SI KWELI PreGE2025 Lema amesema Maria Sarungi ni msaliti anaitafuna CHADEMA ndani kwa ndani

SI KWELI PreGE2025 Lema amesema Maria Sarungi ni msaliti anaitafuna CHADEMA ndani kwa ndani

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
LEMA28JUN2025.jpg
 
Tunachokijua

Godbless Lema awali aliteuliwa kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA kabla ya uteuzi wake kutenguliwa na Msajili wa vyama vya siasa, na kisha baadaye kuteuliwa tena kwa ajili ya kukaimu nafasi hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Lema amekuwa ni moja kati ya viongozi wa chama hicho ambao wamekuwa wakitumia mitandao ya kijamii kufanya uchechemuzi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu demokrasia pamoja na kukosoa utendaji wa serikali, hasa kupitia ukurasa wake wa X.

Aidha Maria Sarungi ni mwanaharakati kutokea Tanzania, ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kupigania haki za binadamu, utawala wa kisheria unaozingatia misingi ya kidemokrasia ambapo pia amekuwa akitumia mitandao ya Kijamii hasa mtandao wa X, ambapo ameonekana kuunga mkono ajenda ya CHADEMA, 'No reforms, No Election' ikishinikiza kufanyika kwa mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi ili kuchochea uhuru, haki na uwazi wakati wa uchaguzi.


Ipo Grafiki iliyotumia utambulisho wa Jambo TV na kunukuu andiko linaloonekana kuchapishwa na Lema kwenye ukurasa wake wa mtandao wa X kwamba Maria Sarungi ni msaliti anaitafuna CHADEMA ndani kwa ndani.

Je, ni upi uhalisia wa Grafiki hiyo?


Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa andiko lililonukuliwa si la kweli ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halikuchapishwa na Lema kwenye ukurasa wake.

Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo, si ya kweli bali ni ya kughushi, kwani haijachapishwa na JAMBO TV.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa X, Godbless Lema amelikanusha andiko hilo lililonukuliwa, akionekana kulishangaa na kwamba halikuchapishwa na yeye.​
Back
Top Bottom