Lengo la Serikali ni kuwaua wakosoaji? Kesi ya Uhaini ni eneo la kujifunza

Lengo la Serikali ni kuwaua wakosoaji? Kesi ya Uhaini ni eneo la kujifunza

Serikali, serikali, serikali. Mimi labda uelewa wangu ni mdogo. Hivi hili dude linaloitwa serikali ni nani? Maana naona kutokana na maoni ya watu wengi humu JF watu wengi wanaliogopa sana hili dude. Hili dude linapata wapi hizi nguvu zisizo na mipaka mpaka watu wanatetemeka wakisiki jina lake.

Katiba yetu inasemaje kuhusu serikali. Inapata wapi mamlaka na inawajibika kwa nani?

Sisi watz ni watu wa ajabu sana ndiyo maana jirani zetu wanatudharau. Kwa hao vibaraka wa "serikali" wafikishieni ujumbe kwamba mbio za sakafuni huidhia ukingoni na siku zote Mungu hanwavhi mja wake.
Sweikali ni dude kuuubwa sana ambalo linawajibika kwa taasisi moja tu na siyo kuwajibika kwa wananchi
 
we elimu yako ni kiwango gani, uchochezi, uzushi, upotoshaji, uhaini siyo ukosoaji. Nchi hii ina sheria na taratibu zake, ina viongozi walioapa kulinda ulinzi na usalama wa nchi yetu, lazima utii sheria za nchi vinginevyo unashughulikiwa. Wale ni wahalifu kila mtu alikuwa anawasikia walichokuwa wanahubiri usituletee upuuzi wako kaa kimya wacha washughulikiwe wapuuzi wale.

Watu wanaongea kabisa kumwondoa rais madarakani, wanaongea habari za kuvunja muungano, wanatukana, wanachochea wananchi kufanya maanadamano ya kuitoa serikali madarakani kwa njia haramu bado useme wanakosoa, we akili umemwazima nani, tuanzie hapo.

Watu wanasema tuamke tusiogope, huu siyo uchochezi? Muungano ni mojawapo ya tunu za taifa letu. siyo wa kuuchezea, aliondolewa aliyekuwa rais wa Zanzibar Aboud Jumbe kutaka kuvunja muungano, sembuse hao sisimizi? Hakuna mtu wa kuuvunja huu muungano una manufaa zaidi kuliko kitu kingine chochote. Hata hivyo wanzanzibari km siyo wote wengi wao ni wenyeji wa Tanzania bara mfano mzee Ally Hassan Mwinyi alihamia Zanzibar akiwa mtoto mdogo, alizaliwa Pwani wilaya ya Mkuranga.

Nenda pale Tanga, ndugu zao wako Pemba, Unguja wengi walitokea mikoa ya Pwani na Dar Es Salaam. Kutoka Dar mpaka Unguja(Zanzibar) ni kilomita 50 tu, kwanza nawashangaa akina Mwabukusi, Nshalla, Slaa na wengine kujifanya wana uchungu na bandari ambayo iko kilomita zaidi ya 1000 kutoka walikozaliwa mpaka iliko bandari kuliko waliozaliwa na kukulia karibu na bandari yenyewe.

Wazanzibar km siyo wakoloni kuigawa nchi zetu ndio wangelikuwa wenye bandari ya Dar Es Salaam kuliko siye tulio mbali huku bara. Muungano wetu una mkono wa Mungu mwenyewe na hautakaa uvunjike, sisi ni ndugu.
Katiba na Sheria inahalalisha Uchochezi na kuutoa madarakani Utawala!
Wanasiasa woote ni wachochezi wanao chochea Fikra mpya vichwani mwa wananchi ili wakiwaelewa wauondoe utawala ulio madarakani!.....
 
Pale wazalendo wanapobadilishiwa Jina na kuitwa wahaini!!!

Wananchi TUMEKATAA hadaa hii!!!

MKATABA Ule ni BATILI na FAKE, ufutwe haraka.
 
Back
Top Bottom