Lengo la dini ni nini?

deni

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2011
Posts
255
Reaction score
191
Nilizaliwa nikiwa sielewi chochote kuhusu huu ulimwengu na maisha kwa ujumla, kadri nilivyozidi kukua nilifundishwa mambo mengi. Dini ni miongoni mwa yale ambayo nilifundishwa wakati nakua, lakini leo nimefikia mahali nimeaza kuona kwamba Dini ni swala amabalo nilikua nafundishwa kwa msistizo mkubwa , lakini ki uhalisia sioni umuhimu wake.

Katika mjadala huu ni jaribu kuziwasilisha fikra zangu kwa kutumia dini ya kikristo kama reference, kwa kua hiyo ndo nilibahatika kuwa na uzoefu nayo; nimekua na uzoefu nayo kwa kuwa ni random chance tu imetokea nikazaliwa kwenye familia ya kikristu.

Wazazi wangu na viongozi wa dini walinifundisha, kupitia dini, kwamba kuna Mungu aliyeumba kila kitu kilichopo na huyo Mungu anasifa zifuatazo:


  • Anaweza yote na anajua yote.
  • Ana upendo kuliko wote, yeye ni mwema kuliko wote.
  • Anachukia uovu, na atawachoma na kuwatesa milele wale walio mkosea.(kwa akili yangu hili kama linakinzana na sifa ya kuwa na upendo).
  • Yeye ana kila kitu hana uhitaji (lakini hili linakinzana na pale nilipofundishwa kwamba Mungu anahitaji sifa na kuheshimiwa, tena kuna wakati Mungu anaonekana ana wivu)
  • Aliumba kila kitu
  • Alimuumba shetani ambaye mabaya yote yanaunganishwa na yeye, alafu badae akamuumba Yesu atuokoe (This is one of tricky things that God is described to do on us) yaani Mungu anatuchezesha kama midoli.

Nilifundishwa sifa nyingi za Mungu, ambazo nyingi zinakinzana, nyingine nimeshindwa kuzikumbuka kwa sasa wakati naandika.

Katika dini yangu nilifundishwa(indirectly), kutokuwasikiliza watu wa dini nyingine kuhusu imani zao. Dini yangu ilinifanya niwatazame watu wa dini nyingine kwa mtizamo wa mashaka na kiasi flani cha chuki, na wakati mwingi niliamini wao wapo upande mbaya. Cha ajabu ni kwamba watu wadini nyingine nao walinitazama kwa mtazamo huo huo.

Dini zinajaribu kuniaminisha kwamba natakiwa kuishi maisha ya kujiandaa ili nipate maisha mazuri ya mbinguni baada ya kufa, kwa sababu bila kufanya ivyo nitaishi maisha ya taaabu milele.

Najua dini nyingine zina baadhi ya mitizamo inayofanana na hii, kwa sababu kabla sijaamua kuzipuuzia dini nimekua nikijaribu kuzifuatilia, ila nyingi zinaonekana zina mitizamo mingi ya kukinzana na mingi isiyoeleweka kiakili.

Nimefikia mahali nimeamua kufikiria bila kuongozwa na dini ambazo nimezaliwa na kuzikuta tu. Nimebadili mitazamo na kuwa na mitazamo ifuatayo.


  • · Ukweli ni kwamba sifahamu asili ya huu ulimwengu ni nini, kunawezekana kukawa kuna jibu la asili ya ulimwengu lakini mpaka sasa sijapata hata moja ambalo halina utata.
  • Kitu nnacho kinachopatana na akili yangu kuhusu baada ya kufa, ni kwamba baada ya kufa kutakua ni sawa na kabla ya kuzaliwa kwangu. Hainiingii akilini kuhusu swala la kuteswa milele au kupewa raha milele.
  • · Sioni umuhimu wa dini.
  • · Kama Mungu (creator) yupo, basi inaonekana hana interest ya kuwasilia na sisi na kutuweka clear. Watu wengi wa dini wameshindwa kulielewa hili, ndio maana tunaona watu wanauana, kuchukiana na kujiua kisa dini-watu wa dini wanahangaika sana kumtetea Mungu wakati mwingine hata kuua, lakini Mungu mwenyewe muweza yote amejificha tu mahali pasipoonekana.
  • · Kwangu mimi lengo la maisha ni KUISHI. Just kuishi.
  • · Mema na mabaya ni vitu vinavyotambulika naturally, siamini kwamba dini inahitajika kutusaidia kutambua mema na mabaya.

Kuhitimisha naomba niseme kwamba binadamu tumeacha dini zichukue furaha yetu, tunazihangaikia sana mpaka tunajiumiza kwa kitu kinachoonekana hakina umuhimu.

