deni
JF-Expert Member
- Aug 7, 2011
- 255
- 191
Nilizaliwa nikiwa sielewi chochote kuhusu huu ulimwengu na maisha kwa ujumla, kadri nilivyozidi kukua nilifundishwa mambo mengi. Dini ni miongoni mwa yale ambayo nilifundishwa wakati nakua, lakini leo nimefikia mahali nimeaza kuona kwamba Dini ni swala amabalo nilikua nafundishwa kwa msistizo mkubwa , lakini ki uhalisia sioni umuhimu wake.
Katika mjadala huu ni jaribu kuziwasilisha fikra zangu kwa kutumia dini ya kikristo kama reference, kwa kua hiyo ndo nilibahatika kuwa na uzoefu nayo; nimekua na uzoefu nayo kwa kuwa ni random chance tu imetokea nikazaliwa kwenye familia ya kikristu.
Wazazi wangu na viongozi wa dini walinifundisha, kupitia dini, kwamba kuna Mungu aliyeumba kila kitu kilichopo na huyo Mungu anasifa zifuatazo:
Nilifundishwa sifa nyingi za Mungu, ambazo nyingi zinakinzana, nyingine nimeshindwa kuzikumbuka kwa sasa wakati naandika.
Katika dini yangu nilifundishwa(indirectly), kutokuwasikiliza watu wa dini nyingine kuhusu imani zao. Dini yangu ilinifanya niwatazame watu wa dini nyingine kwa mtizamo wa mashaka na kiasi flani cha chuki, na wakati mwingi niliamini wao wapo upande mbaya. Cha ajabu ni kwamba watu wadini nyingine nao walinitazama kwa mtazamo huo huo.
Dini zinajaribu kuniaminisha kwamba natakiwa kuishi maisha ya kujiandaa ili nipate maisha mazuri ya mbinguni baada ya kufa, kwa sababu bila kufanya ivyo nitaishi maisha ya taaabu milele.
Najua dini nyingine zina baadhi ya mitizamo inayofanana na hii, kwa sababu kabla sijaamua kuzipuuzia dini nimekua nikijaribu kuzifuatilia, ila nyingi zinaonekana zina mitizamo mingi ya kukinzana na mingi isiyoeleweka kiakili.
Nimefikia mahali nimeamua kufikiria bila kuongozwa na dini ambazo nimezaliwa na kuzikuta tu. Nimebadili mitazamo na kuwa na mitazamo ifuatayo.
Kuhitimisha naomba niseme kwamba binadamu tumeacha dini zichukue furaha yetu, tunazihangaikia sana mpaka tunajiumiza kwa kitu kinachoonekana hakina umuhimu.
Nawasilisha, nikiuliza "Why should we care about religions?",

- Anaweza yote na anajua yote.
- Ana upendo kuliko wote, yeye ni mwema kuliko wote.
- Anachukia uovu, na atawachoma na kuwatesa milele wale walio mkosea.(kwa akili yangu hili kama linakinzana na sifa ya kuwa na upendo).
- Yeye ana kila kitu hana uhitaji (lakini hili linakinzana na pale nilipofundishwa kwamba Mungu anahitaji sifa na kuheshimiwa, tena kuna wakati Mungu anaonekana ana wivu)
- Aliumba kila kitu
- Alimuumba shetani ambaye mabaya yote yanaunganishwa na yeye, alafu badae akamuumba Yesu atuokoe (This is one of tricky things that God is described to do on us) yaani Mungu anatuchezesha kama midoli.
Nilifundishwa sifa nyingi za Mungu, ambazo nyingi zinakinzana, nyingine nimeshindwa kuzikumbuka kwa sasa wakati naandika.
Katika dini yangu nilifundishwa(indirectly), kutokuwasikiliza watu wa dini nyingine kuhusu imani zao. Dini yangu ilinifanya niwatazame watu wa dini nyingine kwa mtizamo wa mashaka na kiasi flani cha chuki, na wakati mwingi niliamini wao wapo upande mbaya. Cha ajabu ni kwamba watu wadini nyingine nao walinitazama kwa mtazamo huo huo.
Dini zinajaribu kuniaminisha kwamba natakiwa kuishi maisha ya kujiandaa ili nipate maisha mazuri ya mbinguni baada ya kufa, kwa sababu bila kufanya ivyo nitaishi maisha ya taaabu milele.
Najua dini nyingine zina baadhi ya mitizamo inayofanana na hii, kwa sababu kabla sijaamua kuzipuuzia dini nimekua nikijaribu kuzifuatilia, ila nyingi zinaonekana zina mitizamo mingi ya kukinzana na mingi isiyoeleweka kiakili.
Nimefikia mahali nimeamua kufikiria bila kuongozwa na dini ambazo nimezaliwa na kuzikuta tu. Nimebadili mitazamo na kuwa na mitazamo ifuatayo.
- · Ukweli ni kwamba sifahamu asili ya huu ulimwengu ni nini, kunawezekana kukawa kuna jibu la asili ya ulimwengu lakini mpaka sasa sijapata hata moja ambalo halina utata.
- Kitu nnacho kinachopatana na akili yangu kuhusu baada ya kufa, ni kwamba baada ya kufa kutakua ni sawa na kabla ya kuzaliwa kwangu. Hainiingii akilini kuhusu swala la kuteswa milele au kupewa raha milele.
- · Sioni umuhimu wa dini.
- · Kama Mungu (creator) yupo, basi inaonekana hana interest ya kuwasilia na sisi na kutuweka clear. Watu wengi wa dini wameshindwa kulielewa hili, ndio maana tunaona watu wanauana, kuchukiana na kujiua kisa dini-watu wa dini wanahangaika sana kumtetea Mungu wakati mwingine hata kuua, lakini Mungu mwenyewe muweza yote amejificha tu mahali pasipoonekana.
- · Kwangu mimi lengo la maisha ni KUISHI. Just kuishi.
- · Mema na mabaya ni vitu vinavyotambulika naturally, siamini kwamba dini inahitajika kutusaidia kutambua mema na mabaya.