Lengo la dini ni nini?

Lengo la dini ni nini?

kwani kuna ubaya gani wewe mwenyewe ukanieleza maana ya hilo neno? mimi sipo hapa ku-act kama najua kila kitu... mimi nakuruhusu unaweza kuendelea na kunielewesha unachoisi sikielewi.

Unauliza swali la kitu ambacho hukijuwi maana yake?

Kama umekiri hujuwi maana ya dini, sasa anza kwa kuuliza ujuzwe dini ni nini.
 
Endelea kuwepo tu na kuzitafuta hizo usemazo "fact" nyingine kwa kuwa hata wewe mwenye hujiamini kwa sababu umekiri kuwa upo tu.

Safari njema ya maisha.
ndo nnavyoona, sasa unataka niact kama nfahamu THE GREAT PURPOSE wakati ukweli ni kwamba sijawahi kuipata hiyo purpose.. kwa nini unaonkeakana kunibeza saana mimi kusema sifahamu lengo la maisha? kwani ww unalifahamu?
 
Nilizaliwa nikiwa sielewi chochote kuhusu huu ulimwengu na maisha kwa ujumla, kadri nilivyozidi kukua nilifundishwa mambo mengi. Dini ni miongoni mwa yale ambayo nilifundishwa wakati nakua, lakini leo nimefikia mahali nimeaza kuona kwamba Dini ni swala amabalo nilikua nafundishwa kwa msistizo mkubwa , lakini ki uhalisia sioni umuhimu wake.

Katika mjadala huu ni jaribu kuziwasilisha fikra zangu kwa kutumia dini ya kikristo kama reference, kwa kua hiyo ndo nilibahatika kuwa na uzoefu nayo; nimekua na uzoefu nayo kwa kuwa ni random chance tu imetokea nikazaliwa kwenye familia ya kikristu.

Wazazi wangu na viongozi wa dini walinifundisha, kupitia dini, kwamba kuna Mungu aliyeumba kila kitu kilichopo na huyo Mungu anasifa zifuatazo:

  • Anaweza yote na anajua yote.
  • Ana upendo kuliko wote, yeye ni mwema kuliko wote.
  • Anachukia uovu, na atawachoma na kuwatesa milele wale walio mkosea.(kwa akili yangu hili kama linakinzana na sifa ya kuwa na upendo).
  • Yeye ana kila kitu hana uhitaji (lakini hili linakinzana na pale nilipofundishwa kwamba Mungu anahitaji sifa na kuheshimiwa, tena kuna wakati Mungu anaonekana ana wivu)
  • Aliumba kila kitu
  • Alimuumba shetani ambaye mabaya yote yanaunganishwa na yeye, alafu badae akamuumba Yesu atuokoe (This is one of tricky things that God is described to do on us) yaani Mungu anatuchezesha kama midoli.

Nilifundishwa sifa nyingi za Mungu, ambazo nyingi zinakinzana, nyingine nimeshindwa kuzikumbuka kwa sasa wakati naandika.

Katika dini yangu nilifundishwa(indirectly), kutokuwasikiliza watu wa dini nyingine kuhusu imani zao. Dini yangu ilinifanya niwatazame watu wa dini nyingine kwa mtizamo wa mashaka na kiasi flani cha chuki, na wakati mwingi niliamini wao wapo upande mbaya. Cha ajabu ni kwamba watu wadini nyingine nao walinitazama kwa mtazamo huo huo.

Dini zinajaribu kuniaminisha kwamba natakiwa kuishi maisha ya kujiandaa ili nipate maisha mazuri ya mbinguni baada ya kufa, kwa sababu bila kufanya ivyo nitaishi maisha ya taaabu milele.

Najua dini nyingine zina baadhi ya mitizamo inayofanana na hii, kwa sababu kabla sijaamua kuzipuuzia dini nimekua nikijaribu kuzifuatilia, ila nyingi zinaonekana zina mitizamo mingi ya kukinzana na mingi isiyoeleweka kiakili.

Nimefikia mahali nimeamua kufikiria bila kuongozwa na dini ambazo nimezaliwa na kuzikuta tu. Nimebadili mitazamo na kuwa na mitazamo ifuatayo.

  • · Ukweli ni kwamba sifahamu asili ya huu ulimwengu ni nini, kunawezekana kukawa kuna jibu la asili ya ulimwengu lakini mpaka sasa sijapata hata moja ambalo halina utata.
  • Kitu nnacho kinachopatana na akili yangu kuhusu baada ya kufa, ni kwamba baada ya kufa kutakua ni sawa na kabla ya kuzaliwa kwangu. Hainiingii akilini kuhusu swala la kuteswa milele au kupewa raha milele.
  • · Sioni umuhimu wa dini.
  • · Kama Mungu (creator) yupo, basi inaonekana hana interest ya kuwasilia na sisi na kutuweka clear. Watu wengi wa dini wameshindwa kulielewa hili, ndio maana tunaona watu wanauana, kuchukiana na kujiua kisa dini-watu wa dini wanahangaika sana kumtetea Mungu wakati mwingine hata kuua, lakini Mungu mwenyewe muweza yote amejificha tu mahali pasipoonekana.
  • · Kwangu mimi lengo la maisha ni KUISHI. Just kuishi.
  • · Mema na mabaya ni vitu vinavyotambulika naturally, siamini kwamba dini inahitajika kutusaidia kutambua mema na mabaya.

Kuhitimisha naomba niseme kwamba binadamu tumeacha dini zichukue furaha yetu, tunazihangaikia sana mpaka tunajiumiza kwa kitu kinachoonekana hakina umuhimu.

