Leo katika historia na Dola la Papa

Leo katika historia na Dola la Papa

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Dola la Papa

Dola la Papa lilikuwa nchi huru chini ya himaya ya Papa kuanzia miaka ya 700 hadi 1870.

Chanzo chake ni uvamizi wa makabila ya Wagermanik uliobomoa Dola la Roma upande wa magharibi wa Bahari ya Kati. Wenyeji, wengi wao wakiwa Wakristo Wakatoliki, walimkimbilia Papa kama kiongozi wao atakayeweza kuwasaidia katika matatizo.

Baadaye Wafaranki walikubali kumuachia Papa mamlaka ya kisiasa juu ya maeneo mbalimbali nje ya Roma. Polepole maeneo yaliongezwa hata kufikia mikoa 3 na nusu ya Italia ya leo: Lazio, Umbria, Marche na sehemu ya Emilia-Romagna.

Dola lilikoma tarehe 20 Septemba 1870, jeshi la Italia lilipoteka mkoa na mji wa Roma, isipokuwa mtaa wa Vatikano.

Kwa mapatano ya tarehe 11 Februari 1929, badala yake ilianzishwa Mji wa Vatikani, nchi ndogo kuliko zote duniani (kilometa mraba 0.44, lakini huru ili mamlaka ya kiroho ya Papa isiingiliwe na watawala wa dunia kama ilivyotokea zamani.
 
Kwa maelezo haya basi Utawala wa Papa ulianza kirahisi sana!!..
 
Ndio maana yake hawa hawatumiagi vita sana
Ni washawishi wakubwa kwa mdomo tu na wanaeleweka mkuu
Hapana mkuu historia ya dola ya Papa haijaweza survive mpaka sasa kiurahisi namna hiyo!.. Zile crusade wars zote zilikuwa kwa maslahi ya ukristo na kusimika nguvu ya Papa. Kuuwawa kwa Galileo kulikuwa ni kupingana na msimamo wa kanisa!.. Watu kuuwawa kwa ajiri ya kukutwa wana miliki biblia ilikuwa ni kuhakikisha nguvu ya kanisa inabaki. Historia ya Papa ni kubwa sana. Kama mkatoliki unaweza kwenda duka la kanisani omba kakitabu fulani kadogo kanaitwa "PAPA NI NANI?" au "MJUE PAPA".. (nimesahau title).
Katoliki tumepitia mengi mpaka leo hii unaona tunaheshimika na Papa wetu!..Amina.
 
Sio kweli ila kiuhalisia hawa ni watu wenye ushawishi mkubwa mno kwa kutumia mdomo
 
Hapana mkuu historia ya dola ya Papa haijaweza survive mpaka sasa kiurahisi namna hiyo!.. Zile crusade wars zote zilikuwa kwa maslahi ya ukristo na kusimika nguvu ya Papa. Kuuwawa kwa Galileo kulikuwa ni kupingana na msimamo wa kanisa!.. Watu kuuwawa kwa ajiri ya kukutwa wana miliki biblia ilikuwa ni kuhakikisha nguvu ya kanisa inabaki. Historia ya Papa ni kubwa sana. Kama mkatoliki unaweza kwenda duka la kanisani omba kakitabu fulani kadogo kanaitwa "PAPA NI NANI?" au "MJUE PAPA".. (nimesahau title).
Katoliki tumepitia mengi mpaka leo hii unaona tunaheshimika na Papa wetu!..Amina.
Hiki ulichoandika hapa ni stori za wabaya wa hili kanisa tu ila hazina ukweli wowote
 
KWa kifupi wakatoliki tuna akili sana.
Kwani wao ninani mpaka wawe na akili kuliko wengine
Wao husaidia sana watu wasiojiweza na wanajikuta wakipendwa tu na watu
Nchi zenye vita kama pakistani, afghanistan, iraq, siria, palestina zinapokea sana misaada mikubwa kutoka kwa hili kanisa huku misaada yao ikilenga watoto wanawake na vijana walioathirika na vita
 
Hiki ulichoandika hapa ni stori za wabaya wa hili kanisa tu ila hazina ukweli wowote
Nilichokiandika nusu yake kimeandikwa kwenye kitabu hicho nilichokwambia!!..Mimi ni Mkatoliki na nilikinunua hicho kitabu sasa unataka nikuaminishe vipi!, wakati kanisa lenyewe tunakubali maovu tuliyowahi kufanya na wahusika wakiwa mapapa!.. Hebu kitafute hicho kitabu kwenye duka la kanisa Katoliki sio mtaani!..
Usione aibu kukubali tulifanya madhambi huko nyuma, ni kitu cha kawaida kilitokea kwa ajiri ya kuja onyesha kizazi hiki maovu hayakuwahi saidia!.
 
Na hiyo ndiyo silaha yenyewe. Na ndiyo iliyoangusha dola ya Roma. Walikuwa na mikuki na ngao, wakatoliki wakawa wanaenda kusaidia masikini.

Watu wa Roma wakaona dini mpya ina amani kuliko watawala wa dola ambao wanatumia silaha kuamrisha watu.