Nawasilisha, nikiuliza "Why should we care about religions?",
 
Wewe unaelewaje maana ya neno dini ni nini halafu
2: jiulize je kuwa na dini ni lazima?
3:jiulize dhumuni la mungu kumuumba mwanadamu ni nn?

hakuna evidence kwamba mungu amemuumba mwanadamu.

na kama ni kweli mungu alituuumba na kama anajali kuhusu sisi, basi yeye anajukumu la kutuweka clear dhumuni lake ni lipi?

mimi sioni sababu ya kujifanya tunalifahamu dhumuni la mungu(ambaye haeleweki kama yupo au hayupo).
 
Mbulaaa......unautak auwendawizumu muda sio mrefu! AAcha kabisa kufikiri juu ya uwepo wa Mungu,..

Wewe kama unaamini hayupo kaa kimya..

Kama unaamini yupo, endelea kumwabudu na kumsifu milele!
 
Mbulaaa......unautak auwendawizumu muda sio mrefu! AAcha kabisa kufikiri juu ya uwepo wa Mungu,..

Wewe kama unaamini hayupo kaa kimya..

Kama unaamini yupo, endelea kumwabudu na kumsifu milele!
kwa nini nikae kimya? kwani kuna uhusiano gani kati ya kufikiria kuhusu uwepo wa mungu na uwenda wazimu?
 
Unaamini Mungu yupo au hayupo? deni
 
Last edited by a moderator:
Umeuliza lengo la "dini" ni nini. Mwisho ukaishia kuuliza kuhusu "religions".

Nilichokiona hapo, kwanza kabisa hauelewi maana ya neno "dini", ukiielewa utajuwa kuwa "dini" haina lengo.

Kwanza jifunze uelewe maana ya neno "dini" na neno "religion" na uelewe kuyatofautisha, kisha urudi hapa kuuliza vizuri.
 
Zaburi 14:1...Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu.....nakuomba hebu jiepushe na jina la upumbavu kwa kuamini kuwa yupo...halafu mambo mengine ya uelewa yatafuata
 


Kumbe ndugu Deni huelewi hata maana ya hivo vitu ulivyouliza Din i
 
deni wewe upo duniani na unaishi kwa bahati mbaya tu> Au ni nzuri tu?

Nini sababu zako za kuwepo?
 
Last edited by a moderator:
kwakiasi furan nipo upande wako deni maana wakat mwingine nashindwa kuelewa ni zumun gan ama lengo gn lilifanya tuwe na hisi dini mbili, tena zikiwa sinakinzana kwakiasi kikubwa japo zote zinadai zana mwabudu Mungu mmoja..! swali kama dini zote zina mwabudu Mungu mmoja ni kipivi ziwe zinatofautino ktk vitambu vyao haswa swala la umbaji?? wenye kujua ukwel wa hii kitu atujuze tafaze zaidi
 
Last edited by a moderator:

Kuna mwalimu nimemuomba apitie hapa awape majibu kuhusu dini na ukweli kumhusu Mungu muumbaji.
 
Last edited by a moderator:
kwani kuna ubaya gani wewe mwenyewe ukanieleza maana ya hilo neno? mimi sipo hapa ku-act kama najua kila kitu... mimi nakuruhusu unaweza kuendelea na kunielewesha unachoisi sikielewi.
 
Zaburi 14:1...Mpumbavu amesema moyoni hakuna Mungu.....nakuomba hebu jiepushe na jina la upumbavu kwa kuamini kuwa yupo...halafu mambo mengine ya uelewa yatafuata

naomba unieleze vizuri nawezaje kuwa mpumbavu kwa kusema ukweli jinsi nnavyoyaona mambo?
 
deni wewe upo duniani na unaishi kwa bahati mbaya tu> Au ni nzuri tu?

Nini sababu zako za kuwepo?
mie nipo tu duniani, ili nishi. na kuishi huko patafika mwisho pale nitakapokufa. na maisha yataendelea kwa watu na viumbe vingine, nao watakufa badae.. kwangu mie naona ulimwengu ni ON AND OFF SYSTEM sio kwa binadamu tu pekeake, bali na kwa wanyama na mimea na kila kitu kilichopo. kwa hiyo mimi na wewe tupo kama vile kiumbe kingine kilivyo na tuna-obey natural laws. (mtazamo wangu huu unaweza ukabadilika wakati wowote nitakapopata fact nyingine zenye mashiko zaidi)
 

Endelea kuwepo tu na kuzitafuta hizo usemazo "fact" nyingine kwa kuwa hata wewe mwenye hujiamini kwa sababu umekiri kuwa upo tu.

Safari njema ya maisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…