Pre GE2025 Lema: CCM hamtatuzuia kwenye kusudi ambalo lipo mbele yetu (Tone tone)

Pre GE2025 Lema: CCM hamtatuzuia kwenye kusudi ambalo lipo mbele yetu (Tone tone)

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
CHADEMA muda huu wanzungumzia kampeni ya Tone tone namna inavyoendelea hadi sasa

Updates...

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Godbless Lema na Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya fedha ya chama hicho amesema endapo wanachama na wadau wakikichangia chama hicho kwa wingi kwa kiasi walichonacho kwani fedha hizo zitakisaidia chama hicho kufanya kazi zake na kuwafikia wananchi wengi.

Akizungumza leo machi 14 kwenye tukio la 'Tone Tone Night'
Lema amesema fedha hizo zitakisaidia chama kuacha hata kutegemea ruzuku ambayo wanapewa na serikali kila mwezi.

Soma Pia: CHADEMA wazindua mkakati maalum wa kidigitali wa tone tone, Februari 27, 2025
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025


Lema ametoa wito kwa wanachama wa vyama vingine ikiwemo chama cha Mapinduzi CCM kukichangia CHADEMA kwani uimara wa CCM unategemea uimara wa CHADEMA

“CCM hamtatuzuia kwenye kusudi ambalo lipo mbele yetu, tumekusudia kuwatoa madarakani tutatafuta hela mbinguni tutatafuta hela duniani hamna maarifa kuliko sisi kwa hiyo hela za nje tutachukulia huko huko nje”​


 
Nendeni kwenye redio za mikoani ambazo zinasikilizwa na wananchi wengi tangazeni namba zenu mtashangaa mwitikio mtakaopata.
Hivi kwani humu hakuna viongozi wa Chadema ambao ni verified, muwe mnawakopi mawazo mazuri kama haya???? Wanakomaa na Dar tu Dar wakati watu wa mikoani wako vibrant sana na mabadiliko.
Tumieni Radio za mikoani, magrouo ya wasap ya mikoani kuhamasisha mchangiwe...
 
Back
Top Bottom