Lengo la rais wa yanga kuwaita mashabiki wa timu yake wala mihogo

Jesus Mlokozi

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2022
Posts
2,684
Reaction score
21,117
Kitendo alichokifanya rais wa yanga ni udhalilishaji wa hali ya juu. Ameonesha namna gani alivyo na dharau na kuwapuuzia mashabiki wa timu ya yanga.

Yanga ilikuwepo tangu miaka ya 1935. Viongozi walimtangulia walikuwa wakiheshimu mashabiki.

Ni kweli mihogo ni chakula mambacho watu wengi wanatumia hapa nchini. Lakini kwa namna alivyosema ni kana kwamba yeye yupo na maisha bora kwamba wala mihogo, hohehahe na watu wa chini hawana cha kuongea ndani ya yanga.

Hizi tabia za kibepari na kunyanyasa watanzania zilikemewa sana na baba wa taifa. Hizi ni tabia za kuwagawa watanzania kwamba wenyenacho na wasionacho. Ni dhahili kwa sasa yanga imewekwa mfukoni mwa watu wachache. Wanawatumia mashabiki kwa manufaa yao binafsi na siyo kwaajili ya timu.

Naiomba TFF ikemee kauli hizi za kibeberu zinazohatarisha amani katika nchi yetu.

Huwezi ukawaita watu walamihogo, tena kwadharau kabisa.
Mpira wa miguu ni furaha na mahusiano mazuri.
 
Wala mihogo ndiyo wanajaza uwanja, hataki timu ikifanya vibaya wala mihogo wasitoe maoni yao maana hawachangii hata mia, anayepaswa kuumia ni GSM.
Na siku GSM Akitoa mkono wake pale
Au tutarudi zile zama za CHANGIA YANGA

TIMU YA WANANCHI
Mnaanza kusumbua tena wala mihogo mwisho iwakwame
 
FB_IMG_1667477964960.jpg
 
Kitendo alichokifanya rais wa yanga ni udhalilishaji wa hali ya juu. Ameonesha namna gani alivyo na dharau na kuwapuuzia mashabiki wa timu ya yanga.

Yanga ilikuwepo tangu miaka ya 1935. Viongozi walimtangulia walikuwa wakiheshimu mashabiki.

Ni kweli mihogo ni chakula mambacho watu wengi wanatumia hapa nchini. Lakini kwa namna alivyosema ni kana kwamba yeye yupo na maisha bora kwamba wala mihogo, hohehahe na watu wa chini hawana cha kuongea ndani ya yanga.

Hizi tabia za kibepari na kunyanyasa watanzania zilikemewa sana na baba wa taifa. Hizi ni tabia za kuwagawa watanzania kwamba wenyenacho na wasionacho. Ni dhahili kwa sasa yanga imewekwa mfukoni mwa watu wachache. Wanawatumia mashabiki kwa manufaa yao binafsi na siyo kwaajili ya timu.

Naiomba TFF ikemee kauli hizi za kibeberu zinazohatarisha amani katika nchi yetu.

Huwezi ukawaita watu walamihogo, tena kwadharau kabisa.
Mpira wa miguu ni furaha na mahusiano mazuri.
Kwa akili kama hizi Hersi yuko sahihi kabisa
IMG-20221103-WA0015.jpg
 
Back
Top Bottom