Kwenye post kama hii ya Lema, hapo majuzi niliwahi kusema Chadema ni kama walikuwa wanapoteza ushawishi, nikiwa na maanisha kuwa na msimamo wa kichama bila kuyumbishwa na wanahakati wa nje ya chama, ila nikapopolewa sana.
Lakini niliangalia jinsi gani viongozi wa Chadema wanaanza kugongana kimsimamo, ikiwamo post ya Lema kupinga/kukataa taarifa rasmi ya Chama kuhusu kauli ya Mwenyekiti iliyoletwa na wakili wake ambae alitukanwa kweli na kuonekana amejituma.
Yote ni baada ya wanaharakati wa nje ya chama kuanza kuikataa.
Narudia tena, ni kweli Chadema kwasasa kina uungwaji mkono mkubwa sana ila ushawishi wake kisera umepungua sana. Kiasi kwamba misimamo mingi ya nje ya chama inaweza kuwa affect ndani kwa ukubwa sana.
Wasipo rekebisha mapema basi kuna mpasuko mkubwa sana unakuja hasa, CCM wakifanya U turn, ambayo inaonekana wazi, kucheza karata ya kuonesha kupinga ccm mtandao, kama kina Polepole na Gwajima. Sasa naona Nchimbi anataka kuhadaa watu kwa namna hiyo.