Leo huenda ikawa siyo siku nzuri kwa Rais wa TFF Malinzi kwani Mapacha hawa kuchukua Fomu rasmi

Leo huenda ikawa siyo siku nzuri kwa Rais wa TFF Malinzi kwani Mapacha hawa kuchukua Fomu rasmi

Nyinyi "wadau" ndio mnaharibu michezo nchini
Mdau ndio cheo au wadhifa gani kwenye mchezo?
Wadau! Wadau ukute mwanao ni mkata viuno stejini halafu unajifanya una uchungu na soka!!
Sio mwanae tuu hata yeye ni mkata viuno kwenye Casinos.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Mkuu hili ni Swali ambalo kiuhakika hata Mimi najiuliza sana kwani hakuna Watu ambao wana Njaa iliyotukuka kama hawa Wajumbe wapiga Kura na kuna Mdau mmoja ambaye yupo karibu na tunayempinga na kumtaka apigwe chini anasema kuwa kwa Hela / Pesa / Fedha aliyoipiga Jamaa anaweza kuwahonga Wajumbe wote Gari mpya aina za IST na akawapa kila mmoja Hela ya Mboga Tsh Milioni Moja Moja.
Mpira pesa. Sasa kama nyie hamna pesa mnalialia nini sasa au mnataka mkishapata huo uongozi muanze kutuibia kwanza then soka baadae?

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Kwa hiyo ukishacheza mpira ndio kujua leadership na management ya mpira sio?only in Tanzania ndio maana soka letu haliendelei sababu mmejaa unafiki na hamjui ñini hasa mnataka.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app

Sijui unazungumza vitu gani, team kubwa za huko Ulaya na South Amerika Viongozi wao wana backgrounds zipi, labda tuanzie hapo - awaleti mambo ya siasa na umangimeza na mambo ya kujuana ili washirikiane kupiga hela ndefu kwa kutumia ujanja janja tu au wewe hilo ulijui? Hicho ndicho kinaendelea hapa kwetu ndiyo maana hatufiki mbali kimpira - we keep going in circles.
 
Sijui unazungumza vitu gani, team kubwa za huko Ulaya na South Amerika Viongozi wao wana background hipi, labda tuanzie hapo - awaleti mambo ya siasa na umangimeza na mambo ya kujuana ili washirikiane kupiga hela ndefu kwa kutumia ujanja janja tu au wewe hilo ulijui?
Tenga na wengineo waliocheza mpira then wakawa viongozi walileta mafanikio gani tofauti na Malinzi?

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Katika kile kinachoonyesha kwamba Watanzania hasa wapenda Soka / Kandanda wamechoka na Uongozi / Utawala wa sasa wa Rais wa TFF Jamal Malinzi hatimaye leo asubuhi mida ya Saa 5 Viongozi wanaotakiwa kuiongoza TFF wanachukua Fomu rasmi ili kupambana na kumtoa Malinzi madarakani.

Na ili kuonyesha kuwa huenda hawa Watu wawili wakawa ni mwiba mchungu kwa Rais wa TFF Jamal Malinzi ni kwamba wamepata baraka zote kutoka kwa Wadau wengi wa Soka nchini na hata Serikalini na kuna uwezekano mkubwa mno kwa jinsi mikakati yote ilivyopangwa huu ukawa ndiyo mwisho wa Jamal Malinzi ndani ya TFF.

Watu hao ni Mchezaji na Nahodha wa zamani wa Yanga FC, Mchambuzi mahiri wa Soka, Mdau mkubwa wa Soka na Msomi mzuri wa masuala ya Biashara na Uongozi Ndugu Ally Mayai Tembele ambaye amepangwa kugombea nafasi ya Urais wa TFF na Makamu wake inasemekana amepangwa kuwa ni Mchezaji wa zamani wa Kiungo wa Simba SC na aliyekuwa na mafanikio makubwa, Mdau mkubwa wa masuala ya Soka na Kiongozi wa zamani wa TFF Mzee Mtemi Ramadhan.

