Uchaguzi 2020 Lema wewe sio wa kuomba kuchangiwa hela ya kampeni

Uchaguzi 2020 Lema wewe sio wa kuomba kuchangiwa hela ya kampeni

Aisee... anyway kuchangia ni hiyari hakuna tatizo hapo maana hata wagombea uongozi wa Marekani huchangiwa fedha za kuendesha kampeni.
 
I will be honest, its been difficult for us to raise funds so desperately needed- it is coming, please acknowledge.
 
Mbona kawaida hiyo, wewe umaskini wako tu unakusumbua...tena hiyo michango ni kipimo cha kukubalika.
Kwanza hatakiwi kutoa hata senti yake mfukoni!!
 
Lema kachanga akili dakika za majeruhi, kasoma alama za nyakati na kile kiganja kinacho andika ukutani. Safari hii ubunge haupati, ngoja arudishe nusu hasara kutoka kwa wajinga.
 
Natambua hilo mkuu lakini mbunge ambaye amekuwa mbunge wa awamu mbili mfululizo hiyo ni aibu.

Kumbuka sababu kubwa ya wabunge kulipwa mishahara na vinuua mgongo vikubwa ni sehemu ya maandalizi ya awamu inayofuata.

Huu ni ubinafsi mkubwa Sana wa viongozi wetu hakuna tofauti na ufisadi.
Viinua mgongo ni ni namba tu, huwa wanakatwa mikopo ya gari..200ml za migari yao sio ndogo.
 
Hii sio sawa.

Yaani starehe zao wengine ndio waingie gharama??
Nileteeni gwajimaaa aendeleza kurekodi movie yake


IMG_20201015_201602.jpeg
 
Lema umekuwa Mbunge wa Arusha mjini kwa vipindi viwili mfululizo, tena ukilipwa mamilioni ya shilingi kwa mwezi.

Kama hiyo haitoshi umelipwa viinua mgongo viwili kingine bado hakijapoa kabisa zaidi ya milioni 200...

View attachment 1601411
Huyo mchagga. Hawa watu wanaijua pesa balaaa
 
Lema umekuwa Mbunge wa Arusha mjini kwa vipindi viwili mfululizo, tena ukilipwa mamilioni ya shilingi kwa mwezi.

Kama hiyo haitoshi umelipwa viinua mgongo viwili kingine bado hakijapoa kabisa zaidi ya milioni 200...
Hivi huy Lema kawahi kuchangia nini pale jimboni Arusha?hiyo hela si afadhali mungechanguia shule kuliko kumchangia mtu binafsi ambaye ananufaika yeye binafsi na familia yake, Lema ni tajiri , kuomba kuchangiwa ni kuwaibia masikini mchana kweupe, huko bungeni hawakai ,kila siku wanagoma,amuombe Mbowe amchangie, hakuna aliyemtuma kugombea ubunge. halafu hawa si ndio walisema tususie Vodacom kumbe yeye bado anatumia Vodacom.
 
Kwenye vitabu vya ndani ya chama wataweka pesa zilizotumika kwenye kampeni wakati ki uhalisia kila mgonbea anapambana na hali yake.
 
Ni jambo la kawaida sana, Marekani wagombea wanachangiwa, mwenye dollar moja haya, mwenye dilkar tano hayaa

Kwahiyo sioni tatizo kwa wanaompenda Lema wakimchangia, ingawa mimi binafsi siwezi kumchangia mbunge, labda Lisu naweza kumchangia najuwa amedhurumiwa na mashetani kina Ndugai.
23 Jun 2020

Fundraising totals are in for the month of May, and for the first time in 2020, Joe Biden raised more money for his campaign than President Trump. Democratic strategist and CBS News political contributor Joel Payne joins CBSN's Tanya Rivero with more on the fundraising numbers and the latest on Biden's search for a running mate.
Source : CBS NEWS
 
Kama kuna wabunge wapuuzi sana na wasio na maana yoyote na sababu ya kuwa wabunge ni Halima Mdee na Godbless Lema.

Hawa wabunge ni wajinga sana wanapokuwa majukwaani.
Wanaongea mambo ya hovyo na ya kihunihuni kama vile wanagombea uongozi wa mateja wale wapiga Debe stend.

Vyama vya Upinzani viwe vinaangalia na watu wakuwapa Nafasi.

Arusha Lema atapata kura kwa Sababu ya watu kuichoka CCM lakini ni mtu asiyefaa kabisa.
Mwanzo alikua anaongea utumbo mtupu ,oooh mmepigika wote ,nikiwaomba hata buku hapo hamna labda Mimi ndio niwape ,;Sasa amebadili gia angani yeye ndio anaomba omba.

Wabunge wa Upinzani walichezea sana nafasi ya Ubunge kwa mambo ya kijinga sana.
Kama kuna MTU aliyewaharibia wabunge wa Upinzani na kuwapa wakati Mgumu sana wa Kurudi Bungeni ni Mbowe. Alishindwa kabisa kutumia nafasi yake kama kiongozi wa kambi Rasmi ya Upinzani kuwaongoza wabunge matokeo yake akawa anahamasisha migomo bungeni na kutoka nje. Alishindwa kabisa kuvaa viatu vya Makame Rashidi na Dr.Slaa.
Kutoka toka Bungeni kuliwasaidia nini wakati Bunge lilikua Gizani.

Upinzani una bahati Kumpata Lisu mwaka huu. Hao akina Lema wamepona kupitia mgongo wa Lisu. Kulalamika lalamika tu.
 
KWANZA TUNAOMBA CHADEMA WATUPE MAPATO NA MATUMIZI YA ZILE FEDHA ALIZOCHANGISHA LISU KWENYEMIKUTANO YAKE KWENYE ZILE NDOO NYEUPE, KIPINDI KILE CHA MWANZONII.
 
Alafu kama anaona gharama kubwa basi asigombee.
Hii nchi kuna wajinga wengi, huwezi amini kuna watu watachanga
Kampeni ni za chama sio za mtu binafsi. Ndio maana mgombea anapeperusha bendera ya chama.
Kuchangia kampeni ni suala LA dunia nzima, ndio ndio maana ukienda bungeni huzungumzi yako Bali ya chama na misimamo yake.
 
Kampeni ni gharama mkuu, ukisema uwekeze pesa binafsi kwenye kampeni unaweza komba akaunti zote alafu ukianguka ndio unarudi chini kabisa.

Kukodi magari, kumobilize watu, kuhost mikutano, kuzunguka mtaa kwa mtaa lazma utoe motisha kwa wapambe, bado media campaign, kuna mabango n.k

So kuepuka risk ni bora uchangishe ili uweze kucover gharama za uchaguzi bila kuziweka rehani mali binafsi
"Kukodi magari, kumobilize watu, kuhost mikutano, kuzunguka mtaa kwa mtaa lazma utoe motisha kwa wapambe, bado media campaign, kuna mabango n.k"

chadema uwa mnasema hamtoi hela kwenye mikutano yenu kama ccm mnasemaga ni rushwa,
mabango this round hakuna,
media na ndo wengine mnawafukuza.hiyo hela ata kama nikukodi magari ni mangapi na mnasema nyie hambebi watu kwenye malori. Acheni wizi na unyonyaji kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom