Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Legacy ya Rais Ali Hassan Mwinyi (91 years) ni nini?

Si ajabu Rais Mstaafu Nyerere alimuita Rais Mwinyi "Rais dhaifu". Na si ajabu yule kijana alimchapa kofi mzee huyu.

Kumbe ukimya huficha mambo mengi sana,ikiwamo ujinga alionao mtu.Mwinyi ni mji**ga anayeonekana ana hekima sababu ya ukimya wake na upole wake tu.
 
Mzee inaoneshwa alipangiwa hadi cha kusema si ajabu alipigwa mkwara kwa mwanae,Hivi wale waandishi wa habari sijui aliwaita nani
 
Kweli baba wa tifa alimuachia ndege nyingi na viwanda mzee we pumzika
 
Pole sana mzee wetu, insikitisha ulivyojidhalilisha na kuwadhalilisha Maraisi wastaafu.

Magufuli sidhani angeweza kusuka usukani awamu uliyorithi wewe, serekali iliyofilisika, nchi iliyokuwa haina chakula, dawa, petroli na ajira. Jee huyu Bw. MWAGAMWAGA angeweza
 
Mchango wa waliotangulia ni Mkubwa sana kuliko watu wanavyofikiria, Mheshimia wetu kwa sasa bado sana.
Fikiria kama PCCB isingeanziswa kipindi cha nyuma je angekuwa na ubavu gani kwa sasa kuwa kamatakama baadhi ya vigogo? Je kama barabara za lami zisingejegwa kipindi cha Mwinyi ama Ben na JK je leo kipaumbele chetu kingekuwa kununua madege? Tukumbuke enzi hizo unatoka Segera mpaka Chalinze hakuna lami, Mtwara mpaka Kibiti hakuna lami, ama Mwanza mpaka Dodoma kulikuwa hakuna lami, je hali hiyo ingekuwepo mpaka sasa kipaumbele chetu ingekuwa ni kununua madege? Jibu ni Hapana.
Swala lingine ni kwamba nguvu kazi ya kipindi kile ilikuwa ndi ndogo sana na uzalishaji ulikuwa mdogo na hivyo baadhi ya vitu vilikuwa vinafanyika taratibu sana, kwa sasa nguvu kazi ni kubwa na hivyo uzalishaji mali unatakiwa kuwa mkubwa sana na hivyo maendeleo yanatakiwa yale kwa kasi kubwa.
Kwa nafasi yake anasimama hapo kwa sababu kuna waliotangulia na kuweka mambo sawa. Na yeye ataacha msingi bora na imara kwa atakayeingia aweze endelea pale alipoishia, ila kwa sasa still long way to go.
La mwisho, watu wengi hawajuhi mtu tunapomchagua anatakiwa akafanye kazi na alete maendeleo pia, inashangaza sana kusoma maoni ya watu hapa yakionyenya kuwa hawajuhi wawakilishi wao waliowachagua majukumu yao ni nini.
 
Mwambieni mzee mwinyi

There is no market for your emotions,so never advertise your feelings just display your attitude!

Wanzuki oyeèeè
 
Rais mstaafu yupo sahihi, kwa upande wa yaliyofanyika, huhitaji tochi kujua Rais john amefanya nini,

Rais mstaafu (kama kwel amesema) amechukulia mazingira halisi, ingelitokea tu kila rais aliepita ukimwacha mwinyi ambae alikuta nchi kwenye wakati mgumu, wakafanya walao moja(mfano wakanunua ndege au kujenga reli na miundo mbinu leo hii rais john angalikuwa anashughulika na umeme tu...

Kwa hyo mstaafu yupo sahihi kwa upande huo, japo inapaswa kujulikana kuwa kila zama na kitabu chake...
 
Ameongea ukweli mtupu. Hivi karibuni reli zote zilizokuwa zimekufa zitakuwa zinafanya kazi zote.
 
ALHAJ Ali Hassan Mwinyi, ametokeza na kumlaumu January Makamba, kutumia picha yao ya zamani wakicheka pamoja kwenye 'twiti' ya kuridhia kutenguliwa Uwaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Mwinyi amehoji, kwa nini picha hiyo itumike kipindi mambo yamekoregeka? Ukimwelewa Mwinyi, ni kama anashawishika kuamini kwamba picha imetumika vibaya na inatoa tafsiri kwamba yeye na January wanachekelea uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa January Baraza la Mawaziri.