Kinachowafanya hawa Watu akina Ally Mayai na Mzee Mtemi Ramadhan wakubalike na Wadau wengi wa Soka / Mpira nchini Tanzania ( GENTAMYCINE inclusive ) ni kwamba kwanza wamecheza mpira katika Kiwango cha juu kabisa hivyo wanajua nini maana ya Soka na Maendeleo yake. Lakini pia hawa Watu wawili ni kweli kuwa mmoja wapo ni mwana Yanga na mwingine ni mwana Simba ila uzuri wao ni kwamba huwa hawana Unafiki na hawatangulizi mapenzi kwa hivyo Vilabu vyao pindi vinapokuwa na matatizo bali wao husimamia Ueledi na Ukweli hasa katika Utendaji wao.

Watoto wa mjini tunasema kwa Kauli mbiu yetu mpya isemayo “ Malinzi pisha njia wenye Mpira wao wamekuja “. Nianze tu kutoa pongezi zangu za dhati kwa hawa Wadau wangu wakubwa wa Soka Kaka yangu Ally Mayai Tembele na Mzee wangu Mtemi Ramadhan kwa kuamua kuwa Viongozi wa TFF na nina uhakika kama Wajumbe wa TFF wataacha Upopoma / Upumbavu wao basi Rais mpya wa TFF atakuwa ni Ndugu Ally Mayai Tembele na Makamu Rais mpya wa TFF ni Ndugu Mtemi Ramadhan.

Nami namalizia kwa kusema “ Malinzi pisha njia wenye mpira wao wamekuja “.

Nawasilisha.
Mkuu mawazo yako ni mazuri ila naomba kukuuliza unawajua wapiga kura ambao wapo madarakani kwa sasa? Unajua km malinzi ndio kaengua wote wasiompenda akaweka watu wake???
 
Mkuu mawazo yako ni mazuri ila naomba kukuuliza unawajua wapiga kura ambao wapo madarakani kwa sasa? Unajua km malinzi ndio kaengua wote wasiompenda akaweka watu wake???

Mkuu ndiyo maana naona kuna haja ya Serikali kuunda tume huru kama iliyo undwa kuchunguza mchanga wenye madini - uendeshaji wa sekta ya SOKA nchini una matatizo makubwa sana Serikali hisifumbie macho kuchunguza usanii ambao unaendelea katika kukuza soka nchini - tusikubali teuzi za chombo muhimu kama TFF kiendeshwe kama mali ya ukoo, watu hao hao wanakuwa recycled as if hakuna Watanzania wengine wenye uwezo wa kuendesha chombo hiki kizalendo, kama vipi wanzishe Kampuni zao binafsi za mpira kama Azam alivyo fanya ambako wanaweza kufanya wapendalo na sio kudumza Taifa letu kimpira kupitia mgongo wa TFF.
 
Kwa hiyo ukishacheza mpira ndio kujua leadership na management ya mpira sio?only in Tanzania ndio maana soka letu haliendelei sababu mmejaa unafiki na hamjui ñini hasa mnataka.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
Kuna utofauti mkubwa sana kwa mtu aliyesoma leadership and management anapokuja kupractise alichokisoma na yule aliyekuwa anapractise bila hata kwenda shule. Soka letu haliendelei kweli kutokana na watu kama wewe,unayempinga mtu bila hata kuuona wasifu wake.. OMBA WASIFU WA WAGOMBEA HALAFU UPIME, Umeshasikia jamaa atatoa pesa kuhakikisha anarudi,kwanini u-force kurudi na usisubiri kurudishwa kwa mambo mazuri uliyofanya na mabaya machache?????
 
bf03a36022e802df2fc77a45e7b84abc.jpg

Malinzi Out....haiwezekani mchezaji mwenye kiwango cha hali ya juu kama Nyosso alipewa adhabu ya uonevu
 
Kuna utofauti mkubwa sana kwa mtu aliyesoma leadership and management anapokuja kupractise alichokisoma na yule aliyekuwa anapractise bila hata kwenda shule. Soka letu haliendelei kweli kutokana na watu kama wewe,unayempinga mtu bila hata kuuona wasifu wake.. OMBA WASIFU WA WAGOMBEA HALAFU UPIME, Umeshasikia jamaa atatoa pesa kuhakikisha anarudi,kwanini u-force kurudi na usisubiri kurudishwa kwa mambo mazuri uliyofanya na mabaya machache?????
Malinzi tushamuona sasa hiyo ni kazi yenu kuweka wasifu wa huyo mgombea wenu mnaempigia porojo hapa.

Sent from my Vodafone Smart Tab 3G using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom