Mkutano wa kilele wa 19 wa Kundi la Nchi 20 (G20) umefanyika hivi karibuni mjini Rio de Jeneiro, Brazil. Rais wa China Xi Jinping amesema katika mkutano huo kwamba, China imetangaza uamuzi wa kuzipatia nchi zote zilizo nyuma kimaendeleo zenye uhusiano wa kibalozu na China huduma ya kuondoa ushuru kwa asilimia 100.
Awali, rais Xi alisema kuwa maendeleo yanapaswa kuwa kiini cha ushirikiano wa G20, hatua inayoendana na kaulimbiu ya mwaka huu ya Kundi hilo, “Kujenga Dunia ya Haki na Sayari Endelevu” iliyotolewa na Brazil, nchi mwenyekiti wa G20.
Hatua hii inaliwezesha Kundi hilo kuendelea kujikita katika masuala ya maendeleo, na kuleta matarajio mazuri kwa jamii ya kimataifa.
Mkutano huo ulikuwa na ajenda kuu tatu, ambazo ni kukabiliana na njaa, umasikini na ukosefu wa usawa, kushughulika na mabadiliko ya tabianchi, na kubadilisha mfumo wa utawala wa dunia.
Ajenda mbili kati ya hizo zinahusiana moja kwa moja na maendeleo, na kusisitiza mabadiliko muhimu katika Kundi la Nchi 20 katika miaka ya karibuni, ambapo kundi hilo limebadilika hatua kwa hatua kutoka jukwaa la majadiliano ya dharura kwa ajili ya kukabiliana na migogoro na kuwa mfumo wa muda mrefu wenye ufanisi wa utawala unaolenga kuboresha utaratibu wa dunia mbao ni wa haki zaidi, jumuishi, na wa usawa.
Mabadiliko mengine ya kihistoria ni kuwa sauti za nchi za Dunia ya Kusini zimeongezeka, huku mahitaji zaidi kutoka nchi zinazoendelea yakionekana katika ajenda za G20.
Kutimiza mageuzi hayo sio kazi rahisi, hususan katika miaka ya karibuni ambapi vitendo vya kujilinda kibiashara na vya upande mmoja vimekuwa vikiongezeka duniani, pia mivutano kati ya pande mbalimbali imeongezeka, na masuala ya siasa za kijiografia mara kwa mara yameibuka, hivyo kukandamiza ushirikiano wa kimkakati ndani ya majukwaa ya pande nyingi.
Hata hivyo, G20 haikufuata mwelekeo huo. Katika mkutano wa kilele wa G20 uliofanyika Hangzhou, China mwaka 2016, China, kama nchi mwenyeji, iliweka maendeleo kama kiini kwa mara ya kwanza, na kuboresha kwa ufanisi mageuzi ya G20 kutoka katika masuala ya kiuchumi pekee mpaka kushughulikia masuala mengine mengi, ikiwemo maendeleo, mwelekeo ambao umeendelea mpaka hivi sasa.
Katika miaka ya karibuni, China imekuwa ikiboresha mageuzi ya aina hiyo, kwa mfano, imependekeza na kuendeleza ajenda kuu muhimu kama uchumi wa kidijitali na akili bandia, huku ikitambulisha ajenda kama uchumi wa kijani. China imeshikilia bila kusita uhusiano wa pande nyingi,
kutetea kuheshimiana, ushirikiano wa usawa, na matokeo ya kunufaishana, na hivyo kukabiliana kwa ufanisi na kuingilia kati vitendo vya upande mmoja na kujilinda kibiashara ndani ya G20.
G20 kujikita katika masuala ya maendeleo sio tu kunasaidia nchi zilizo Dunia ya Kusini kutimiza maendeleo makubwa, lakini pia ni manufaa kwa nchi za Magharibi zilizoendelea. Jumla ya uchumi wan chi wanachama wa G20 inachukua karibu asilimia 85 ya pato la jumla la dunia, na thamani yao ya biashara inawakilisha asilimia 80 ya jumla ya dunia.
Kundi hili linajumuisha nchi zilizoendelea kiuchumi na zinazoibuka kwa kasi kiuchumi, hata baadhi ya nchi za Magharibi ambazo mara nyingi zimekuwa na upendeleo, zimekiri umuhimu wa nafasi ya G20, na kusisitiza kuwa majadilianno katika jukwaa la Kundi hilo yanapaswa kupewa kipaumbele.
Kutoka Hangzhou mpaka Rio, maendeleo yamebaki kuwa ajenda kuu ambayo inafuatiliwa sana katika mikutano ya kilele ya G20. Kutimiza maafikiano makubwa na matokeo dhahiri katika maendeleo ndani ya G20 ni jambo ambalo kila upande unategemea na pia ni matakwa ya umma.