Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Lengai Ole Sabaya na Wenzake wawili wahukumiwa miaka 30 Jela kwa kosa la unyang'anyi wa kutumia silaha

Ana kesi za kutosha huko mahakamani, hukumu hii ikipita ajiandae kwa nyingine na nyingine na nyingine tena, nadhani CCM watafanya kamchezo kumkwepesha huyu mtu wao balaa linalomkaribia.
 
Wanajukwaa poleni kwa kumbukumbu ya kifo cha muasisi wa Taifa letu,Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bila shaka baada ya Hukumu ya Lengai Ole Sabaya kuhairishwa tarehe 1/10/2021 ilipangwa kwamba itatolewa leo. Hivyo tuelekeze masikio yetu katika viunga vya mahakama.
Sabaya atashinda, Sabaya akifungwa na Mbowe amefungwa maana Sabaya ni mbuzi wa kafara
 
Hakuna kesi hapo. Kulikuwa na maigizo tu. Mtu kashikiliwa lakini kila mahudhurio ya mahakamani kapata super black.
Tutasikia ngonjera za maigizo ya sheria na kuambiwa alipe faini maisha yaendelee. Na msihangae baada ya haya yote akateuliwa nafasi nyingine.
Bado anakesi nyingine hivyo hawezi kuachiwa huru, japo hii kesi atatoboa mapema sn.
 
Siasa ni mchezo wa kuigiza kwani huonagi kila wanapokwenda wanasiasa kuna kuwa na ma camera ! Hata wakiwa ofisini kwenye kikao kuna kua na ma camera!

Hiyo ni tamthilia mkuu utakuja kustuka baadae sanaa
 
Watu kwa kujifariji hamjambo, hamna kesi hapo, alihifadhiwa kwa usalama wake mwenyewe dhidi ya shambulio la kigaidi…
Hilo litakuwa ajabu lingine la dunia!!kwani leo ndio uamuzi wa kuwa ana kesi au hana?au umekurupuka mkuu?
 
Back
Top Bottom