawala wake. Hayo kwa upande wangu ndio mazuri yake niliyoona, na kwakuwa uzi wako haujahitaji mapungufu yake basi tusubiri uzi wa hivyo ukija hapa jukwaani.
 
Ngoja Tuanze na mazuri yako, maana hata wewe ukifa ndugu zako na watu mbali mbali watakumwagia sifa kedekede. Ngoja Tuanze na wewe then tuje kwa mimi pamoja na Mwinyi. Maana unaweza ukafa wewe au Mimi kabla ya Mwinyi..... Tuanze na wewe Mkuu.
 
swali la kizushi
pia unaweza usilijibu
kwanini ukimgusa Mwinyi na SAS lazima uje uwakingie vifua humu jamvini una uhusiano nao ??
 
Halafu kuna njemba ilimkataga mabanzi mubashara hadharani yaani watu wana laana dunia hii.

Na upole ule wa Mzee mwinyi unatoa wapi ujasiri wa kumuadhibu na sucker slap...alinifurahisha alipomsamehe. That's was tottaly humane and humble.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]najaribu kuwaza ndo angekua faru john.......pasingekalika angeteketeza ukoo mzima[emoji188][emoji188]
 
swali la kizushi
kwanini ukimgusa Mwinyi na SAS lazima uje uwakingie vifua humu jamvini una uhusiano nao ??

Sababu najua kuna unfairness ya uandishi wa historia
Nyerere anatukuzwa....Kawawa anapondwa..akati utawala ni huo huo
Hata sasa pay attention siku moja Magufuli ataitwa 'mtakatifu'

Historia ya nchi hii inajulikana kwa hitilafu zake....
 


well said,,,,,,, katika maRais walioisaidia hii nchi kiukweli kabisa huwezi kumuacha MZEE RUKSA..
 
mbona wapo wengi ujahoji jombi !kama mwalimu, karume ,mkapa ,kikwete ,muheshimiwa magu ! au nao sio watu jombi ?
 
Napenda ucha Mungu wake, kiukweli alikuwa Rais bora kipindi chake,,,,,kikubwa zaidi na wanae nahisi amewalea katika mfumo wa dini ya kiislam,,,Hawana makeke wala mbwembwe,,,, Mungu ampe umri mrefu mzee wetu na Nguvu tele
 
Sababu najua kuna unfairness ya uandishi wa historia
Nyerere anatukuzwa....Kawawa anapondwa..akati utawala ni huo huo
Hata sasa pay attention siku moja Magufuli ataitwa 'mtakatifu'

Historia ya nchi hii inajulikana kwa hitilafu zake....

Nashukuru leo brother unamwaga Nondo zakutosha... tujiulize kwanini KAWAWA anapondwa na kwa nini MWINYI ANAPONDWA NAKIKWETE AMEPONDWA LAKINI WENGINE WANATUKUZWA KWA KUONEKANA NI WAZURI KIUTENDA..
 
Mkuu kinacho nishangaza ni kuwa mfumo wa vyama vingi sifa nyingi anapewa Nyerere wakati aliyekuwepo madarakani ni Mwinyi sijajua kwa nini anasifiwa Nyerere

Kwenye hilo Nyerere ni kweli ndie alieanzisha
Nyerere alipoacha Urais alibaki mwenyekiti kwa miaka miwili hadi 1987
mwenyekiti wa CCM....moja ya sababu ni kuwa Mwinyi hakuwa chaguo lake
alimtaka Salim akashindwa..so hakumuamini Mwinyi....akabaki kama anamchunga hivi..

Ndo aliposema kwa mara ya kwanza 'sio dhambi kuzungumza kuhusu vyama vingi'
hapo mwaka 1987...Mwinyi akaja kukubali hilo wimbi....
kabla ya hapo ukisema una chama cha siasa kingine except CCM unafungwa
uliza kina Chipaka na Mapalala....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]najaribu kuwaza ndo angekua faru john.......pasingekalika angeteketeza ukoo mzima[emoji188][emoji188]
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji16] [emoji115]
 
swali la kizushi
pia unaweza usilijibu
kwanini ukimgusa Mwinyi na SAS lazima uje uwakingie vifua humu jamvini una uhusiano nao ??

Mkuu kwani hayo ayasemayo THE BOSS kuhusu MZEE RUKSA ni ya uongo??

RUKSA ALIITOA HII NCHI KWENYE TONGOTONGO NA GIZA KALI..
 
Alibadilisha maisha yangu kuwa mazuri hadi leo. Kwa kuruhusu ajira huria / ruksa nilipata kibali toka wizarani kufanya kazi DANIDA. Halikuwa jambo jepesi miaka hiyo. Huko niililipwa dolar 11,000 mkupuo na maisha yangu kipesa kuwa safi mpaka leo. Mungu aziidishie maisha azine kuona vitukuu, vilembwe nk.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…