Leicester City, Special Thread

Leicester City, Special Thread

The Foxes.....dah!!mimi si mshabiki wa timu hii ila hawa watu watamaliza ndani ya TOP 4 msimu huu.
 
Team yoyoye ikiweza kusoma fomeshein wa timu nyengine ni rahisi kuifunga pia yule kocha musisahau mfumo anaotumia ni mfumo wa kwao.mfumo wa itali ni anza nyuma usikae na mpira sana.piga mbele tafuta goli sasa kuiangalia hilo utaliona ndio linalofanywa na LC.
 
musijemukaiteleleza thread yenu, toka lini sikio kuzidi kichwa? nakuhakikishieni huyu hata top 4 haingii
 
mchepuko raha sana,ukidibuliwa njia kuu unaenda kucheki mchepuko mara OMG! FT Leicester 3:2 Everton, ukichek table mchepuko unakimbiza speed 120 tena kwenye kona
 
Mambo kama haya yalitokea 95 Blackburn rovers wakatwaa ndoo.Sasa tuweke akiba ya maneno kama watakaza hivi au watapwaya game zinazokuja.
 
Mbona hukunipa mwaliko niwe nakuja kukutembelea kwenye jamvi lako?
Kwa sababu hukulianzisha kama ulivyoahidi, au una ids nyingi na hiyo iliyoanzisha ni yako?

Bado una nafasi ya kuyafungua matatu, Crystal Palace, West Ham na Newcastle.

Kama ni wewe ulilifungua bado unasubiri nikuite?
Haya ukuje basi, kaliibuu!

Siipi nafasi kubwa Leicester kutwaa ubingwa, imeanza kwa kasi lakini itakutana na vizingiti kuanzia Januari. Sababu ya kuiona timu hii ni kuwa imekuwa inaadhibu Timu kubwa, yenyewe haijafikia ukomavu wa kuitwa Timu kubwa.

Leicester inacheza kitimu, kila mmoja anajituma na imebahatika kuwa na Vady na Mahrez ambao wakiona nyavu tu, mpira unaokotwa huko. Tayari Vady alionekana akitoka nje akiwa ameshikilia Hamstring, si dalili nzuri. Na pia tayari timu matai zinamnyemelea kumtwaa. Timu inaweza kuwa top 4 lakini ubingwa haina mpira huo kwa sasa.
 
Bado nina imani na Leicester City hilo liko wazi...
 
Bado nina imani na Leicester City hilo liko wazi...
Ali Mwinyi: kuwa na imani na Leicester ni Ruksaaa!
C.T.U siwezi kukuomba au kukuzuia usiwe na imani na Leicester.
Leicester pia inaweza kuibuka kidedea kama wataendelea na mori kama hii waliyoanza nayo. Hata hivyo , haiondoi ukweli kuwa Lecester ni underdog na ikiweza kutwaa ubingwa itawashangaza wengi, mimi nitakuwa mmoja wapo.

Uchezaji na mtindo wa uchezaji wa Leicester naufananisha na wa Crystal Palace na mimi ni mpenzi wa aina hii ya uchezaji kandanda.
 
leo tunakutana na LIVERPOOL....
mnakaribishwa kutoa LIVE UPDATES ZENU HAPA...
 
Etlast wamepunguzwa nguvu hawa jamaa walikuwa hataree sana aisee
 
Back
Top Bottom