Lengai Ole Sabaya hawezi kugombea 2024 wala 2025, sababu hii hapa

Desprospero

JF-Expert Member
Joined
Feb 1, 2023
Posts
1,015
Reaction score
2,493
Nimesoma bandiko la mtu humu ndani akitoa wito kwa mfungwa Ole Sabaya akagombee Ubunge Jimbo la Hai.

Nimweka sawa mtoa wito na wengine wanaofikiria hivyo kwamba Sabaya hakuachiwa huru, hapana. Sabaya amekutwa na hatia na amehurumiwa kwenda jela mwaka mmoja isipokuwa ni kifungo cha nje!

Sheria yetu ya Uchaguzi inakataza mtu yeyote aliyewahi kushitakiwa na kuhukumiwa kwenda jela kwa kosa lolote la jinai ndani ya miaka mitatu iliyopita anakosa sifa ya kugombea iwe ni Serikali za Mitaa (2024) au Udiwani, Ubunge na Urais (2025). Kwa mantiki hiyo Sabaya atakosa sifa hizo. Mwacheni atumikie kifungo chake.
 
Hata kama angegombea nani angempitisha,?
labda Bashite awe mwenyekiti wa hicho chama ila syo Mama na Kinana
 
Woote wale wa sampuli ya Sabaya hawawezi gombea tena na LAANA ya Mwenyezimungu itawarudia SOONER OR LATER
 
Sheria inamtakbua mtu aliyehukumiwa kifungo za zaidi ya miezi 6 anakosa sifa ya kugombea, kimsingi Sabaya amekiri makosa kwakuwa haoni kama Serikali inampango wa kumaliza kes, DPP alifanya kila analoweza ili Sabaya akose sifa za kuwa mtumishi wa umma, kiufupi Serikali haikuwa na ushahidi wa kutosha wa kufunga Sabaya ila iliona akae tu ndani na Sabaya alijitahidi sana kuvumilia ili abaki na sifa yake ya kuwa mtumishi wa umma lakini mwisho wa siku ameonabhakuna dalili youote ya serikali kupeleka mashahidi.
 
Nisaidie ufafanuzi kidogo: Amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja, si atamaliza kifungo April 24? Je! November 24 na November 25 atakuwa Bado na kizuizi Cha kugombea?
 
Huna akili
 
Nisaidie ufafanuzi kidogo: Amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja, si atamaliza kifungo April 24? Je! November 24 na November 25 atakuwa Bado na kizuizi Cha kugombea?
Good question! Sheria inasema, "hajakutwa na hatia ya jinai ndani ya miaka 3 nyuma." Kwa maneno mepesi ni kwamba baada ya kumaliza kifungo umalize miaka 3 na siku moja + hapo unakuwa na sifa.
 
Kugombea au kutogombea Kwa mtu kama Sabayau kunaleta manufaa Gani Kwa mwananchi?
 
Kwanza anakubalika wap? Tuanzie hapo! Hakuna asiejua wengi walipatw mbeleko toka kwa JPM
 
Kuna watu mnapenda sana kuanzisha Thd aisee,
Sasa si ungemjibu tu hili jibu lako kwenye thd yake huyo aliyetoa wito kwa Sabaya kugombea bunge?
 
Hakuna linaloshindikana wakitaka awe MB atakuwa regardless his issues za mahakamani, trust me!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…