LGE2024 Lema wa CHADEMA afichua madudu mazito kwenye zoezi la uandikishwaji wa wananchi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Asema Serikali inaiba Uchaguzi

LGE2024 Lema wa CHADEMA afichua madudu mazito kwenye zoezi la uandikishwaji wa wananchi Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Asema Serikali inaiba Uchaguzi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Sijaona ushahidi wa namna Serikali au CCM inavyopanga kuhujumu uchaguzi

Nadhani Lema ameishiwa hoja amebakia na mipasho
 
Hki chama why always Lema si atafute ajira nje ya SIASA? Amekuwa na platforma kubwa sana ndani ya hii SACCOS shauri ya mwenyekiti binamu yake🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
Hapa ndio umeongea ukhanithi gani dogo?!
 
Sijaona ushahidi wa namna Serikali au CCM inavyopanga kuhujumu uchaguzi

Nadhani Lema ameishiwa hoja amebakia na mipasho
Lema anasumbuliwa na tatizo la kutokuwa na Elimu dunia ya kutosha ,imagine anatumia bilia kulaani fikra zake mwenyewe🙆‍♂️🙆‍♂️🙆‍♂️
 
chadema baada ya kutokujipanga na kuelekeza nguvu kwenye vitimbi vya matembezi sasa wanatafuta nusura baharini
 
This time ccm wataabika sana , kila mtaa mashinay za chama kuanzia mtaa wapitie jina moja moja , na pale inapogundulika mwandikishaji aliingiza majina bandia au wasio na vigezo ,aburuzwe mahakamani kwa jina binafsi , tuone kama ccm watawatetea nchi nzima kwa kuwawekea wanasheria nchi nzima

Uchaguzi ni November 2025 ,twende kazi ,mda bado upo
 
Huku Tanzania ikijiandaa kwa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mnamo Novemba 27, Chadema inaonekana kuingia katika hali ya sintofahamu inayofichua woga wa kushindwa.

Zoezi la kujiandikisha kwenye daftari la makazi linaendelea kutoka Oktoba 11 hadi 20, lakini matamshi ya viongozi wa Chadema yanaibua maswali kuhusu dhamira yao ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi huu.

Leo, Godbless Lema, mwenyekiti wa Kanda ya Kaskazini na mbunge wa zamani wa Arusha Mjini kupitia Chadema, amefanya mkutano na waandishi wa habari, akitoa lugha kali zilizojaa matusi kwa wasimamizi wa uchaguzi.

Lema amemwita mmoja wa wakurugenzi “mshamba na mpuuzi,” akitishia kwamba iwapo uchaguzi huo hautawiana na matarajio yao, “vita ya wenyewe kwa wenyewe itatokea kwani Chadema watalipuka.”

Maneno haya yameonesha kwamba Chadema wanapanda mbegu za hofu na taharuki miongoni mwa wanachama wao, badala ya kujipanga kwa ushindani wa kweli.

Kama inavyojulikana, Chadema wametumia muda mwingi kulalamika kuliko kuhamasisha wanachama wao kujiandikisha na kushiriki kwenye uchaguzi wakati vyama vingine vikiweka mikakati ya kuwafikia wapiga kura, Lema anajikita zaidi katika matusi na malalamiko, ikiashiria kwamba chama chake hakijawa na mipango madhubuti ya ushindani.

Aidha, Lema alilalamika kuhusu uandikishaji wa vijana wa shule za sekondari, akisema, "Kwa nini watoto wa Form 3 wanaandikishwa?" Hii ni ishara ya kutokuwa na uwezo wa kuelewa sheria na taratibu za uchaguzi, kwani Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaruhusu vijana wenye miaka 18 na wale wenye miaka 17 ambao mwakani watakuwa na umri wa kupiga kura.

Badala ya kujiandikisha na kuwajengea vijana uelewa kuhusu umuhimu wa kushiriki kwenye uchaguzi, Lema na Chadema wanaendelea na malalamiko yasiyo na msingi.

Kwa mujibu wa Lema, licha ya baadhi ya wanachama wa Chadema kuonesha nia ya kususia uchaguzi huu, yeye amesisitiza kwamba atashiriki, akijinasibu kuwa "jasiri" asiyeogopa kushindwa.

Hata hivyo, kauli hii imeonesha kujificha nyuma ya ujasiri wa maneno, wakati ukweli ni kwamba Chadema hawana mipango ya kina ya kushinda.

Je, hii inamaanisha kuwa Chadema wanajaribu kuhalalisha hatua yao ya kusitasita, wakitafuta kisingizio cha kushindwa mapema huku wakihamasisha hofu kwa wapiga kura?

Je, ni woga wa ushindani au ni mikakati ya kujitenga na kushindwa?

Muda utaamua, lakini kwa mtindo huu wa kujiandaa, ni dhahiri kwamba Chadema wanakabiliwa na changamoto kubwa ya kushinda uchaguzi ujao.

IMG-20241014-WA0040(1).jpg
 
Ya hawa maccm dawa yao ndogo sana
Wanajisumbua kuandikisha watu mara mia mia sasa kwenye System si itaonyesha tu? Na Mimi mtaani kwetu yakibandikwa majina ya wapiga kura nitaanza kufanya research ya kujua huyu anakaa wqpi na anaishi nyumba ipi. Mbona simple hiyo ni kazi ya siku mbili tu nakua nishamaliza na Kwenye kampeni hawa inatakiwa kupiga spana za nguvu mpaka Wananchi wabadilike. Mwendazake alilia pale Kawe. Niliteeni Gwajima nileeteeni Gwajima na alipendwa na wengi watakuwa hawa Watu wanakufa watu wanatekwa na kupotea halafu Mwenyekiti wao anasema drama.
Erythrocyte
 
Mkuu Erythrocyte Kampeni ndio zitakazobadilisha upepo na tunawapiga mapema lifikishe juu lijadiliwe hili. Na Kampeni zipewe uzito.
Nimekuambia hotuba ya Martin Luther ilikuwa ya dk 17 tu. Je sisi hizi kampeni za Serikali tena mtaani karibia wiki nzima tunashindwa vipi?
Nina hasira nao hawa
 
This time ccm wataabika sana , kila mtaa mashinay za chama kuanzia mtaa wapitie jina moja moja , na pale inapogundulika mwandikishaji aliingiza majina bandia au wasio na vigezo ,aburuzwe mahakamani kwa jina binafsi , tuone kama ccm watawatetea nchi nzima kwa kuwawekea wanasheria nchi nzima

Uchaguzi ni November 2025 ,twende kazi ,mda bado upo
Hiyo kazi ngumu kupitia jina moja moja yaani ukiwa na smartphone una scan majina yote halafu unaya save kwenye pdf format baadae unaingia kwenye computer una convert yawe kwenye excel format. Wajinga wote waliondikisha zaidi ya mara moja wote wataonekana na balaa ndio linaanzia hapo.
Cc: Erythrocyte
 
Serikali ifuatiilie taarifa za mlipuko wa ugonjwa usiojulikana mkoa wa Singida
Kata ya Stanza
Wilaya ya Manyoni Mashariki


Taarifa hii imetolewa na mwananchi anayetoka huko kupitia mtandao wa Sauti ya Watanzania (Clubhouse)
 
Back
Top Bottom