Lengo mojawapo la bajeti ya mwaka huu ni kusomesha kwa wingi Wataalamu Fani na Ujuzi Adimu/Maalum, wazazi shaurini watoto vizuri shahada za kusomea

Lengo mojawapo la bajeti ya mwaka huu ni kusomesha kwa wingi Wataalamu Fani na Ujuzi Adimu/Maalum, wazazi shaurini watoto vizuri shahada za kusomea

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Posts
36,902
Reaction score
52,001
Watu hawaelewi siri ya bajeti wengine hawataki kusikiliza kabisa matokeo yake hukosea kwenye maisha baadaye kuilalamikia serikali.

Bajeti hii moja ya malengo yake iliyoweka ni Kusomesha kwa wingi Wataalamu kwenye Fani na Ujuzi Adimu/Maalum

Wahindi na wawekezaji wa ndani na nje na wafanyabiashara hufuatilia sana bajeti kujua fursa ziko wapi.

Lakini hata watu wa kawaida hutakiwa kufuatilia bajeti nimechukua hicho kipengele ndani ya bajeti iliyosomwa na serikali

Hapo ina maana mtoto kama anataka kusoma na baadaye awinde ajira ni vizuri aombe kusoma fani za ujuzi adimu na maalumu akienda kujisomea chochote nje ya hapo shauri yake na mzazi wake.

Bajeti ni kitu sensitive na serious lakini tatizo watanzania walio wengi mitandaoni wanapenda vitu ambavyo sio serious ikiwemo humu JamiiForums.
 
usome kwa mwaka mmoja? shida ya bajeti zenu hazina projection ya miaka mingi. mwaka huu wako hapa mwaka mwingine wako kuleee. huoni utajikuta shule kila mwaka?
Kalaghabaho na ujuaji wako
 
YEHODAYA,

Budget ambayo hata serikali yenyewe huwa hawaifuati wewe mwananchi ujilipue?
Kwanza hizo taaluma adimu/ maalumu ni zipi?
 
Mi nachojua budget iliyopita ilichangiwa zaidi na sekta ya madini 17%ikifatiwa na sekta sanaa na burudani hapa maana yake kuna hela kwenye Sana'a na burudani kama ukiwekeza vizuri.
 
Mi nachojua budget iliyopita ilichangiwa zaidi na sekta ya madini 17%ikifatiwa na sekta sanaa na burudani hapa maana yake kuna hela kwenye Sana'a na burudani kama ukiwekeza vizuri
uko sahihi kabisa ina maana ukitaka kuanzisha biashara hilo eneo ni la kulifikiria umeisoma bajeti vizuri uko sahihi
 
No one cares about this budget mzee

Wananchi matumaini yao na hopes zao zote zilishakufaga..

Mjiulize sana aisee
Sema wewe Mimi hopes hazijafa nimeona fursa kibao ndani bajeti hiyo bajeti mipesa yote hiyo Kama wewe huoni fursa kwenye hiyo bajeti wewe hata Mungu hawezi elewa akusaidiaje
 
Unapotoa budget halafu hakuna mwananchi amefungua chombo cha habari kusikiliza,ujue kuna tatizo kubwa sana na serikali!

Hapo tawala za zamani,budget day ilikua nchi nzima inasimama,kila mtu anasikiliza kujua ameguswaje

Sasa hivi ni kinyume,no one cares,maana matumaini yalishakufa siku nyingi!

Bajeti ipitishwe,ikishatumika isikaguliwe,na pia itakayokaguliwa report zisijadiliwe bungeni kwa lazima!

Hapo una bajeti ya serikali au hela za mfuko binafsi wa mtu?

Kuna shida kubwa sana,na kuna financial malfucntion itatokea mtaumbuka in a out!

Ni kama Greece,asubuhi nchi ni stable financially,saa nne asubuhi financial system is in flames,jioni wananchi wapo barabarani hawana hela kwenye account benki zao!

I see this,mifuko ya hifadhi imeisha,hazina imeisha,mashirika ya umma yameisha,bandari imeisha,TRA imeisha maana hakuna uzalishaji wowote nchini,mabenki yamekonda kama minyoo....ni one day tu mabenki yote asubuhi saa nne yata declare bancrapy deposits zetu zote zitaenda na maji,then nchi inakufa na njaa maana hakuna hela ya kununua chakula maana watu hawana hela za ku draw benki na kutumia.

Greece ilikua ni tatizo la kufoji data za uchumi na mifumo ya kihela,reality striked,the country went into flames mpaka Germany ikakopesha watu wasife njaa!
 
Umejaribu kufuatilia walosoma Petroleum Engineering?....
Enzi zile wote waliokuwa wakisoma masomo ya Sayansi na ualimu walipewa mikopo wote ambacho kilikuwa kitu ok Rwanda wanasomesha Sana Tena bure wanasayansi sio kwa ajili ya soko la ndani Ni kuwinda soko la nje ya Nchi kwa lengo la kuwa exporters wa wataalamu wa fani adimu serikali inasaidia kusomesha Halafu waliosoma wanajiongeza

Digrii hizo hutakiwi kuangalia soko la ndani tu ingia mitandaoni saka ajira za hiyo degree nchi za Afrika Mashariki,kusini Kati na kaskazini ,saka nchi za uarabuni nk ukikaa tu una shinda mtandao wa jamii forums na ku chat ujinga magroup ya watsap hata hiyo digrii ikiwa na demand Hapo Uganda tu itakudodea
 
Wewe roho ya umaskini inakuita na imeshakufikia.Bajeti imejaa fursa kibao huzioni .Ok it is ok for you to die poor you have chosen that way go ahead

Masikini?

Mimi masikini?

Are you listening to yourself bro?

I'm not one of 'em!

Government can never help you on anything!

Budget ya serikali ni budget ya serikali sio yako!

Hufanyi kazi,hufanyi biashara,hutoi jasho lako kwa nguvu zako,no one gives you shit!

Hii concept ya kusema serikali eti "inatoa fursa" ni concept ya chooni and shitty way of thinking!

Yaani the whole country ni welfare state,waiting for government to give out money,aisee!
 
Watu hawaelewi siri ya bajeti wengine hawataki kusikiliza kabisa matokeo yake hukosea kwenye maisha baadaye kuilalamikia serikali.

Bajeti hii moja ya malengo yake iliyoweka ni Kusomesha kwa wingi Wataalamu kwenye Fani na Ujuzi Adimu/Maalum

Wahindi na wawekezaji wa ndani na nje na wafanyabiashara hufuatilia sana bajeti kujua fursa ziko wapi.

Lakini hata watu wa kawaida hutakiwa kufuatilia bajeti nimechukua hicho kipengele ndani ya bajeti iliyosomwa na serikali

Hapo ina maana mtoto kama anataka kusoma na baadaye awinde ajira ni vizuri aombe kusoma fani za ujuzi adimu na maalumu akienda kujisomea chochote nje ya hapo shauri yake na mzazi wake.

Bajeti ni kitu sensitive na serious lakini tatizo watanzania walio wengi mitandaoni wanapenda vitu ambavyo sio serious ikiwemo humu JamiiForums.
Kuna kozi inabidi zifutwe hapa TZ
 
Waulize waliokimbilia kusoma petroleum engineering wako wapi leo, kamwe usisome kwa kufuata sera za CCM kwakua siku zote hua hazina dira wala mwelekeo.
 
Back
Top Bottom