Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Mwinyi ndio mwanasiasa mkongwe kwa sasa kuliko wote walio hai. Hataki kuunganishwa na siasa za kihuni wanazofanya wastaafu, siasa za dharau na fitina.
 
Si role model kabisa. Hata maongezi yake Jana yalilenga kulinda kibarua Cha mwanae tu
 
Ni upuuzi kupost barua ya kughushi, haina saini wala nembo ya Taifa na wakati mtu yeyote anapoandika barua ya kujiuzulu huwa bado ni mwenye cheo husika hadi pale anapojibiwa au anapoteuliwa mwingine badala yake. Sasa wewe unatupostia upumbavu
 
Hekima ni nini??

Alipojiuzulu UWAZIRI WA MAMBO YA NDANI ya Nchi mwaka 77 kama sijakosea nafasi yake aliteuliwa Mzee mmoja kutoka Zanzibar anaitwa Mzee Natepe kushika Uwaziri wa Mambo ya ndani ya Nchi

Natepe alipoingia tu ofisini, alimtaka waziri aliemtangulia (ALI H. MWINYI) kutoka katika nyumba ya waziri ili yeye aweze kukaa hapo kama Waziri.

Ilikuwa shida kidogo maana ALI MWINYI bado alikuwa anatafuta Makazi lakini alitakiwa haraka kutoka na Natepe.

Ikampasa Mzee Mwinyi kutoka kwa haraka na siku anatoka pale nyumbani alikuwa amenunua mabati 150 na mifuko ya saruji 100 ya kwake wala sio mali ya serekali.

Natepe alimkatalia kuvichukua akidai ni mali ya serekali kweli mzee MWINYI akaviacha akaondoka.

Baada ya miezi kadhaa tu Mzee Mwinyi akateuliwa kuwa Rais Zanzibar. Natepe wakati anajipanga kumuomba radhi kwa aliyomfanyia.... kabla ya kufikiria njia atakayoitumia....Mzee Mwinyi akaletwa bara mwaka 1985 kama Rais wa JMT.

Hapa sasa Natepe akajua kazi hana na atatimuliwa haraka iwezekanavyo tena na kutengwa na nyadhifa za JMT kwakuwa kuna mabaya ya wazi na ya sirini aliyomtendea akawa anajifikiria jinsi ya kwenda kumpongeza mzee mwinyi.

Mzee mwinyi baada tu ya kuapishwa kuwa Rais wa JMT wakati anateua baraza la mawaziri akamteua tena Natepe kuwa waziri pale pale Mambo ya ndani.

Siku ya kumuapisha akamwambia Natepe sio kwamba nakupenda sana hapana ila napenda kazi yako unavyofanya, endelea kufanya kazi.

Siku moja Mzee MWINYI yupo Ikulu kapumzika akaona malori yanaingia na akaambiwa mzigo wako huu mh Rais akashtuka mbona sijaagiza kitu mie??

Ndipo akaambiwa umetoka kwa Natepe... Mzee Mwinyi akacheka sana akawaambia wasaidizi wake shusheni mabati 150 na saruji 100 hizo ndio haki yangu zingine mrudishieni tu.

Hapa kuna masomo makubwa ma tatu vema viongozi wetu wa sasa wakajipambanua kwayo ili tuende kwa weledi na umakini sana. Hata kwetu sisi wanadamu ni somo zuri sana la kujifunza.

Acknowledgement:
PATRICK MUJUNGU
 
ni kisa kizuri,hiki kisa na kile cha nyerere na kwaya ya ;moses nnayue zinatakiwa kuweka katika vitabu vya history
 
Malori yalienda ikulu pasipo taarifa kwa usalama Wa taifa au walinzi Wa ikulu na Rais? Mbona ni ngumu sana mana hapo inaonyesha hata Rais mwenyewe hakuwa na taarifa
 
Inawezekana simulizi ya Malori ina walakini lkn mantic ya Msimulizi alitaka tupate ujumbe namna Mh. Natepe alivohaha kujenga upya taswira yake kwa A. H. M
 
Rais mstaafu mzee Mwinyi ameonyesha uungwana uliotukuka kwa kukiri uchapakazi wa Rais Magufuli hadharani.

Mwinyi amesema kazi waliyoshindwa kuifanya yeye, Mkapa na Kikwete kwa miaka 30 Dr Magufuli ameifanya kwa miaka mitatu tu

Maendeleo hayana vyema!
 
Rais mstaafu mzee Mwinyi ameonyesha uungwana uliotukuka kwa kukiri uchapakazi wa Rais Magufuli hadharani.

Mwinyi amesema kazi waliyoshindwa kuifanya yeye, Mkapa na Kikwete kwa miaka 30 Dr Magufuli ameifanya kwa miaka mitatu tu
Mwinyi amesifia ununuzi wa ndege bila kufuata utaratibu Bunge halijui pesa zilikotoka nk
 
Rais mstaafu mzee Mwinyi ameonyesha uungwana uliotukuka kwa kukiri uchapakazi wa Rais Magufuli hadharani.

Mwinyi amesema kazi waliyoshindwa kuifanya yeye, Mkapa na Kikwete kwa miaka 30 Dr Magufuli ameifanya kwa miaka mitatu tu

Maendeleo hayana vyema!
Amesema ukweli kabisa kwa miaka yote hiyo hakuna aliyejenga kwao kama huyu,hakuna aliyenunua madege mengi bila hata mtu yoyote kujua pesa imetoka wapi, hakuna aliyekandamiza demokrasia kama huyu na mengine mengi ya hovyo
 
Back
Top Bottom