Hivyo wanaosema wakatoliki tuna ushawishi ninakubaliana nao, na hiyo ndiyo akili yenyewe.
 
Hiki ulichoandika hapa ni stori za wabaya wa hili kanisa tu ila hazina ukweli wowote
Mkuu Eden acha ubishi mm ni mkatoriki nakubali hilo, mapadri wanakili hilo.. Labda hujui histori ya RC, Mkuuu kanisa katoriki limepitia vpind vitatu ambavyo ni..
Kanisa linaloteseka/ lililoteseka
Hiki ni kipindi ambapo kanisa lilidhurumiwa hususani katika karne zake za mwanzo.
Kanisa lililokuwa linatesa/linadulumu
Hiki kilikuwa ni kipindi ambapo lilikuwa linatoa adhabu kwa mtu yeyote aliyepotosha mafundisho ya Kanisa au aliyefundisha kinyume na mafundisho ya Kanisa. Lilikuwa linaua na kudhani kuwamba Mungu anafurahia vitendo hivyo. Lilidhani Mungu anahitaji kutetewa na binadamu
Lakini lilifanya hivyo ili kulinda mafundisho na imani sahihi ya Kanisa,
Ni katika kipindi hiki, cha pili ambacho Kanisa limekipitia, ndipo hao wenzetu waliotambuliwa kkuwa ni wazushi walikabiliwa na mateso hayo ambayo yalisimamiwa na Kanisa kwa lengo la kulinda imani yake. Hivyo mateso hayo waliyoyapata katika kipindi hicho ni adhabu sahihi waliyostahili kwa sababu walionekana kuwa walizusha mafundisho ya uongo yanayopingana na mafundisho sahihi ya Kanisa.
nyakati za maaganzo mapya.
Baada ya kufanya mambo kama hayo yliyofanika katika kipindi cha pili, kanisa ilipata ufunuo zaidi likagundua kuwa mambo hayo ya mateso yalikuwa ni mawazo batili ya binadamu mwenyewe. Liligundua kuwa Mungu wa amani na Baba wa watu wote hapendi vita au madhulumu. Basi likaachana na mambo hayo ya mateso dhidi ya watu waliopotosha mafundisho sahihi ya kanisa.
 
Nilichokiandika nusu yake kimeandikwa kwenye kitabu hicho nilichokwambia!!..Mimi ni Mkatoliki na nilikinunua hicho kitabu sasa unataka nikuaminishe vipi!, wakati kanisa lenyewe tunakubali maovu tuliyowahi kufanya na wahusika wakiwa mapapa!.. Hebu kitafute hicho kitabu kwenye duka la kanisa Katoliki sio mtaani!..
Usione aibu kukubali tulifanya madhambi huko nyuma, ni kitu cha kawaida kilitokea kwa ajiri ya kuja onyesha kizazi hiki maovu hayakuwahi saidia!.
Anaongea kwa ushabiki huku hajui kitu
 
Mkuu Eden acha ubishi mm ni mkatoriki nakubali hilo, mapadri wanakili hilo.. Labda hujui histori ya RC, Mkuuu kanisa katoriki limepitia vpind vitatu ambavyo ni..
Kanisa linaloteseka/ lililoteseka
Hiki ni kipindi ambapo kanisa lilidhurumiwa hususani katika karne zake za mwanzo.
Kanisa lililokuwa linatesa/linadulumu
Hiki kilikuwa ni kipindi ambapo lilikuwa linatoa adhabu kwa mtu yeyote aliyepotosha mafundisho ya Kanisa au aliyefundisha kinyume na mafundisho ya Kanisa. Lilikuwa linaua na kudhani kuwamba Mungu anafurahia vitendo hivyo. Lilidhani Mungu anahitaji kutetewa na binadamu
Lakini lilifanya hivyo ili kulinda mafundisho na imani sahihi ya Kanisa,
Ni katika kipindi hiki, cha pili ambacho Kanisa limekipitia, ndipo hao wenzetu waliotambuliwa kkuwa ni wazushi walikabiliwa na mateso hayo ambayo yalisimamiwa na Kanisa kwa lengo la kulinda imani yake. Hivyo mateso hayo waliyoyapata katika kipindi hicho ni adhabu sahihi waliyostahili kwa sababu walionekana kuwa walizusha mafundisho ya uongo yanayopingana na mafundisho sahihi ya Kanisa.
nyakati za maaganzo mapya.
Baada ya kufanya mambo kama hayo yliyofanika katika kipindi cha pili, kanisa ilipata ufunuo zaidi likagundua kuwa mambo hayo ya mateso yalikuwa ni mawazo batili ya binadamu mwenyewe. Liligundua kuwa Mungu wa amani na Baba wa watu wote hapendi vita au madhulumu. Basi likaachana na mambo hayo ya mateso dhidi ya watu waliopotosha mafundisho sahihi ya kanisa.
Huwa napendezwa na ukweli ulio uchi/usiopindishwa
 
Back
Top Bottom