lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,571
- 35,475
Tanzania ni Taifa la ajabu sana sijawahi kuona. Dunia inatushangaa na vizazi vijavyo vitakuja kutushangaa. Hivi lengo ni kuwapata viongozi au lengo ni usahihi wa kujaza FOMU? Kwanini imekua ni kama mtihani fulani hivi kwamba mtu akikosea kujaza FOMU anaondolewa kwenye nafasi ya kugombea?
Kwa Nini kusiwe na FOMU nyingi tu katika ofisi za Tume na ziwe ZIKIUZWA. Mgombea aelekezwe jinsi ya kujaza na ikitokea akakosea anunue FOMU nyingine, kwani shida iko wapi? Hata hivyo kwa nini wanaokosea wote ni kutoka vyama vya Upinzani tu? Kwa Nini Tume imeweka mitego kwenye Fomu.
Kwa nini umnyime mgombea haki ya kugombea ikiwa kakosea kujaza FOMU tu, kwa Nini uwanyime wananchi haki ya kumchagua mgombea wanaemtaka kwa kumkataa jina lake kwa sababu tu kakosea kujaza FOMU, kwa nini kusiwe na nafasi ya kupewa fomu nyingine hata kwa kuinunua?
Saa nyingine huwa najisikia mnyonge kuwa Mtanzania. Ni nchi pekee Duniani mgombea akikosea kujaza fomu hana nafasi ya kusahihisha na anaenguliwa kabisa. Halafu hebu fikiria mtu Kama Tundu Lissu kweli anaweza kukosea kujaza Fomu. Iko miaka kuna watalii watakua wanakuja kutangalia au kututazama sisi Watanzania kama Ni binadamu halisi au nusu binadamu nusu wanyama.
Anakua amepoteza Haki yake na wanaompenda wanakua wamepoteza Haki yao ya kumchagua.
Mungu ingilia Kati.