Lema: Kufanya vikao vya kimkakati sio usaliti. Watu wamesaidiwa kwa njia hiyo

tucker carlson

Senior Member
Joined
Oct 5, 2025
Posts
182
Reaction score
759
Wakuu,

Mwanasiasa Godbless Lema ameeleza hofu ya viongozi kufanya mikakati ya mashauriano ya chinichini (strategic engagement) kwa kuogopa kuitwa wasaliti au kuonekana wamepewa pesa na serikali, hali inayoweza kusababisha wanachama kuendelea kuozea magerezani kwa mambo ambayo yangeishia ofisini.

"Imefika mahali hata kutaka kufanya strategic engagement ya namna ya kusaidia watu unaogopa, kwa sababu ukiifanya unaambiwa umepewa hela! Kwa hiyo maanake kuna watu wataozea jela mambo ambayo pengine yangeisha kwa kikao ofisini cha Lema na OCCID. Vikao vya kimkakati ama kupiga simu kwa maaskofu ama kupiga simu mbalimbali tumekuwa tukifanya, sio usaliti. Ni mikakati ya kisiasa ambayo haiko hadharani, na watu wengi wamesaidiwa kwa njia hiyo."

Lema is very right
Kazi ya kiongozi ni kutatua changamoto na kutafuta majawabu sio kuleta changamoto au ugumu.

Na sio kila mbinu iwekwe hadharani la Sivyo nchi hii isingepata uhuru
 
Kwenye hivyo vikao vya kimkakati ndio Abdul na jopo lake wanaenda na mabegi ya pesa kama hongo.

Huyu jamaa ni mjinga sana.
umewahi kusikia msemo unasema ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya?

Kwa ufahamu mambo yote yenye mafanikio hadharani yameanzia gizani. Lazima mipango iwekwe kabla ya hatua kuchukuliwa copy hiyo itakusaidia
 
CCM mnapenda sana mambo ya gizani ambayo ni konyume cha katiba na sheria ila yana manufaa kwenu.

Mambo hayatakiwi kuanzia gizani na kuishia hadharani.

Kwanini mnapenda sana mambo ya nyuma ya pazia?

Kwanza Lissu ameshakataa mambo ya nyuma ya pazia anataka kama ni mkosaji basi sheria ifuate mkondo wake.

Sio mmwambie tutakuachia lakini usifanye siasa za kweli za upinzani kinyume chake hama nchi au fanya siasa oya oya kama za kina Zito kabwe na Mbowe.

Mambo yanatakiwa yaanzie kwenye katiba na sheria na kuishia kwenye katiba na sheria.

Chochote nje na hapo ni ujanja ujanja ambao mara zote mnufaika ni CCM.
 
Aliye Jela amekataa madalali amesema iachwe mahakama wewe unapata wapi huo ujasiri wa kukaa vikao vya udalali na mhusika mkuu alikataa dhahiri shahiri?
Na mimi Nashangaa.

Kwanini mambo yaanzie gizani?

Mambo yaanzie na sheria na katiba na kuishia na sheria na katiba.

Nje ya hapo ni ujanja ujanja ambao mnufaika mkubwa ni CCM na muumiaji ni mwananchi wa kawaida.
 
Wakuu,

Mwanasiasa Godbless Lema ameeleza hofu ya viongozi kufanya mikakati ya mashauriano ya chinichini (strategic engagement) kwa kuogopa kuitwa wasaliti au kuonekana wamepewa pesa na serikali, hali inayoweza kusababisha wanachama kuendelea kuozea magerezani kwa mambo ambayo yangeishia ofisini.

"Imefika mahali hata kutaka kufanya strategic engagement ya namna ya kusaidia watu unaogopa, kwa sababu ukiifanya unaambiwa umepewa hela! Kwa hiyo maanake kuna watu wataozea jela mambo ambayo pengine yangeisha kwa kikao ofisini cha Lema na OCCID. Vikao vya kimkakati ama kupiga simu kwa maaskofu ama kupiga simu mbalimbali tumekuwa tukifanya, sio usaliti. Ni mikakati ya kisiasa ambayo haiko hadharani, na watu wengi wamesaidiwa kwa njia hiyo."

Kisha kabisa, huwezi kushindana na ccm miaka 20 ukabaki na msimamo, LISSU NA MAALIM SEIF pekee walioweza
 
Wakuu,

Mwanasiasa Godbless Lema ameeleza hofu ya viongozi kufanya mikakati ya mashauriano ya chinichini (strategic engagement) kwa kuogopa kuitwa wasaliti au kuonekana wamepewa pesa na serikali, hali inayoweza kusababisha wanachama kuendelea kuozea magerezani kwa mambo ambayo yangeishia ofisini.

"Imefika mahali hata kutaka kufanya strategic engagement ya namna ya kusaidia watu unaogopa, kwa sababu ukiifanya unaambiwa umepewa hela! Kwa hiyo maanake kuna watu wataozea jela mambo ambayo pengine yangeisha kwa kikao ofisini cha Lema na OCCID. Vikao vya kimkakati ama kupiga simu kwa maaskofu ama kupiga simu mbalimbali tumekuwa tukifanya, sio usaliti. Ni mikakati ya kisiasa ambayo haiko hadharani, na watu wengi wamesaidiwa kwa njia hiyo."

Watu wenye akili ndogo watabisha sana hii hekima ya lema lakini huu ndo uongozi. Sema watanzania wengi shule ni zero wanabaki kuendeshwa na akina mqnge kimambi tu. Uongozi ni hekima kubwa sana l. Lisu ana akili lakini hekima zero
 
Lema is very right
Kazi ya kiongozi ni kutatua changamoto na kutafuta majawabu sio kuleta changamoto au ugumu.

Na sio kila mbinu iwekwe hadharani la Sivyo nchi hii isingepata uhuru
Kwanini iwe kwa upande Mmoja?. Yani wengine wanaruhusiwa kufanya uharamia ila CHADEMA ndio wanalazimishwa wawapigie magoti. Kuna nini?
 
umewahi kusikia msemo unasema ukitaka kumuua mbwa mpe jina baya?

Kwa ufahamu mambo yote yenye mafanikio hadharani yameanzia gizani. Lazima mipango iwekwe kabla ya hatua kuchukuliwa copy hiyo itakusaidia
Acha upotoshaji
 
Kama walizoea hivyo chini ya Mbowe basi wajue kwa sasa watu hawataki hayo, maana ndio yametufikisha hapa. Hatupati mabadiliko kumbe sababu watu wanakuwa na vikao vya pembeni kujadili kwa faida zao binafsi.
Yaani maana yake kakubali kuwa yeye alikua anaenda gerezani usiku, ili lissu alegeze kamba, kumbe ni kweli kafika bei meku.
Alooo
 
Back
Top Bottom