Msanii
Platinum Member
- Jul 4, 2007
- 25,252
- 36,513
Kuwakamata na kuwashtaki wakosoaji wa mkataba mbovu wa DPW na Tanzania ni picha inayodhihirisha lengo la serikali yetu tukufu inayojitukuza kuliko uwepo wa Mungu.
Wakili Mwabukusi, Nyangali, Slaa ni public figures ambao serikali inahofia kuwanyamazisha kama ilivyojaribu kwa Tundu Lissu hapo awali.
Kuwashtaki kwa kosa la Uhaini ni picha inaiweka serikali kwenye mizania ya malengo yake kwa hatua mbalimbali za kuizima hii hoja inayojadiliwa sasa nchi nzima na wananchi.
USHAURI
Serikali iwaachie wanaharakati na wakosoaji wanaohoji maudhui ya mkataba huu ambao kila mtu sasa amegundua kuwa tunawekwa rehani.

- Serikali inabidi ikubali kukosolewa kwa kila hatua inayopiga ya maendeleo
- Ukosoaji na kupinga waziwazi siyo tishio kwa ustawi wetu kama nchi bali ni afya ya ushindani wa kifikra hususani kwenye kujenga hoja
- Kuwajengea hofu wananchi kwa kuonesha matumizi makubwa ya nguvu kupitia dola ni kuongeza athari za kukosa uvumilivu wa hoja na kisiasa
- Serikali kufanya maamuzi na yakaleta utata kimantiki ni vyema ikatumia njia za kidemokrasia kuzikabili hoja kuliko mabavu na vitisho
- Mimi kama mwananchi sijioni salama mbele ya serikali yangu. Kwa nini serikali inishughilikie kwa kutoiamini? Je, NI LAZIMA kuiamini serikali kwenye kila kitu?
Serikali iwaachie wanaharakati na wakosoaji wanaohoji maudhui ya mkataba huu ambao kila mtu sasa amegundua kuwa tunawekwa rehani.