Hekima ni nini??
Alipojiuzulu UWAZIRI WA MAMBO YA NDANI ya Nchi mwaka 77 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa Mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa Mzee Natepe kushika Uwaziri wa Mambo ya ndani ya Nchi
Natepe alipoingia tu ofisini, alimtaka waziri aliemtangulia (ALI H. MWINYI) kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama Waziri.
Ilikuwa shida kidogo maana ALI MWINYI bado alikuwa anatafuta Makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.
Ikampasa Mzee Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serekali.
Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee MWINYI akaviacha akaondoka.
Baada ya miezi kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais Zanzibar. Natepe wakati anajipanga kumuomba radhi kwa aliyomfanyia.... kabla ya kufikiria njia atakayoitumia....Mzee Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.
Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea akawa anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza mzee mwinyi.
Mzee mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Natepe kuwa waziri pale pale Mambo ya ndani.
Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya, endelea kufanya kazi.
Siku moja Mzee MWINYI yupo Ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??
Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe... Mzee Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.
Hapa kuna masomo makubwa ma tatu vema viongozi wetu wa sasa wakajipambanua kwayo ili tuende kwa weledi na umakini sana. Hata kwetu sisi wanadamu ni somo zuri sana la kujifunza.
Acknowledgement:
PATRICK MUJUNGU