Uchaguzi 2020 Lengo ni kuwapata viongozi au lengo ni usahihi wa kujaza fomu?

Uchaguzi 2020 Lengo ni kuwapata viongozi au lengo ni usahihi wa kujaza fomu?

Inasikitisha sana ila tukikua tutaacha. Ni kama wakati ule tulivyokuwa tunaporana hata saa za mikononi, leo hii hamna mwenye time nazo.

Jiulize kwa nini zoezi limewekwa siku moja tu? Kwa nini siyo wiki au hata wiki mbili kiasi kwamba kama kuna mapungufu wahusika wajulishwe wayarekebishe?
Ni sawa. Lakini hata hiyosiku moja ingetosha kurekebisha suala kama la pichae
 
Pengine nimechelewa kulileta hili, ila Tume ikiona lina umuhimu bas busara itumike kama ilivyotumika kwa wagombea urais..
Huko kwenye ubunge ndio vituko kabisa, bila kuangalia pia sifa za mgombea ubunge kwa mujibu wa katiba ni pamoja na kujua kusoma na kuandika basi. Sasa tunatarajia kwamba mtu mwenye literacy ya level hiyo kukosea mara moja au mara mbili iwe ni jambo la kawaida...

Ningeomba tume itumie busara zaidi hasa kwa level ya wabunge na madiwani kwenye suala la kujaza form isipokuwa pale kwenye maswala ya msingi sana ndio mbunge apitishwe.

Haiwezekani eti mgombea kakosea kuweka Capital letters, Punctuation, Comma, etc ndio useme hafai kuwa mgombea.... huu ni uharamia.

Kama taifa lazima tulinde demokrasia yetu kwa namna ambayo inawapa wananchi fursa ya kuchagua na kuchaguliwa tena kwa nafasi kubwa zaidi.

Kusema ukweli kabisa inakera sana kuona jambo kama hilo linaweza wanyima wananchi haki ya kuchagua kiongozi wanaemtaka...
Naangalia ya Mtama, Morogoro mjini, na Ruangwa... nasema hapana.. something is not right.! we can do better!
 
Back
Top Bottom