Leo hujaenda kanisani? Kwa nini?

Namshukuru Mungu toka nimepata akili na kujielewa hadi sasa nina 30+ nimekuwa naiheshimu sana hii siku...sijawahi kuona sababu ya msingi iliyonifanya nisihudhurie ibada ila kabla sijaowa kwa7bu ya ujana kuna siku moja moja nilikuwa naingia kwenye dhambi mbaya so nilikuwa sihudhurii ibada ila miaka minne sasa hakuna siku niliyokosa,vijana tujiweke karibu na Mungu kwa kumuabudu inavyopasa si'ajabu mambo mengi tunayaona magumu kwa7babu tumejitenga nae mbali.fikiria mtu mwaka mzima,mwezi mzima au wiki nzima hakuna lolote baya lililokupata na dhambi katazwa karibia zote unazifanya ila japo siku moja tu tena kwa masaa kadhaa unashindwa kumuabudu aliyekuonea huruma{mie ni Mkatoliki ibada inakuwa masaa 2 tu},tuwe na tahadhari ndugu zangu hatujui siku wala saa atakayokuja mkuu wa nyumba!
 
Wengine tulikosa nauli na sadaka, kwa hiyo tukawa tunasikiliza ibada kupitia Radio
 
Mi sienda kwavile sina sadaka, maana ukienda halafu usitoe sadaka mchungaji anakasirika sana.
 
Ujumbe wa leo kutoka kwenye somo la injili.

Mpe ya kaisari yaliyo ya kaisari, Na mpe MUNGU vilivyo vyake MUNGU.
Aiseee ujumbe murua apo padri alirudia mara mbili ya kaisari ni ya kaisairi na ya Mungu ni ya Mungu
 
Hivi ya kaisari ni yapi ayo na ya Mungu pia ni yapi? Msaada tafadhali kabla sijakomenti kwanini leo sijaenda chapel
 
Nipo baa nakunywa pombe. We umeenda? Kwa nn umeenda?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…