Maneno ya 'twiti' ya January akisema, amepokea mabadiliko yaliyofanyika kwa moyo mweupe kabisa, akiambatanisha 'emoji' ya cheko la upendo, kisha picha kuwaonesha January na Mzee Mwinyi wakichekelea, hapo ndipo mwanzo wa nongwa.

Ni hofu tu! Inawezekana Mzee Mwinyi alielewa vibaya au kuna watu walimshawishi kuelewa tofauti. Hofu ingeondoka, picha hiyo ina thamani kubwa kwa Mwinyi. Na Mwinyi angeona raha namna anavyokuwa hamasa kwa vijana viongozi wa kizazi cha sasa.

Ipo hivi; mwaka 1974, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Shinyanga, Michael Mabawa, alitumia askari wa Jeshi la Polisi, kufanya oparesheni ya kusaka wachawi, wananchi wasio na hatia walipigwa na kudhalilishwa mno kwa tuhuma za kujihusisha na ushirikina.
Kwa kitendo hicho, Mwinyi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, bila kupoteza muda, alimwandikia barua ya kujiuzulu, Mwalimu Nyerere, kwa sababu polisi ambao walikuwa chini ya wizara aliyoiongoza, walipiga na kutesa raia.

Mwaka 1984, miaka 10 baada ya tukio hilo, kikao cha Halmashauri Kuu CCM kilimvua Urais wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe kisha Mwinyi akapitishwa kuwa Rais wa visiwa hivyo. Mwaka 1985, Mwinyi akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akamrithi Mwalimu Nyerere.

Hivyo, Mwinyi ni alama yenye kutoa hamasa kwa viongozi hasa vijana, kutambua kuwa zipo nyakati za kuteleza na kuanguka, lakini muhimu ni kujikusanya, kunyanyuka na kuendelea na mwendo. January katika picha yake na Mwinyi, bila shaka alikusudia tafsiri kuwa aliyopata ni ajali kama ya Mwinyi, hivyo atanyanyuka kama alivyonyanyuka Mwinyi. Hapo kuna ubaya gani?

Muhimu ni kwamba January ana ndoto za kuwa Rais. Mwinyi alikuwa Rais baada ya ajali ya kujiuzulu. Ni kosa January kujipa moyo kuwa ipo siku atakuwa Rais baada ya ajali ya kutenguliwa? Tatizo siku hizi hofu inafubaza uwezo wa kufikiri. Uoga umetamalaki!

Ndimi Luqman MALOTO
 
CC ya Ccm ya January 6, 1984 haikumvua Urais Alhaj Almarhum Sheikh Aboud Jumbe bali alivuliwa Uanachama wa Ccm na automatically akapoteza sifa ya kuwa Rais wa Znz

2010 Hayati Mzee Sitta alikumbushwa kuwa punguza ujuaji tunaweza kuchukua kadi ya Chama over night ukajikuta umepoteza hadhi ya kuishi kama Senior citizen , aliufyata mpaka mwsho wa Maisha yake
 
ALHAJ Ali Hassan Mwinyi, ametokeza na kumlaumu January Makamba, kutumia picha yao ya zamani wakicheka pamoja kwenye 'twiti' ya kuridhia kutenguliwa Uwaziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.

Mwinyi amehoji, kwa nini picha hiyo itumike kipindi mambo yamekoregeka? Ukimwelewa Mwinyi, ni kama anashawishika kuamini kwamba picha imetumika vibaya na inatoa tafsiri kwamba yeye na January wanachekelea uamuzi wa Rais Magufuli kutengua uteuzi wa January Baraza la Mawaziri.

Maneno ya 'twiti' ya January akisema, amepokea mabadiliko yaliyofanyika kwa moyo mweupe kabisa, akiambatanisha 'emoji' ya cheko la upendo, kisha picha kuwaonesha January na Mzee Mwinyi wakichekelea, hapo ndipo mwanzo wa nongwa.

Ni hofu tu! Inawezekana Mzee Mwinyi alielewa vibaya au kuna watu walimshawishi kuelewa tofauti. Hofu ingeondoka, picha hiyo ina thamani kubwa kwa Mwinyi. Na Mwinyi angeona raha namna anavyokuwa hamasa kwa vijana viongozi wa kizazi cha sasa.

Ipo hivi; mwaka 1974, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Shinyanga, Michael Mabawa, alitumia askari wa Jeshi la Polisi, kufanya oparesheni ya kusaka wachawi, wananchi wasio na hatia walipigwa na kudhalilishwa mno kwa tuhuma za kujihusisha na ushirikina.
Kwa kitendo hicho, Mwinyi akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, bila kupoteza muda, alimwandikia barua ya kujiuzulu, Mwalimu Nyerere, kwa sababu polisi ambao walikuwa chini ya wizara aliyoiongoza, walipiga na kutesa raia.

Mwaka 1984, miaka 10 baada ya tukio hilo, kikao cha Halmashauri Kuu CCM kilimvua Urais wa Zanzibar, Alhaj Aboud Jumbe kisha Mwinyi akapitishwa kuwa Rais wa visiwa hivyo. Mwaka 1985, Mwinyi akawa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akamrithi Mwalimu Nyerere.

Hivyo, Mwinyi ni alama yenye kutoa hamasa kwa viongozi hasa vijana, kutambua kuwa zipo nyakati za kuteleza na kuanguka, lakini muhimu ni kujikusanya, kunyanyuka na kuendelea na mwendo. January katika picha yake na Mwinyi, bila shaka alikusudia tafsiri kuwa aliyopata ni ajali kama ya Mwinyi, hivyo atanyanyuka kama alivyonyanyuka Mwinyi. Hapo kuna ubaya gani?

Muhimu ni kwamba January ana ndoto za kuwa Rais. Mwinyi alikuwa Rais baada ya ajali ya kujiuzulu. Ni kosa January kujipa moyo kuwa ipo siku atakuwa Rais baada ya ajali ya kutenguliwa? Tatizo siku hizi hofu inafubaza uwezo wa kufikiri. Uoga umetamalaki!

Ndimi Luqman MALOTO
Unadhani Nyerere " alimaanisha" au Mwinyi alipata bahati ya mtende baada ya Salim kusita sita!
 
Makamba amekosea kwa sababu zifuatazo

1, Mzee Mwinyi ni mwenyekiti wa baraza la wazee, kitendo cha kutumia picha yake katika maji haya yaliyokorogeka ni kujaribu kutuma meseji kuwa mzee yuko upande wa akina January na dingi yake

2. Kutumia picha ya raisi mstaafu baada ya maamuzi ya raisi aliyeko madarakani ni kujaribu kumteta au kumsimanga raisi wa sasa dhidi ya yule wa zamani hasa ukizingatia mzee Mwinyi ni senior kwa huyu wa sasa

3. Mzee Mwinyi ni mzazi wa mtoto ambaye ni waziri wa wizara nyeti ya Ulinzi, kitendo chochote cha kujaribu kumhusisha mzee ambaye ni mzazi wa waziri mwenye dhamana ya Majeshi katika kipindi chenye kusemwasemwa kuwa kuna watu wanafanya njama za kumng'oa rais wa sasa madarakani kunatuma meseji mbaya kwa raisi wa sasa!. Kumbuka vetting ya nafasi nyeti kama hii ya ulinzi huhusisha kujua hata wazazi wako wana mitizamo gani.

January alifanya kosa la ufundi kutumia picha ya mzee mwinyi katika kipindi hiki.
 
Unadhani Nyerere " alimaanisha" au Mwinyi alipata bahati ya mtende baada ya Salim kusita sita!
Ni nan alikwambia kuwa SAS alisitasita? Unajua figisu na makundi yaliotamalak ndan ya kikao cha CCM? Unaujua uhasama wa kimakundi kutoka. Zanzibar ulivyokuja na hoja zao hata Mwalimu hakashindwa kushinikiza jina la SAS?

Rudi kasome historia ya Chama unachojinasibisha nacho!!!
 
Sababu ya kumuweka Mzee wa watu kwenye ugomvi wako ni nini, kama sio uchuro?
 
Mzee bila shaka anatetea ugali wa mwanae, japo anafahamu vema picha haikuwa na nia mbaya
 
Sababu ya kumuweka Mzee wa watu kwenye ugomvi wako ni nini, kama sio uchuro?
Mbona hatuchukui hii kitu in a positive way? Mwinyi si alijiuzulu? 1976 then tatizo Ni Nini? Acheni uswahili..achaneni na fb na insta, twitter Ni nyoko!
 
Back
Top Bottom