Nawasilisha, nikiuliza "Why should we care about religions?",
"When I was a child, I spoke like a child, I thought like a child, I reasoned like a child. When I became a man, I gave up childish ways." (1 Corinthians 13:11).

Apparently there's existence of a substantial, intelligent, educated atheist/agnostic community, and by the hundreds of mutually contradictory opinions about the gods believed in (i.e., religions). But the evidence for any supernatural beings is clearly inadequate to explain the widespread and profound belief in so many particular ones. Scientific and philosophical argument has, it seems, convinced no one and changed very few minds on the matter.

it cannot explain the ubiquitous belief in gods across almost every culture on Earth because no consensus has developed supporting belief in any of them even after several thousand years of research and debate
 
dini ni nini, FaizaFoxy?

Kwanza ukumbuke kuwa neno "dini" limetokana na lugha ya Kiarabu, kwa ukaribu kabisa wa kulifafanua Kiswahili, linamaanisha "njia".

Kwa mafunzo ya Uislam dini (njia) ya kufika kwa (ayatakayo) Allah (Mwenyeezi Mungu) ni Uislam (kujisalimisha kwa Allah (Mwenyeezi Mungu) mmoja.

Katika Uislam tunajifunza kuwa hakuna kulazimishana katika dini (njia). Wewe una yako nami nina yangu. Isipokuwa kuna kueleweshana tu na kuelimishana kwa apendae kujuwa.
 
Mbona tumuona na kushuhudia matukio mengi tu ya kulazimisha watu wawe waislam tena hata kuwaua maelfu kwa maelfu...Boko haram ndio kazi waliyo tumwa na kiongozi wenu ambaye sitamtaja kwa sababu maalum..._,hilo unalionaje.?
 
ndo nnavyoona, sasa unataka niact kama nfahamu THE GREAT PURPOSE wakati ukweli ni kwamba sijawahi kuipata hiyo purpose.. kwa nini unaonkeakana kunibeza saana mimi kusema sifahamu lengo la maisha? kwani ww unalifahamu?

Mkuu nimeukubali sana upeo wako I,e uko na fikra pevu.
 
mie nipo tu duniani, ili nishi. na kuishi huko patafika mwisho pale nitakapokufa. na maisha yataendelea kwa watu na viumbe vingine, nao watakufa badae.. kwangu mie naona ulimwengu ni ON AND OFF SYSTEM sio kwa binadamu tu pekeake, bali na kwa wanyama na mimea na kila kitu kilichopo. kwa hiyo mimi na wewe tupo kama vile kiumbe kingine kilivyo na tuna-obey natural laws. (mtazamo wangu huu unaweza ukabadilika wakati wowote nitakapopata fact nyingine zenye mashiko zaidi)

Laiti kama robo tu ya wakaazi wa dinia hii wangekua na akili na fikra kama hizi..basi dunian pangekuwa na mahali salama na pazuri sana pa kuishi.._ila ndio hivyo tena dunia imejazwa na watu wenye mihemko ya hizi dini I,e wamejazwa roho mbaya ya visasi,chuki,husda na dini zao kiasi cha kufanya maasi na mauaji ya kutisha.
 
better shut up!! Kumbe huelewi chochote,unarandaranda tu

Yamekuingia ndiyo maana umejibu, la sivyo ungekaa wewe kimya. Watu hawadandii daladala kwa mbele.

Wewe itakuwa katika wale waliopewa dozi na Mkapa.
 
“When I was a child, I spoke like a child, I thought like a child, I reasoned like a child. When I became a man, I gave up childish ways.” (1 Corinthians 13:11).

Apparently there's existence of a substantial, intelligent, educated atheist/agnostic community, and by the hundreds of mutually contradictory opinions about the gods believed in (i.e., religions). But the evidence for any supernatural beings is clearly inadequate to explain the widespread and profound belief in so many particular ones. Scientific and philosophical argument has, it seems, convinced no one and changed very few minds on the matter.

it cannot explain the ubiquitous belief in gods across almost every culture on Earth because no consensus has developed supporting belief in any of them even after several thousand years of research and debate

Sijaelewa chochote...nehi yaani
 
Ana point lakini waliolewa dini wanajitoa ufahamu wanamjibu kimapokeo tena kwa jazba kana kwamba analazimishwa kuamini.

Dini ni mapokeo..na binadamu ndo wamecreate...zinaweza zikawa na maana na zinaweza pia zikawa hazina maana yoyote. Dini ingeleta maana Kama binadamu wote tungekuwa na imani moja tunaamini kitu kimoja. Sasa dini zipo lukuki kila moja na imani yake na sheria yake. Tuache ipi na tufate ipi
 
"Dini ni serikali ndogo" kuheshimu sheria na utawala ( Rules and Laws ) deni ukivunja sheria lazima uadhibiwe !!
 
Last edited by a moderator:
Kwanza ukumbuke kuwa neno "dini" limetokana na lugha ya Kiarabu, kwa ukaribu kabisa wa kulifafanua Kiswahili, linamaanisha "njia".

Kwa mafunzo ya Uislam dini (njia) ya kufika kwa (ayatakayo) Allah (Mwenyeezi Mungu) ni Uislam (kujisalimisha kwa Allah (Mwenyeezi Mungu) mmoja.

Katika Uislam tunajifunza kuwa hakuna kulazimishana katika dini (njia). Wewe una yako nami nina yangu. Isipokuwa kuna kueleweshana tu na kuelimishana kwa apendae kujuwa.
Na kunibeza kote kule, ndio umekuja kutoa mawazo yaliyo ndani ya box kama hayo? mie naona inabidi ufikirie kiupana zaidii
 
Back
Top Bottom